Je, kuna Mungu? - Mchango wa Nuru Shabani

Kuna wachangiaji wananiandikia kwa barua pepe. Sijui ni kwa nini wanataka tujadiliane sirini. Nadhani tukijadili waziwazi inapendeza zaidi kwa faida ya wasomaji wengine.

Hapa ninao mchango wa Nuru Shabani kupitia kisanduku cha maoni. Kwa kuheshimu mchango wa msomaji huyu, naomba niupandishe hapa uusome.

"...Ningependa kuungana na Kamala kuwa hakuna kitu kinachoitwa Mungu,kama wengi tulivyoambiwa.
Zamani kabla hawajaja wakoloni(wazungu na waarabu) hakukuwa na kitu kinachoitwa Mungu,wao waliamini ktk Nguvu kuu.Ndiyo maana utakuta wengine waliamini ktk miti wengine katika majabali,na kikubwa ndugu zangu ieleweke wengi wa watu wa zamani waliamini zaidi katika kanuni za kimaumbile ndiyo ilikuwa msingi wao.

Kwa mtazamo wangu wengi hatumwelewi mungu sana tunachofanya ni kujenga hofu kwa Mungu,linapokuja suala la kutaka kumjua huyo mungu kwa undani utaambiwa unakufuru,sasa mi huwa ninajiuliza iweje utake kujua asili za aliyetuumba uambiwe unakufuru? Haingii akilini umuulize mzazi wako asili yake wapi akuambie unakufuru.
kwa kukazia mchango wa kamala kuna wakati mtu akishindwa jambo husema ni mpango wa mungu,lkn ukichunguza utagundua kuna baadhi ya kanuni za kimaumbile hazikufutwa ndiyo maana likashindikana hilo jambo.

ninaweza kukubaliana na wanasayansi kila kitu kinaendeshwa na kanuni za kimaumbile na kanuni hizo zinaratibiwa na nguvu kuu ambayo wengi tunaiita ni mungu.
Mi nimejaribu sana kuongea na watu wengi ambao tunaona wamefanikiwa kikubwa wengi ukiwachunguza utaona walifuata kanuni za kimaumbile zaidi ingawa wengi husema mungu amenisaidia kufika hapa.

Pia hata ukienda makanisani na misikitini hafundishi ukweli kuhusu huyo mungu wengi tunamuoona ni mungu wa hasira mungu wa kulaani mungu wa kuwapa mikosi,mungu wa kuadhibu.Hivi jamani ni nani ambaye anaweza akaumba kitu na kisha akakiaadhibu?sanasana atakuwa anakifanyia marekebisho kionekane ni bora zaidi.Tumeona wagunduzi wa vitu mbalimbali duniani huzidi kuviboresha vile vitu walivyovivumbua.Huku unaambiwa ameadhibiwa na Mungu, mi nadhani kuna haja ya kulitazama upya suala la mungu." Anahitimisha.

Wewe unasemaje ndugu msomaji? Unakubaliana naye? Unapingana naye? Karibu tujadiliane.

Maoni

  1. Ningeanza kwa kukuuliza Nuru: Kwa nini unafikiri ipo nguvu inayoratibu kanuni za maumbile?

    JibuFuta
  2. Ni kweli akili za binadamu na Mungu tofauti sana na mambo ya rohoni ni siri kubwa sana.
    Mungu yupo wala huhitaji mambo mengi hata ukiandika tarehe tu unakubali kwamba Yesu alikuwepo Miaka 2000 iliyopita na alitokakwa Mungu, kama huamini kwamba Mungu yupo pinga kwanza kukubali kuandika tarehe.

    Sasa siku ukutane na Mungu na ulisema hayupo, shauri yako!

    JibuFuta
  3. Mbilinyi bado kuna utata juu ya tarehe ya kuzaliwa kwa huyo Yesu km ni 25/12/01 au vinginevyo? waislamu, wayahudi nao wanamifumo yao ya kuhesabu!
    kunna kalenda ya Gregory (Gregorian calender) na za wengina kama julius nk, kwa hiyo tarehe isikutishe sana

    JibuFuta
  4. Mbilinyi bado kuna utata juu ya tarehe ya kuzaliwa kwa huyo Yesu km ni 25/12/01 au vinginevyo? waislamu, wayahudi nao wanamifumo yao ya kuhesabu!
    kunna kalenda ya Gregory (Gregorian calender) na za wengina kama julius nk, kwa hiyo tarehe isikutishe sana

    JibuFuta
  5. Kwa mtazamo wangu naona mungu yupo ambae ndio nguvu ikaribiwayo kwa kanuni za kimaumbile na upendo usio na mashaka.

    Na dini ni mtazamo maoni yalio onekana ya hekima na yanafaa zaid kwa kipindi fulan na watu husika na wakaamua kua iwe sehem ya maisha yao na kurithisha kizaz baada ya kizaz

    Kwahivyo linapootokea jema lakuongezwa katika iman au maon au mapendekezo ambayo yalichaguliwa kufwatwa (dini) wanaona ni dini mpya imeibuka ila jambo ni lilelile

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia

Pay $900? I quit blogging