Mtumwa asiyeona haja ya uhuru?
Haishangazi kuwa mtumwa. Kinachoshangaza ni kule kuwa mtumwa asiyejielewa kwamba yu utumwani. Kule kuwa mtumwa mzoefu kiasi cha kuuhesabu utumwa kuwa sehemu ya maisha yako kamili. Kiasi cha kushindwa kutofautisha kati ya utumwa na uhuru. Unajikuta ukiogopa kuwa huru. Mtumwa mzoefu. Mtumwa mwaminifu. Mtumwa anayefurahia kuwa utumwani, utatumia lugha gani kumwelewesha kuwa hayuko huru? Maana kwake yeye uhuru ni utumwa, na utumwa ni uhuru. Unawezaje kumsaidia akasaidika? Nimeamka na sentensi hizo asubuhi ya leo.
Heri ya mwaka mpya.
Heri ya mwaka mpya.
Maoni
Chapisha Maoni