Hivi mtoto huwaza kama mtu mzima?
Kama umewahi kujiuliza swali kama hilo, tafadhali karibu tuchangie mawazo. Mtoto huwaza nini? Mtoto hufikiri nini na kwa upana gani?
Katika mambo yanayofurahisha sana katika akili ya binadamu, ni vile ubongo wake unavyoweza kutengeneza mtandao wa kuhusianisha "tukio" moja na lingine, na hivyo kuleta mtiririko wa matukio unaoweza kujulikana kama mawazo.
Unapowaza maana yake ni kwamba ubongo wako unao uwezo wa kuunganisha vipande vingi vya matukio (schema) kwa kadiri yanavyohusiana, na hivyo kuleta mtiririko fulani, unaleta mlolongo wa uhusiano wa aina fulani. Inakuwa kama ile mikanda ya sinema yenye picha nyingi zisizotembea zenye mtitiriko wa matendo yanayokaribiana ambayo huunganishwa na kuleta mtiririko unaotembea.
Mawazo hapa yakimaanisha mtiririko wa vipande vya habari katika ubongo wa binadamu.
Ikiwa ubongo utashindwa kufanya hivyo, kwa maana ya kukosekana kwa mwendelezo wa vipande hivyo, kamwe mwenye ubongo huo hawezi kuwaza jambo. Sababu ni kwamba kati ya kipande kimoja cha tukio hapajawepo uhusiano unaotembea.
Tangu unapoamka mpaka unapolala usiku, na hata unapolala, ubongo wako huwa na mwendelezo wa tamthilia yenye mfululizo wenye mantiki. Hii, hata hivyo, haimaanishi kwamba unakuwa umewaza jambo moja kwa siku nzima. La, ila ukweli ni kwamba vyote uvionavyo, na kusikia kupitia milango ya fahamu, hutafutiwa mahali lilikohifadhiwa ubongoni na kuunganishwa kwa mtiririko wenye kuleta maana. Yaani, katukio kamoja hukufanya uwaze cha pili. Cha pili hukupekeleka kwenye cha tatu, cha tatu cha nne na kadhalika.
Na haya yote ni lazima yawe ubongoni tayari. Huwezi kuwaza kitu kisichopo ubongoni tayari. Kwa sababu ili kuwaza lazima stoo ya ubongo iwe na kitu hicho tayari. Endapo hakitakuwepo ubongoni tayari, basi pawepo na uhusiano wa kimantinki kati ya hivyo viwili ili kutengeneza mtiririko.
Kwa mtoto, inakuwaje? Je, ubongo wake unao uwezo wa kutafuta uhusiano kati ya kipande kimoja cha tukio na kingine? Je, kiasi cha vipande vya habari alichonacho kinatosha kuhusiana, na hivyo kuleta mtiririko unaoeleweka?
Nayasema haya yote, na kuuliza maswali hayo, ili tubaini sababu ya kwa nini miaka ya mwanzo ya maisha ya binadamu, huamua aina ya maisha atakayoishi mbeleni.
Karibu kujielewa.
Bwaya nafikiri kuwaza kunakua kama mwili unavyokuwa. Sasa kianachosababisha iwe hivyo ndo sijajua bado.Maelezo yako yamenipa mwanga na nina picha ingawa sijaelewa vizuri inakuwaje kuwaje.Blogu hii ni nzuri nimeipenda.Nasubiri kusoam mawazo ya wasomaje wengine. Asante.
JibuFutaMtoto anaweza kufikiri na kuwaza zahidi ya watu wanavyofikiria........ kunamwanapsycholojia mmoja anayeitwa piaget.. ambaye alikuwa anafikira kama zako... nakusema kuwa ubongo wa mtoto unakuwa kwa stage.....
JibuFutaMtoto anaweza kufikiri na kuact muda mchache tu anapotoka tumboni... lakini kugundua kwake kunakuwa kugumu kwasababu mtoto huyu ajui lugha tunayotumia sisi.... jinsi anavyoencode (weka) information kwenye ubongo wake na kuziprocess ni tofauti na binadamu mkubwa....
Mzee blog yako ni tamu sana....