Tusitegemee uzalendo kwa elimu hii

Kati ya mambo ambayo wana wa Kitanzania wanayakosa katika vyumba vyao madarasa, ni elimu ya kujielewa. Elimu ya kuwafanya waelewe nafsi zao wenyewe. Elimu ya kuwapandikizia falsafa za taifa lao wenyewe. Elimu ya kuwakomboa kimtazamo, wajue umuhimu wa utamaduni wao. Elimu ya kuwafanya waelewe wajibu wao katika kuufufua utamaduni huo ndani yao wenyewe na katika watu wao.

Wenye kufundisha, hawajui nchi inayofalsafa gani. Nchi yenyewe haieleweki inayo falsafa ipi. Mitaala nayo haifahamiki imetayarishwa kwa shinikizo la nani na nani atapanda dau lini kuibadilisha.

Na matokeo yake ni kwamba kila kijana "huhitimu" na falsafa yake anayoijua yeye na huelekea anakokujua mwenyewe. Kila jambo linakuwa shaghalabagala!

Ndani ya mfumo kama huu, haitokaa iwezekane kuwa na Tanzania yenye dira inayoeleweka. Haitokaa itokee kuwa na Tanzania iliyojipembua kwa utamaduni wake. Haitokaa itokee tuwe na Tanzania yenye wazalendo waliotayari kuitetea raslimali za nchi yao kwa dhati ya mioyo. Haitokaa itokee tuwe na viongozi wanaoingia madarakani bila mlungula. Haitokaa itokeee!

Na endapo itatokea, basi hapatakuwepo na msamiati mwingine bora kuelezea tukio hilo, zaidi ya huu wa "muujiza".

Inatosha kwa leo.

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?