Tuache ubabaishaji, tubadilike

Nchi yetu inarudi nyuma kwa kasi. Zipo sababu nyingi. Moja wapo ninayoiona ni ubabishaji uliokithiri. Ile hali ya kushindwa kufanya mambo kama yanavyopaswa yawe, na kule kuchukulia mambo kirahisirahisi pasipo uwiano wa ukubwa wa suala na majibu yake. ( Asomaye na afahamu)

Angalia siasa. Tizama wataalamu wetu. Madaktari. Wahandisi. Waalimu. Waandishi. Wote. Ubabaishaji. Ubabaishaji kila kona. Watu wanajitia kujua kila kitu. Inakuwa kama nchi hii haina wajinga. Ni kama nchi hii ina watu wanaojua kila aina ya kitu. Nchi ya wajuaji.

Watu hatutaki kukubali ukweli wa kibinadamu kuwa ufahamu wetu una ukomo na hivyo hatuwezi kujua kila kitu. Ndio maana wetu hatukubali ukweli kuwa tu wajinga. Uliza kila mtu swali lolote, unapewa majibu. Ni kama kila mmoja ana majibu ya kila swali. Hakuna anayeomba "excuse" kwamba hapo bwana nimegota sijui.

Ninanchotaka kusema mchana wa leo ni kwamba hatuwezi kuendelea endapo tabia ya kuamini kwamba tunajua kila kitu haitaondoka. Hatuwezi kuendelea ikiwa hatuwezi kukiri udhaifu wetu mpaka tuundiwe tume. Hatuwezi kuendelea ikiwa tutajitia ujuaji. Hatuwezi kuendelea ikiwa hatuwezi kujikosoa sisi wenyewe. Hatuwezi kuendelea ikiwa tunaendelea na hii tabia ya kuamini kuwa tunajua kila kitu.

Hatuwezi kujua kila kitu. Hatuwezi kufahamu yote. Tusisite kukiri kutokujua kila inapobidi. Hii, hata hivyo, haimaanishi kuwa tusithubutu kufanya yale "tunayoaamini" kuwa tunayajua. Nitafafanua zaidi.

Maoni

  1. Nakubaliana kabisa na wewe kaka. Lakini nahisi hii hali ya kukataa kukubali kuwa hatujui kitu, inatokana na kufundishwa kulinganisha kutokujua jambo na kuwa huna akili. Wengi huogopa kukiri hatujui kutokana na kudhani kuwa kutokujua = hatuna akili.Hili swala ndio linifanyalo kupinga maswala ya IQ test. Kama hujui mlenda ni nini na mwingine kakulia mlenda mkiulizwa maswala ya mlenda, aliyekulia mlenda lazima ataonekana anajua ingawa inawezekana asiyejua swala la mlenda ndio mwenye akili zaidi. Hivi kuwa na akili ni nini?
    DUH!
    Kazi kwelikweli!
    Tuko Pamoja Kaka.

    JibuFuta
  2. Kuwa na akili? Nadhani ni kiwango cha uwezo wa ubongo kufanya kazi yake inavyotakikana. Kurekodi taarifa zinazoufikia (ubongo)mahala sahihi, uwezo wa kupembua ziliko taarifa hizo baadaye (inapobidi)na pia namna ubongo wenyewe unavyoweza kutafuta uhusiano kati ya taarifa moja na nyingine (kufikiri) na hata uwezo wa kujaribu kuhusianisha kinachoonekana na taarifa zilizoko ubongoni tayari ili kupata maana. Mie nadhani hiyo ndiyo akili. Kwangu mimi huo ni uwezo asilia. Hausomewi ila una tabia ya kukua kulingana na umri wa mbebaji, kiasi cha taarifa amabzo mbebaji hukutana nazo, kulingana na mazingira yake.

    Kwa maana hiyo, mimi nadhani kutokujua mlenda hakupitishi hukumu kwa asiyeujua kuwa eti hana akili. Na anayetumia vigezo vinavyofanana na hicho kupima akili za watu, kwa kadiri yangu, anakosea.

    Karibu sana kaka.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?