Jenga Fikra Chanya, Uwe na Furaha

Kuwa na furaha ni uamuzi wako mwenyewe. Furaha ni matokeo ya namna ulivyoamua kufikiri. Kadhalika, kukata tamaa na kukosa amani mara nyingi ni matokeo ya kufikiri mambo yanayokatisha tamaa na wakati mwingine tusiyo na majibu yake. Tunatafsiri vibaya mambo tunayokutana nayo na ndiyo sababu tunapatwa na msongo wa mawazo.

Ndio kusema, fikra zako zina nguvu kubwa. Ukiweza kubadili fikra ulizonazo huwezi kusumbuliwa na chochote kile kinachoweza kutokea katika maisha yako. Katika makala haya tunaangalia mambo kadhaa yanayoweza kukusaidia kuwa na fikra chanya zitakazokufanya uwe na furaha.
Furaha ni uamuzi wako mwenyewe. PICHA: Jaguda.com


Jaza ufahamu wako na mambo chanya

Wekeza kwenye mambo yanayokujenga kiufahamu. Badala ya kutumia muda mwingi kusoma, kusikiliza, kuzungumza, kuangalia habari zinazosikitisha na kuumiza moyo, badili mazoea, Tangu unapoamka, shibisha ufahamu wako na habari zinazoinua moyo. 

Usisubiri watu wengine wakutie moyo. Jiinue moyo mwenyewe kwa kusoma mambo chanya, kusikia mambo yanayojenga, na kutafakari mambo yanayokuinua. Kadri unavyojenga mazoea haya, ufahamu wako utajaa habari njema na huo utakuwa mwanzo wa kuwa na furaha.

Jione kama mtu anayeweza

Huenda umekulia katika mazingira yaliyokuaminisha huwezi. Pengine ulikejeliwa na kudhihakiwa kuwa huna unaloweza. Matokeo yake akili yako imeamini huwezi na huachi kujifikiria kama mtu duni na asiyejiweza kitu.

Hakuna sababu ya kuendelea kujifikiria hivyo. Hupati faida yoyote kwa kujiona huwezi. Anza kujiona kama mtu wa maana, mtu wa muhimu, mtu anayetegemewa na watu. Tembea kifua mbele kwamba unaweza. Jisemee maneno ya kukuinua kwamba unaweza. Badili ile sauti uliyozoea kuisikia ikikunong’oneza kuwa huwezi. Ikatae. Jisemee unaweza. Furaha yako itarejea.

Tarajia mambo mazuri

Inashangaza kwamba mara nyingi tunajikuta tunatarajia kuwa mambo mabaya yatatokea hata katika mazingira ambayo hatuna ushahidi wowote. Kwa mfano, unaweza kuwa unaandaa ripoti ya kupeleka kwa wakubwa wako wa kazi, lakini unafikiria namna watakavyoipinga ripoti hiyo. Kwa nini usitarajie kuwa jambo jema litatokea badala ya kufikiria usichotaka kitokee? Jenga matarajio chanya kwa yale unayoyapanga. Tegemea mambo mazuri yatatokea.

Futa historia ya mabaya uliyokutana nayo

Kufikiria mabaya yaliyowahi kutukuta hutuumiza na kutukosesha amani. Kama umewahi kushindwa jambo fulani, kwa mfano, hiyo haimaanishi utaendelea kushindwa milele. Hakuna sababu ya kuendelea kuamini fikra duni kwamba kwa sababu mabaya yalishatokea basi lazima yaendelee kutokea.

Ukweli ni kwamba lolote baya lililowahi kukupata huko nyuma haliwezi kuwa msingi wa utambulisho wako. Ni wakati wa kufuta historia ya mabaya yaliyokufundisha kujisikia vibaya. Itazame leo badala ya jana na kesho. Ifurahie leo utapate nguvu za kuiona kesho. Utakuwa mtu mwenye furaha.

Acha kujilaumu kwa makosa ya wengine

Kwa nini ujiandikie hatia kwa kosa la mwingine? Kama aliyekosea ni ndugu yako, rafiki yako au mfanyakazi mwenzako, kuna sababu gani ya kujibebesha lawama kwa makosa yasiyo ya kwako moja kwa moja? Kwa hakika, huna sababu ya kujivisha aibu kwa mambo usiyowajibika nayo. Kujitesa kwa mambo yasiyo ya kwako binafsi, na kujihesabia hatia ni kuifukuza furaha yako mwenyewe.


Kuwa na furaha haimaanishi huna matatizo. Hapana. Furaha maana yake ni kuwa umeweza kuyatazama matatizo yanayokukabili kwa jicho chanya. Badili fikra zako, angalia matokeo yake.

Unaweza kufuatilia safu ya Saikolojia kwenye Gazeti la Mtanzania kila Alhamisi kwa mijadala kama hii.

Maoni

  1. Chapisho hili limeondolewa na msimamizi wa blogu.

    JibuFuta
  2. Chapisho hili limeondolewa na msimamizi wa blogu.

    JibuFuta
  3. MEJAQQ: AGEN JUDI POKER DOMINOQQ BANDARQ ONLINE TERBESAR DI ASIA

    Yang Merupakan Agen Judi Poker DominoQQ BandarQ Online Terbesar di Asia Hadir Untuk Anda Semua Dengan Games dan Bonus Yang Menarik!

    Bonus yang Kami Berikan di MEJAQQ :
    * Bonus CASHBACK 0,5% (Dibagikan setiap hari SENIN)
    * Bonus REFERRAL 10% + 10% SEUMUR HIDUP (Total kemenangan REFERRAL anda)
    * Minimal Deposit 20,000
    * Minimal Withdraw 20,000
    * 7 Bank Lokal (BCA, BNI, MANDIRI, BRI, DANAMON, CIMB NIAGA, PERMATA)
    * Deposit via E-Money, Pulsa XL dan TELKOMSEL
    * 100% Member vs Member
    * Pelayanan Bank dan Livechat 24 jam
    * Tersedia Dalam Aplikasi Android atau IOS.

    Mau dapet duit tanpa kerja? Bisa banget!
    Caranya? Buruan Kunjungi Sekarang Juga ^.^

    Info Lebih Lanjut :
    WA 1 : +855975482150
    WA 2 : +855978975095

    Kunjungi situs kami di :
    BandarQ Online
    Agen BandarQ Online

    BLOGSPOT :
    DUNIA VIRAL
    DUNIA MOVIE
    DUNIA GAME
    DUNIA ANIME

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Uislamu ulianza lini?