Machapisho

Udhaifu wa sayansi (1)

Haya tuendelee. Tunahitaji aya nyingi kufafanua dhana ya sayansi. Kwanza nijitete kwamba sina msamiati wa kutosha kukwepa maneno yanayoitwa ya kisayansi ila nitajaribu kadiri niwezavyo. Kwa uchache sana, na katika lugha rahisi zaidi, sayansi ni namna ya upatikanaji wa maarifa kwa njia ya utafiti. Utafiti hapa humaanisha majaribio ambayo hukusudiwa kuchunguza na hatimaye kuthibitisha ama kukanusha bashiri ya kisayansi. Sayansi hutumia mbinu katika kuchunguza dhana, ili kuongeza maarifa ama kurekebisha maarifa yaliyopo. Huanzia katika ukusanyaji wa ushahidi unaochunguzika, unaopimika, na wenye chanzo mahususi kinachokubaliana na ufahamu wa kawaida. ( Sina masamiati sahihi sana ). Ushahidi huo, ndio kile kinachoitwa data, ambazo hupatikana kwa majaribio ambapo bashiri hujengewa hoja ili kufanyika maelezo ya dhana iliyokuwa ikichunguzwa. Majaribio haya hupangiliwa kitaalamu kwa kutumia vibadiliko (variables) ili kuzijaribu bashiri za awali. Majaribio haya hufanyika katika ma...

Utangulizi wa hoja: Tumetokea wapi?

Kujielewa ninakokuzungumzia, kunahusisha na uelewa wa mambo kadhaa yanayoaminika kuongoza maisha ya viumbe katika ulimwengu ( pamoja na dunia) tunamoishi. Kwamba sisi binadamu tulitokea wapi na tunatafuta nini hapa duniani. Huko ni kujielewa. Ulimwengu na viumbe vilitokea wapi? Swali kama hili si rahisi sana, pamoja na umuhimu wake katika kujielewa. Yapo mawazo mengi yanayojaribu kutafuta uhalali wa fikra kadha wa kadha kuhusu chanzo hasa cha ulimwengu wenyewe pamoja na uhai na maisha ya viumbe hai na visivyo hai katika ulimwengu huu. Mawazo haya yanaweza kuganywa katika makundi makubwa mawili: Wanaoamini zaidi pasipo ushahidi, na wanaojaribu kutumia akili zao katika kutafuta ushahidi wa mambo haya. Wale wa kwanza, kwa wingi wa idadi, ni wanadini. Wale wa pili, ni wanasayansi. Mwanadini, anatafuta kujenga imani zaidi hata kama haielezeki. Mwanasayansi anatafuta ushahidi unaoelezeka. Katikati ya hao wawili, wapo wengine ambao kazi yao ni kuhoji uhalali wa mahitimisho yanay...

Laiti ningeweza kuisemea nafsi vizuri!

Natamani sana kuandika kila siku. Natamani ningekuwa na shughuli moja tu ya kusema yaujazayo moyo. Kusema na kusema. (Hakuna kitu nafurahia kama kuyatoa yaliyopo moyoni). Huwezi kuyatoa kama hayapo huko yanakodhaniwa kutokea. Huwezi kusema kama huna cha kusema. Huwezi kuandika kama huna cha kuandika. Mimi nina agenda moja kubwa: Kujielewa. Natafuta namna nzuri ya kuiweka agenda hii mahala pale. Kuisema mpaka isemeke. Lakini tatizo kubwa ninalokabiliana nalo ni mwingiliano wa majukumu. Majukumu mengine hayasubiri kama ambavyo wengi wetu tunajua. Majukumu ya kitumwa tumwa hivi, kwamba tuwasikilize wenzetu watujaze yale yanayoitwa maarifa yapatikanayo katika taasisi ziitwazo 'shule'. Nadhani hatujafika mahala tukakubaliana kwamba majukumu haya yanaweza kusubiri. Hivyo ninawajibika kwayo, walau kwa sasa. Pamoja na ukosefu wa muda (hivi kweli ni ukosefu ama udhaifu wa mpangilio wa muda?) wa kubwabwaja hapa, huwa nafidia kwa kujibwabwajia mwenyewe. Nadhani kujisemea kuna nguvu...

Unaujua uongo wa Charles Darwin?

Picha
Charles Darwin ni yule jamaa aliyepata kuandika ile nadharia maarufu ya "Natural Selection" . Nadharia hii kwa muda mrefu imekuwa ikiaminika kutoa maelezo ya kweli kuhusu namna viumbe vilivyoweza kuwa hivi vilivyo leo hii (organic evolution). Kwamba viumbe havikuumbwa bali vilibadilika kwa kile kinachoitwa kwa kadiri ya Darwin "struggle for existance" na " survival for the fittest". Katika kuipitia pitia, hatimaye nimebaini uongo uliojikita katika nadharia hiyo inayoonekana kulazimisha kuukana uwepo wa Mungu pasipo hoja inayojitosheleza. Lengo la kuyaandika haya, ni kusema wazi kwamba pamoja na akili alizokuwa nazo huyu jamaa, kwangu mimi (Darwin) ni mwanasayansi mwongo (na wa kuandikiwa kitabu kabisa kabisa). Kwa sababu hiyo, nitaandika baadae uongo huo ulivyo wa wazi.

Mazoezi ya kusikiliza wanafunzi wangu

Miezi kadhaa nilikuwa nawafundisha (soma kuwasikiliza) wanafunzi fulani. Niliwapenda vijana wale. Kuna siku nitasimilia zaidi habari zao. Nilibahatika kuwafundisha ile mada katika Biolojia ambayo (ikifundishwa vyema) huwafanya wanafunzi wajifunze kufikiri. Mada yenyewe inaitwa organic evolution. Basi. Mimi ni kati ya wanaoamini kuwa kazi ya mtu aitwaye mwalimu si kufundisha bali kuongoza mijadala. " Mnafikiri viumbe na kila kilichomo katika dunia pamoja na dunia yenyewe vilitokea wapi?" Niliwauliza. Bila shaka unaweza kuelewa walijibu nini. " Sasa (Mungu) aliumbaje viumbe?" Nikawauliza. Mmoja akajibu kwa haraka: " Kwa nguvu zake(Mungu)...maana anao uwezo wote" Maneno mengine siyakumbuki. Kufupisha ilibidi nijie kwa njia hii: " Kwani huyo mnaye mwita Mungu alitokea wapi?" Wakashangazwa sana na swali la kijinga namna ile. Hawakulitazamia kutoka kwa mtu waliyemheshimu kama mimi. Mwalimu wa mazoezi. Huku nikijua kabisa wanahangaika kunilewa, ...

Tuache ubabaishaji, tubadilike

Nchi yetu inarudi nyuma kwa kasi. Zipo sababu nyingi. Moja wapo ninayoiona ni ubabishaji uliokithiri. Ile hali ya kushindwa kufanya mambo kama yanavyopaswa yawe, na kule kuchukulia mambo kirahisirahisi pasipo uwiano wa ukubwa wa suala na majibu yake. ( Asomaye na afahamu) Angalia siasa. Tizama wataalamu wetu. Madaktari. Wahandisi. Waalimu. Waandishi. Wote. Ubabaishaji. Ubabaishaji kila kona. Watu wanajitia kujua kila kitu. Inakuwa kama nchi hii haina wajinga. Ni kama nchi hii ina watu wanaojua kila aina ya kitu. Nchi ya wajuaji. Watu hatutaki kukubali ukweli wa kibinadamu kuwa ufahamu wetu una ukomo na hivyo hatuwezi kujua kila kitu. Ndio maana wetu hatukubali ukweli kuwa tu wajinga. Uliza kila mtu swali lolote, unapewa majibu. Ni kama kila mmoja ana majibu ya kila swali. Hakuna anayeomba "excuse" kwamba hapo bwana nimegota sijui. Ninanchotaka kusema mchana wa leo ni kwamba hatuwezi kuendelea endapo tabia ya kuamini kwamba tunajua kila kitu haitaondoka. Hatuwezi kuendel...

Watu wanapata taswira gani wanapokutazama?

Binadamu anao uwezo wa kujenga taswira yake - namna anavyoonekana - kwa wengine kwa kadiri apendavyo awe. Binadamu anaweza kuamua kuonekana mtu wa heshima zake, ama hata kuonekana mtu asiye na heshima zake. Uamuzi wa kujenga taswira hiyo, self-image kwa msisitizo, uko mikononi mwake yeye mwenyewe. Kwamba tunafikiri wengine wanatuchukuliaje ni suala la kujenga taswira zetu. Kwamba zaidi ya kule kujitathimini wenyewe, kujiangalia kwa macho yetu wenyewe, tunajaribu kujitazama kwa macho ya watu wengine. Tunajaribu kujifikiria kwa miwani ya wanaotuzunguka. Tukijiuliza swali kubwa: hivi huyu jamaa ananionaje hapo alipo? Self-image. Si tu kujiaminisha kuwa tu watu wa aina fulani kwa kutumia vigezo vyetu, bali kujaribu kurudusu, wengine wanatuonaje. Hatuwezi kujifahamu sisi ni akina nani kwa kujiangalia kwa macho yetu wenyewe. Macho yetu hutudanganya na mara zote hutafuta kutupendelea. Macho yetu hutafuta kutufanya tujisikie vizuri kuhusu nafsi zetu. Hivyo, tunapotaka kujifahamu kwa usahi...

Fujo huanzishwa na 'wenyenguvu' si wanyonge

Hakuna mahali katika historia (labda niambiwe vingine) panapoonesha kuwa matumizi ya nguvu - mapigano na vita, huanzishwa na wanyonge. Ni hivyo kwa sababu wao wenyewe (wanyonge) ni matokeo ya ' maguvu' ya wenye nguvu. Ni hivyo kwa sababu pasingelikuwapo watu wanaoitwa wanyonge, bila hao wanaojiona wana nguvu kuzidi binadamu wenzao, wenye haki kama wao. Hivyo, mapigano huanzishwa na mabwana wakubwa wao wenyewe, kwa kiburi chao cha kugoma kuwatambua na kuwasikiliza wenzao kama binadamu pia. Mapigano huwa hayaanzishwi na wale wanaoonewa, wanaonyonywa na wasiotambuliwa na kuheshimiwa. Wasiopendwa huwa hawasababishi chuki, bali wale wasiopenda wenzao ambao hujipenda wao wenyewe. Si wasiojiweza - waathirika wakuu wa ugaidi - huweza hata kufikiri kuanzisha ugaidi, bali wenye maguvu ambao hutumia maguvu hayo kupunja haki za wenzao kwa kuwahesababu kama watu wawezao kuondoshewa uhai wao wakati wowote ule. Si waliodharauliwa huweza kuanzisha visasi, bali wale wenye dharau wenyewe. ...

Mtumwa asiyeona haja ya uhuru?

Haishangazi kuwa mtumwa. Kinachoshangaza ni kule kuwa mtumwa asiyejielewa kwamba yu utumwani. Kule kuwa mtumwa mzoefu kiasi cha kuuhesabu utumwa kuwa sehemu ya maisha yako kamili. Kiasi cha kushindwa kutofautisha kati ya utumwa na uhuru. Unajikuta ukiogopa kuwa huru. Mtumwa mzoefu. Mtumwa mwaminifu. Mtumwa anayefurahia kuwa utumwani, utatumia lugha gani kumwelewesha kuwa hayuko huru? Maana kwake yeye uhuru ni utumwa, na utumwa ni uhuru. Unawezaje kumsaidia akasaidika? Nimeamka na sentensi hizo asubuhi ya leo. Heri ya mwaka mpya.

Unahusianaje na nafsi yako?

Huwa unajisikiaje ukijitazama kwenye kioo? Unaridhika na sura unayoiona? Vipi ukiangalia picha zako za hivi karibuni? Unaridhika na ulivyo? Umbo lako? Mtindo wa nywele zako? Rangi ya ngozi yako? Unajionaje? Watu wengi tunapata shida sana kujikubali. Hatujipendi. Kila tunapojitazama, tunaona kasoro. Wachache wetu huziona kasoro hizo kama vitu vidogo visivyotupa tabu sana. Mtu aweza kujiangalia kwenye kioo, akaona kasoro ndogo, lakini akajipa moyo: "Ngoja nichane, nitapendeza". " Ngoja niende saluni, nikabadili mtindo". Akaziona kasoro na zisimsumbue. Lakini wengi wetu huvunjika moyo kwa kudhani/amini kuwa kasoro hizo hazirekebishiki. Pengine rangi ya ngozi si nyeupe vya kutosha. Ama umbo letu halivutii, na mambo kama hayo. Kuvunjika moyo kwa namna hiyo, husababisha kujengeka kwa hisia hasi kuhusu nafsi ya mtu mwenyewe. Jambo moja kabla hatujaendelea: Mahusiano mema na nafsi zetu hutokana na vile tujichukuliavyo. Mahusiano mabaya na nafsi zetu husababisha kujidh...

Sherehe bila mwenye sherehe, inawezekanaje?

Picha
Umewahi kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mtu fulani bila ridhaa yake? Au unaigeuza kabisa inakuwa sio kumsherehekea yeye, ila kufanya utakayo, kwa mwamvuli wa kumsherehekea yeye! Kama ingekuwa ni wewe ndiye mwenye sherehe, ungejisikiaje? Watu wala, wanywa, hata kadi ya mwaliko hawakupi. Na bado wanadai wanakumbuka kuzaliwa kwako. Kweli? Hivi ingekuwa wewe ungejisikiaje?

Tofautisha dini yako na utamaduni wa "wenye dini"

Wakati umefika wa kuchukua juhudi binafsi za kutenganisha dini na utamaduni wetu kama vitu viwili tofauti. Tuweze kupambanua mambo ambayo ni ya kidini na yale ya utamaduni wa nje, ambayo kwa kujua ama kutokujua tunadhani kwa kuyafanya maana yake tunashika dini. Kuvaa kanzu na baibui si utamaduni wetu. Kuitwa Mathayo hakuhalalishi ukristo wako. Kukaa chini katika ibada, wakati kuna uwezekano wa kupata viti, ni kujaribu kuwaiga wenye dini na mazingira yao. Na bahati mbaya twayafanya hayo tukiamini kuwa tunashika dini kumbe ni ulevi tu wa utamaduni wa watu fulani fulani. Tujielewe.

Tusitegemee uzalendo kwa elimu hii

Kati ya mambo ambayo wana wa Kitanzania wanayakosa katika vyumba vyao madarasa, ni elimu ya kujielewa. Elimu ya kuwafanya waelewe nafsi zao wenyewe. Elimu ya kuwapandikizia falsafa za taifa lao wenyewe. Elimu ya kuwakomboa kimtazamo, wajue umuhimu wa utamaduni wao. Elimu ya kuwafanya waelewe wajibu wao katika kuufufua utamaduni huo ndani yao wenyewe na katika watu wao. Wenye kufundisha, hawajui nchi inayofalsafa gani. Nchi yenyewe haieleweki inayo falsafa ipi. Mitaala nayo haifahamiki imetayarishwa kwa shinikizo la nani na nani atapanda dau lini kuibadilisha. Na matokeo yake ni kwamba kila kijana "huhitimu" na falsafa yake anayoijua yeye na huelekea anakokujua mwenyewe. Kila jambo linakuwa shaghalabagala! Ndani ya mfumo kama huu, haitokaa iwezekane kuwa na Tanzania yenye dira inayoeleweka. Haitokaa itokee kuwa na Tanzania iliyojipembua kwa utamaduni wake. Haitokaa itokee tuwe na Tanzania yenye wazalendo waliotayari kuitetea raslimali za nchi yao kwa dhati ya mioyo. Haitokaa i...

Je, umewahi kuiadhibu nafsi yako mwenyewe?

Wajibu ni nini? Haki ni nini? Je, waweza kudai haki fulani fulani kutoka katika nafsi yako mwenyewe? Je, waweza kujiadhibu wewe mwenyewe kwa kutokutimiza wajibu fulani? Je, ni sahihi kudai haki (zako) kutoka kwa wengine, wakati (wewe mwenyewe) hujitendei haki? Tujielewe.

Unapojielewa nini huwa kimetokea?

Kujielewa. Tunasisitiza sana kujielewa. Lakini je, kujielewa maana yake nini? Unapoelewa jambo nini hasa huwa kimetokea katika ufahamu wako? Je, kuna tofauti gani iliyopo unapolinganisha kabla hujaelewa na baada ya kuelewa jambo? Je, twaweza kuelewa na/au kujua kila kitu? Je, upo ukomo (limit) wa uelewa?