Kwa mabingwa wa Tafsiri fasaha

Kwa wanaopenda kiingereza.Tafadhali naomba tafsiri ya maneno haya kwa kiingereza ambacho hakitabadili maana iliyopo katika kiswahili hiki:

"MAMA, HIVI MIMI NI MWANAO WA NGAPI KUZALIWA?"

Ukipata tushirikishane.

Maoni

  1. Bro bwaya hili swali nimesha ulizwa tena kama mara 2 mimi huwaga jibu langu ni
    "mom whose am l born to among your children have?,huo ni mtazamo wangu.

    JibuFuta
  2. maswali mengine bwana.
    wewe unataka ujue ni wangapi kwa kiigereza iliiweje? je tukikupa matokeo utayakubali yote? akisema alikuokota msituni? just found you in forest.
    vitu vingine vinahitaji imani ya kibiblia kuvijibu, yaani amini bila kuuliza maswali usijemkufulu mamako.

    kwakweli mimi sijui. ila wewe kkubali na amini kwamba huyo mama alikuzaa vinginevyoutaumiza kichwa kujua kwamba mama ashasahau.

    lakini kwa nini tumuulize mama tu na sio baba? kwa sababau mama ndo atuonyeshaye baba?

    samahani kwa kwenda nje ya mada MANENO YA MKOSAJI

    JibuFuta
  3. @Bwaya:Kwanini katika mambo yote ya kujua unataka kujua swala hili?

    JibuFuta
  4. Wajameni, kwani bwan'kaka hujui we ni wangap kuzaliwa kwenu hadi wataka mwuliza mamayo tena kwa kirengesa?
    Ama ni lazima afahamu kuwa ile ada aliyokulipia kusoma pale Namanyere praimari haikwenda bure?
    Kaka eh! Kwanini ulisahau kumwuliza mwalimu ticha pale klasi faivu?
    Tatizo linalotufanya tushindwe kukujibu, sie sote tu wageni maeneo hayo!
    Ni hayo tu!

    JibuFuta
  5. Wadau,

    Kisa cha kuuliza haya yote ni kutaka kuonyesha tu kwamba kiswahili chetu kina maneno ambayo hayana kiingereza chake.

    Wale jamaa wanaopenda kutuonyesha ubabe kuwa wanajua kiingereza kwa kusema eti aaah sina kiswahili chake, watambue kuwa hata kiswahili nacho chaja! Tukilee. Tukitunze. Tukitumie. Tujisikie fahari nacho. Tukikuze.

    Kuhusu mengine yanyojitokeza bado natafakari. Ila ni vizuri kuwa na imani na mama. Na baba pia. Mambo mengine ukiyachonoa sana hayasaidii.

    JibuFuta
  6. Jamani swali la Bwaya naona baadhi yetu hapo juu hatukuliewa. hakutaka kwa hakika kujua ni wangapi kwani hilo anaju. Swali lake ni la lugha na si la uadilifu, adabu na kadhalika. Tuwage wepesi kuelewa maana.

    JibuFuta
  7. "mom whose am l born to among your children have?" Huu ni ushahidi wa wazi kwamba kiingereza kina matatizo makubwa. Sina hakika kwa nini watanzania tunang'ang'ania luha tusiyoifahamu.Naona kama ukitumia tafsiri hii maana yake si tu kwamba inapotea, bali hata namna ya kuelewa kinachmaanishwa inakuwa haipo. Kazi kweli kweli.

    JibuFuta
  8. Bwaya nakupata,kidogo nijiume.
    Mwaipopo kuishia na neno na "ga" mfano alikwendaga.alikulaga,kuwaga,na kuna wale wenzentu wa kanda ya Ziwa wanaishia sana na "epo" kama nitokeepo,kujapo,naombapo huwa ni kiswahili sahihi?

    JibuFuta
  9. Edigio,

    Mimi hufikiri kwamba matumizi ya 'ga' ni muafaka kabisa. Ni suala la BAKITA kulingalia suala hili.

    'ga' ikiongezwa kwenye kitenzi huleta maana ya wakati endelevu, hali ya mazoea kama ilivyo kwenye kiingereza. Ukiongeza 's' kwenye verb.

    Mfano, anakulaga=he eats, anakwendaga=he goes.

    Inaleta maana nzuri zaidi kuliko ilivyo kwa sasa.

    Labda Mwaipopo mwenyewe atupe maelezo mazuri ya kisarufi. Mimi siajsoma lugha.

    JibuFuta
  10. Jamani sikuishia hapo. Nilikuwa nafanya kautafiti kadogo ili nije tena.

    Kabla sijaendelea niungane na bwaya hapo juu. Kwa kuwa kunaushahidi wa kutosha kuwa Kiswahili kiko karibu zaidi na viluga vya kibantu kuliko kiarabu basi Kiswahili ni kibantu. na kama Kiswahili ni kibantu basi matumizi ya -ga kama alivyosema bwaya hapo juu ni sahihi. Ukichunguza lugha nyingi za kibantu wakati uliopo endelevu huwekwa -ga. chunguza kihehe na kinyakyusa kwa mfano. na vingine vingi.

    Kwenye mada yetu sasa. Swali hili liliponitoa jasho nikaona nimuulize rafiki yangu mzungu. Nae kaiona shida.Bahati njema anajuajua kidogo Kiswahili cha kuendea kariakoo.


    Kama mjuavyo mimi ni linguist.Niliwahi kusoma translation course. Hili ni tatizo miongoni mwa matatizo ya fasili - maneno ama miundo yenye kuegemea katika utamaduni wa lugha husika. hata hivyo panapo nia ya kutafsiri lazima njia itafutwe. hasa ni kwa nia ya kujifunza kuliko kujifanya kujua.

    Nilimuuliza mzungu wangu huyu hivi:
    i have a question that seemingly gives many of us a headache. it is about asking for one's ordinal number of your birth. Suppose you are 4 in total from the same mother and you don't know exactly whether you are 1st, 2nd, 3rd or 4th (imagination) and you want to ask say your parents as to what is your ordinal number. In Kiswahili we have a version of it which is: "MAMA, MIMI NI WA MWANAO WA NGAPI KUZALIWA?" We cant get one sentence that is a correct translation of the same. My friends and i end up with funny sentences. Do we have one sentence to ask for that?

    Akanijibu:
    In answer to your question, I would say there are several ways to ask. "Mom, what child am I?" Or "which child am I?" But those questions wouldn't exactly prompt someone to answer with the order of your birth. Alternatively you could ask "Am I the first born?" In which hopefully unless it was true that you were the first born child, your mother would say, no you're the second or third child, etc.

    I can see your problem, as I would translate that question to "Mama, I am of which birth?" or "I am how many born?"

    Does that solve any problems or win any bets?

    Nami nauliza vipi inasaidia saidia?

    Maswali haya yanaleta changamoto

    Alamsiki binuur

    JibuFuta
  11. Asante sana Mwaipopo. Mfano uliouonyesha ni wa kuigwa na kila mwanablogu.

    Nimeupandisha mchango wako kwa maoni zaidi.

    JibuFuta
  12. Nimewapata wakuu

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?

Pay $900? I quit blogging