Akili hutengenezwa!

Huwezi kufikiri jambo ambalo halipo ubongoni. Haiwezekani. Kufikiria ni kupekua mafaili. Kama mafaili yenyewe hayapo, huna cha kutafuta.

Ubongo wa mtoto ni kama ofisi mpya ambayo mamlaka ya kuifanya upendavyo yako mikononi mwako. Unaingiza fanicha uzipendazo, kwa kadiri ya mahitaji ya Ofisi yako hiyo. Unapanga makarabrasha yako kwa utaratibu uupendao mwenyewe. Sababu wewe ndio ofisi. Na unapohitaji sasa kuyatumia makrabrasha hayo, uchaguzi wako utakuwa “katika” yale yale uliyoyihifadhi awali. Pamoja na mapungufu ya mfano huu, bado unaweza kutumika kuelezea hali halisi. Huwezi kutafuta kitu ambacho ni wazi hukukiweka.

Au labda tuseme, ubongo wa binadamu ni sawa kompyuta tupu isiyoweza kufanya chochote mpaka mmiliki apandishe (install) programu azipendazo mwenyewe. Na uchaguzi wa kipi akifanyie kazi kwenye kompyuta yake unategemea na yaliyomo.

Watafiti wengi wanakubaliana kuwa kila mtoto huzaliwa na ubongo safi. Wenye uwezo safi. Wenye nguvu (potential) ya kuwa chochote. Pamoja na tofauti ndogo ndogo zinazotokana na kurithi, lakini kimsingi kila ubongo “unalipa”. Najua wapo watu kama akina Plato (babu yake Watson), walioamini kuwa watu hawafanani hivyo watengwe kulingana na uwezo wa bongo zao. Nitaendelea kuonyesha kidogo kidogo upungufu wa dhana za wawili hao.

*********************

Tulishatangulia kusema kuwa huwezi kufikiri jambo lisilokuwapo ubongoni. Nakazia haiwezekani. Kufikiri maana yake ni kupekua mafaili kama wafanyavyo watu wa masijala.

Chukulia mwanao hamjui mbogo, yule myama matata, mkazi wa porini. Hali ukijua hamjui, ukampa picha ya mbogo ukitaka aitambue, ubongo wake utapekua kuangalia kama kuna taarifa kama hiyo ubongoni. Kwa kuwa taarifa hiyo (schema) haipo kichwani mwake, basi ubongo wake unaweza kubofya kwenye taarifa ya ng’ombe anayemjua, na hilo ndilo jibu utakalopata. Masahisho utakayomfanyia, yana maana ya kuongeza taarifa ambayo haikuwapo kichwani mwake, na ndiyo itakayomsaidia kumtambua mbogo siku nyingine.

Ndio maana tunasema, namna ya kufikiri inategemea kilichoingizwa kichwani tangu tunapozaliwa. Tunaweza kuonekana wenye ubongo duni, kwa sababu tu waliotuzunguka hawakujisumbua kuwekeza katika vichwa vyetu. Ikiwa watu wanaomzunguka binadamu aliyezaliwa, watawekeza programu sahihi katika ubongo wake, watakuwa wamemlazimisha kufikiri sawa na uwekezaji wao. Vivyo hivyo, ikiwa watu hao hao watacheza na ubongo huo mpya na kuwekeza ubatili, wategemee kuvuna mabua.

Binadamu huwaza kile kilichopo.

Nani anabisha kwamba tangu tunazaliwa tuliaminishwa kuwa mzungu ni mtu bora mwenye “mihela” ? Nani anabisha kuwa tulishajengewa kichwani kwamba eti kuwa mweusi maana yake ni umasikini? Ndio maana leo hii mzungu akipita mtaani kwenu, kila mtoto anapiga kelele kwa kukenua: “mdhungu! Nipe hela!”

Pengine utasema hao ni watoto. Nenda Arusha ukaone vituko. Akishuka mzungu kwenye Skandnavia, kila “mwuungwana” anampamia na kiingereza za kuungaunga: Me ze kampani ofa yu gudi slip. Mwingine: “I luv yu”. Alimradi inaonekana kama jibu la matatizo yote liko mikononi mwa huyo kaburu.

Nenda New Arusha Hoteli upate picha ya sisi vijana wa kiswahili. Utakuta huyu ana gazeti (ambalo hajui hata limeandikwa nini). Huyu ana hereni. Fulana. Hirizi. Na kila aina ya harakati za kuwashawishi watu fulani wanaopatikana hapo kununua. Sisemi vijana “wajasiriamali” wasifanye biashara, hapana. Ila yanapokuwepo mawazo katika “wajasiriamali” hao, kuwa biashara hiyo haiendi bila ngozi nyeupe, hapo lazima pawepo tatizo. Inauma kuzungumza mambo kama haya. Nasita kuelea zaidi ya hapa kwa leo. Tujielewe.

Maoni

  1. yo, wanted to inform you everyone a tip on how you can save some money monthly, Getting a conversion
    kit for your vehicle will save you hundreds of dollars on gas by switch to an american made fuel 'Ethonal'.
    More americans are upgrading their vehicles to support both fuel types and buying ethonal to fill up your vehicle.
    Ethonal is not only an American made fuel, which you'll be support our economy alot more than buying fuel
    that we have to import making us more depended on foreign supplies.
    Run your vehicle on a [url=http://www.e85-kits.info]e85 Conversion kit[/url]

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?