Jumuiya yetu isife bila taarifa...


(picha kutoka Mawazoni bila ruhusa)

Ningependa kumwomba mheshimiwa Katibu Mtendaji wa JUMUWATA ruhusa ya kuuliza swali hili. Tumefikia wapi na ile Jumuiya ya Wanablogu Tanzania? Mnaonaje tukifanya mjadala wa wazi kuhusu 'ufufuaji' wa jumuiya yetu?

Jamani yasijeyakawa yale ya mwaka elfu tisa mia sabini na saba.

Maoni

  1. Bwaya hapo umenena,mimi nilishaliuliza swali hilo mara nyingi sana lkn mimi sikupata jibu,kwa kifupi mimi hilo jambo linaniumiza sana.hebu mwenyekiti/katibu watujibu.

    JibuFuta
  2. Kaka Bwaya hapo nakuangushia gwala. Umenena kitu chenye. Wakubwa inakuwaje? Si hatuyataki mambo ya alfu tisa mia sabin' na saba. Jumuiya yetu haipaswi kutokomea.
    Tunapaswa kuifanyia kitu.

    JibuFuta
  3. Kaka Bwaya umenene,

    hili jambo tulivalie njuga.asante sana kwa kujituma.

    amani rasta hapa.

    JibuFuta
  4. Mjadala mzuri. Kumbe mnayo organization? How do you go about it? Kwani hatuisikii!

    JibuFuta
  5. tumsubiri ndg kitururu atupeyake majibu kwanza

    JibuFuta
  6. tumsubiri ndg kitururu atupeyake majibu kwanza

    JibuFuta
  7. Nimesoma msuto na nitajibu!

    JibuFuta
  8. Nafikiri uwe ni mjadala wetu wote. Wale wapya ambao hatukuwepo wakati jumuiya inazaliwa, nao wanakaribishwa. Tuulize maswali ikibidi. Na Katibu wetu (kwa niaba ya viongozi wengine wasiojulikana walipo hivi sasa) atajaribu kujibu, kuelekeza na kuweka mambo vizuri.

    Nia si kushutumu bali kujaribu kuangalia wapi tulikojikwaa ili tujisahihishe.

    Labda tuanzie hapa. Kwamba jumuiya yetu imelala. Hilo halina mjadala. Sasa tujadili kipi kinakosekana na cha kufanya ili kuifufua ni kipi.

    Tafadhali tusiogope mjadala.

    JibuFuta
  9. Hivi kumbe kulikuwa na Jumuiya?
    Ndio kwanza nasikia hizi habari.
    Haya wale walioaminiwa na kupewa dhamana ya kuongoza mashua hiyo wajitokeze wenyewe hadharani tuwaweke kiti moto na kama wamechemsha basi wajitoe wenyewe wasisubiri kustaafishwa kwa manuafaa ya jumuiya.

    JibuFuta
  10. Da! Kumbe kuna jumuia ya wanablog,? Ni hatua nzuri iliyokwisha kupigwa.
    Hivi malengo hasa ya jumuia hii ni yapi?
    Viongozi wa jumuia hii wako wapi? Namfahamu Kaka Kitururu basi.
    Kuna malengo gani ya baadae kuhusu jumuia hii?
    Mpaka sasa jumuia hii imeshapata mafanikio gani?
    Ni vigezo gani vinazingatiwa ili mtu kuwa mwanachama?
    Kuna kauli mbiu yoyote ya jumuia?

    JibuFuta
  11. samahani fungua kurasa ya kuchangia mawazo kuhusu jumuiya ya wanablogu tanzania.

    http://blogutanzania.blogspot.com/

    www.ringojr.wordpress.com

    N.B nimejaribu kuweka au kusambaza ujumbe huu takribani blogu 15.Naomba tusaidiane katika hili,tuhamasishe ili wengi waelewe umuhimu wa blogging na kuwa na jumuiya.

    Bwaya kwa pamoja tunaweza.

    amani.

    JibuFuta
  12. Hivi mwili unaweza kufanya kitu kinachoeleweka kama kichwa kina matatizo? Niambieni. How can it be?

    JibuFuta
  13. tufanye kitu kimoja muhimu. sisi wenye blog fualni zinazojikita kwenye kutafuta majibu ya changamoto tulizo nazo, tuunde jumuiya yetu ya kujitegemea

    ni wazo langu tafadhalini

    JibuFuta
  14. Ringo, asante kwa hamasa. Ni kiu yetu sote kwamba wazo lililozaliwa mwaka 2006 lisife bila sababu.

    Uhai wa Jumuiya yetu unatutegemea sisi sote. Si jukumu la watu fulani pekeyao ambao kimsingi hawatastahili lawama yoyote ikiwa mambo hayatakuwa kama inavyotarajiwa.

    Tuifufue jumuiya yetu kwa pamoja.

    JibuFuta
  15. Kamala, sijakupata vizuri. Naomba ufafanue vizuri kwa sababu jumuiya tayari ipo na kinachofanyika ni kuifufua.

    JibuFuta
  16. basi tufanye juhudi za makusudi za kuifufua ili na sisi tusiokuwemo tuwemo. vinginevyo tujadili kwa mkabala mwingine. ni vyema tukawa na chombo chetu imara. basi tuunde kamati maalumu ya kuifufua kamati hiyo iwe chini ya uenyekiti wako ndugu bwaya, amina

    JibuFuta
  17. Kamala, nadhani tunachokifanya sasa hivi ni juhudi hizo hizo za kuifufua Jumuiya yetu. Ufufuzi huu unapofanyika kwa njia ya mijadala ya wazi inapendeza zaidi badala ya kuunda kamati kama wanavyofanya wanasiasa. [Manake tunaweza kuunda kamati ikaja na mapendekezo ambayo tunayaundia kamati ili kuja na hatua zitakazotekelezwa na kamati nyingine!]

    Nadhani (kwa maoni yangu) kuwa kujadiliana kama tunavyofanya kunaweza kabisa kuifufua jumuiya hii.

    Halafu Kamala ukiisha kuwa mwanablogu tu ni 'automatiki' kwamba unakuwa mwanachama wa Jumuiya hiyo (Labda taratibu zikibadilishwa). Kwa msingi huo, nawe umo japo hukuwaunablogu wakati inazaliwa mwaka 2006.

    Narudia tena kwamba haipendezi tunapoanzisha vitu halafu tunaviacha vinaelea elea hivi na hatimaye vinajifia bila sababu.

    Hata kama ni kweli kwamba wengi waliokuwepo enzi za 'vuguvugu' la Jumuiya hawaonekani lakini hiyo haitufanyi tuogope kushiriki ufufuzi huu kwa pamoja.

    Unaonaje hapo?

    JibuFuta
  18. Nimeipitia ile blogu ya Jumuiya. Iko kimya tangu mwaka juzi. Mimi nimwulize Katibu, nani mwenye access na blogu ile?

    JibuFuta
  19. Bwaya ni lazima tupate access ya ile blogu ili mijadala ianze au
    tutumia hata hii blogu yako kuendesha mijadala.

    jamani naomba tuchangie.

    ringojr.

    JibuFuta
  20. Ringojr tupe maoni yako nini kifanyike

    JibuFuta
  21. Nakubaliana na anon wa 10/3/09 2:37AM. Tatizo linaloimaliza jumuiya yetu ni la kiuongozi zaidi. Mwenyekiti mbali na kutokufahamika kwa 'wananchi' lakini inaelekea kuna mazingira yasiyoeleweka yaliyomweka madarakani. Kwa mfano nilipokuwa nafuatilia kumbukumbu za mwenendo mzima wa uchaguzi kwenye blogu ya blogtanzania, nilibaini hitilafu kubwa. Uchaguzi ule ulifanyika kwa mizengwe ya kimaslahi ambapo nahisi msimamizi wa uchaguzi huo alizidiwa na damu.
    Pamoja na malalamiko mazito yaliyotolea baada ya 'upishi' wa matokeo hayo, bado jamaa walibaki yakichekelea na kukejeli.

    Ndugu zangu kinachotokea sasahivi ni matokeo ya kuchezewa kwa uchaguzi ule. Msilalamike

    JibuFuta
  22. nimekuelewa bwaya. japo umekosea nilianza kublog toka 2006.

    sawa, tuendeleze mjadala

    JibuFuta
  23. Mimi ni mgeni kabisa sikujua kama kuna jumuiya ya wanablog. Na sijui mlikuwa mnajadili nini na kama kumekuwa kimya hivi basi inapaswa tufanye kitu nini sijui wenyeji watuambie.

    JibuFuta
  24. Amani, Heshima na Upendo kwenu nyote.
    Nashukuru kaka Bwaya kwa changamoto hii. Kwangu naweza sema machache. Kwanza ni kwamba tutahitaji kujua mipaka ya nani anaweza kujiunga na jumuiya. Ninalomaanisha ni kuwa kwa kuwa nina imani kuwa wanajumuiya tutakuwa na orodha mahala fulani, tunahitaji kujua kama kutakuwa na "ratings" za blogs zetu. ni kwa kuwa kuna wenye habari za kiutambuzi, kiuchanganuzi, kijamii, misaada ya kielimu, misaada ya kijamii kwa ujumla, taswira na hata wapo ambao wao ni "strictly" ngono. Kwa hiyo kujua ni vipi tutaweza kuwa na mipaka ya nani atakuwepo kwenye jumuiya na ambaye hatakuwepo ni kwanini asiwepo. Na hapo ndipo linapokuja suala alilosema ndugu Kamala hapo juu kuwa na vi-branch vya jumuiya ambavyo vuinaendana na yale muandikayo. Na hili lina ukweli maana sisi wa changamoto, utambuzi na mijadala hatuna utendaji sawa na wale wa taswira pekee. Naamini umeliona hili. Lakini pia hata namna tunavyoshirikiana (baina ya bloggers) utagundua kuwa ni tofauti. Na kuendelea kung'ang'ania jumuiya kubwa isiyo na watu wa mtazamo mmoja ni afadhali kutengeneza ndogo itakayokuwa mfano kwa wengine na namna ambavyo tutaweza kutumia uzoefu wa hii kuendeleza hiyo KUBWA.
    Nawakilisha na ntarejea kuendeleza mjadala kwa manufaa yetu sote.

    JibuFuta
  25. Asante Mube bila shaka Katibu atalichukua hili kama changamoto.

    JibuFuta
  26. Nipo mlaumiwa!Nitaongea kidogo baada ya muda nini kinaendelea na hakikuendelea!

    JibuFuta
  27. Nimeupandisha huu mjadala kwenye http://blogutanzania.blogspot.com/

    JibuFuta
  28. Nimesoma maoni mazuri ya mchangiaji mzee wa changamoto. Wazo lake ni zuri na linakusudia kujenga jumuiya imara.
    Lakini tahadhari ninayoina ni uwezekano wa kuongezeka mipasuko iliyopo hivi sasa. Hizi clusters zilizopo zitapata nguvu ya kutengana kuliko hata ilivyosasahivi.
    Haya ni maoni yangu kwenye mjadala huu.

    JibuFuta
  29. ndugu wanajumuwata au wanablogu kutoka Tanzania.

    mimi nawazo au maoni.

    kwanza tuanze kuwaalika wanablogu wenye jumuiya ili watuelimishe tufanye nini,kwa mfano kenya wanajumuiya yao, kwa ivo tunaweza kuwaomba watupe mawazo ya kufufua
    jumuwata.

    pili mimi naomba tupate wawakilishi wakujitolea kuendesha hii jumuwata.

    mimi ringojr.

    JibuFuta
  30. Kama alivyosema Luihamu, ni vizuri tukipata mawazo kutoka kwa wenzetu wenye jumuia ambazo ni hai.
    Kwa upande mwingine mawazo ya mzee wa chamgamoto nafikiri yana changamoto fulani. Kuunda jumuia ndogondogo kwa kuzingatia mwanablog anazungumzia nini, hii inataweza kuzua matabaka ya ajabu.Mtu anayezungumzia siasa anaweza kuacha hata kufuatilia kinachozungumzwa ktk blog zinazozungumzia maswala mengine ya kijamii.Hii itasababisha kutokufahamiana vizuri kwa wanablog wote tz bali watafahamiana wale tu wenye kuandika au kutoa mawazo ktk nyanja fulani.

    JibuFuta
  31. Asante MSOMAJI WETU.
    Nimekupata na kukuelewa. Na uliyosema yana ukweli kuwa kunaweza kukatokea mgawanyiko kuliko ujenzi wa jumuiya. Nililokuwa nawaza wakati naandika ni namna tunavyoweza kuimarisha jumuiya kubwa na changa kutoka kwa watu wenye mitazamo tofauti kabisa kama alivyosema Kaka Kissima. Kama inawezekana ni vema, lakini inapoonekana kusuasua basi hizi ndogo zianze ili kwa uzoefu wa ndogo hizi tuweze kuona wapi kuna ufanani na utofauti na vipi tutaweza kuziuwianisha na kujenga moja kubwa.
    Asante kwa wote

    JibuFuta
  32. Kesho jumapili napandisha Hitimisho!

    JibuFuta
  33. Jamani wengine sisi wageni bado tunakamba mguuni,naomba kuuliza hiyo jumuiya ilikuwa na majukumu gani?

    Inajihusisha na nini? kuwakusanya wanablog na kutoa mawazo yao,au matatizo wanayokumbana nayo au vipi?

    Au ilikuwa kama una malalamiko unayapeleka kwenye jumuiya yanatafutiwa ufumbuzi au vipi?

    Samahani naona nauliza maswali ya kijinga lakini nahitaji kufahamu zaidi.

    JibuFuta
  34. Nashukuru kuwa mjadala huu umenikutanisha na watu wengi wapya ambao link zao sikuwa nazo, na mjadala huu sasa umeniwezesha kuzipata, na kuwaelewa, na kama ilivyo ada, tayari zinaonekana katika side bar ya kushoto kijiweni kwangu sehemu ya blogroll.

    Mbali ya kuwakaribisheni sana wale ambao mtapata nafasi na hamu ya kunitembelea, pia napenda kuchukua fursa hii, kuwakaribisha kwa ajili ya kufuatilia maelezo kidogo kuhusu JUMUWATA, ambapo nitaandika kazi kadhaa nikiwa kama mmoja kati ya waasisi wa Jumuiya hiyo, na mwenyekiti wa jumuiya hiyo hadi sasa.

    Kwa kifupi lakini kwa kina sana, nitajaribu kuzungumzia mambo kadhaa huko, ambayo wengi wetu tukiyapitia basi tutaelewa what is JUMUWATA, why JUMUWATA na mengine kama hayo.

    Ninaamini, kama wengi wanavyoamini kuwa, mijadala ni njia bora ya kuelekea maendeleo thabiti.

    mchambuzi kutoka
    www.uchambuzi.blogspot.com

    JibuFuta
  35. karibu sana ndugu Ramadhani Msangi,
    nifuraha kuona uongozi uliochaguliwa kuongoza jumuwata unachangia mada.

    mkuu Simon Kitururu
    mkuu Ramadhani Msangi.

    JibuFuta
  36. Nimefurahi kusoma mchango wa Mwenyekiti wetu. Bila shaka wasomaji tutafika ofisini kwake kama alivyotuelekeza kupitia makarabrasha ya Jumuiya. Hizi ni habari njema kwa kila anayeipenda Jumuwata. Mimi ningependa kuamini kuwa sasa jumuiya yetu imepuliziwa pumzi ya uhai.

    Katibu alishatuelekeza ukumbi wa mijadala ya kijumuiya. Tafadhali tusisahau kupitia kule kujielimisha zaidi na kutoa maoni yenye lengo la kuijenga jumuiya yetu.

    Amani

    JibuFuta
  37. Waswahili husema AHADI NI DENI, nami basi ni nani hadi nipingane na wahenga?

    Naam, kama ambavyo nilijitokeza na kuahidi hapo awali, nimeanza rasmi mjadala ambao nimeupa jina la JUMUWATA, ILIPOTOKA, ILIPO NA HATMA YAKE.

    Pamoja na mambo mengine, kwenye nilichokianzisha, natarajia kugusia changamoto kadhaa ambazo zimetolewa na wadau kupitia maskani hii, kwa lengo la kutoa ufafanuzi pale ambapo kuna utata na kujaribu pia kutoa majibu kwa pale ambapo pameonekana kuwa na maswali mengi.

    Ni matarajio yangu kuwa, tutakuwa pamoja katika safari ya kufika tunakotaka JUMUWATA ifike. Tafadhali shiriki katika mjadala niliouanzisha kupitia anwani hii

    http://uchambuzi.blogspot.com/2009/03/jumuwata-ilipotoka-ilipo-na-hatma-yake.html

    MAJADILIANO NI NJIA BORA YA KUFIKIA MAENDELEO ENDELEVU

    JibuFuta
  38. Kule naendelea kufanyia kazi ni swala la ufundi mitambo ndio limechelewesha!

    :-(
    Mjadala uendelee

    JibuFuta
  39. Ahadini deni, kile nilichoahidi kuwa nitakifanya, nimeahakifanya tayari. Taarifa yangu kama mwenyekiti wa JUMUWATA, hadi sasa iko tayari na nawaomba wadau sasa mjitokeze muipitia kwa undani na kuijadili.

    Tafadhali tembelea
    http://uchambuzi.blogspot.com/2009/03/jumuwata-taarifa-toka-kwa-mwenyekiti.html, kwa ajili ya kuipata, kuisoma na kuijadili taarifa hiyo.

    MJADALA UENDELEE

    JibuFuta
  40. Ahadini deni, kile nilichoahidi kuwa nitakifanya, nimeahakifanya tayari. Taarifa yangu kama mwenyekiti wa JUMUWATA, hadi sasa iko tayari na nawaomba wadau sasa mjitokeze muipitia kwa undani na kuijadili.

    Tafadhali tembelea
    http://uchambuzi.blogspot.com/2009/03/jumuwata-taarifa-toka-kwa-mwenyekiti.html, kwa ajili ya kuipata, kuisoma na kuijadili taarifa hiyo.

    MJADALA UENDELEE

    JibuFuta
  41. Huyu mwenyekiti kupatikana naomba niwapongeze waliomchomoa huko alikokuwa. Kazi kweli kweli

    JibuFuta
  42. Heshima zenu wakubwa, mabibi na mabwana,

    Nimerudi tena, nilikaa kimya ili kusoma maoni ya wenzangu.

    nadhani maoni yangu yatatofautiana sana na ya wenzangu.

    Mimi naona kuna haja ya kufanya mapinduzi kama yale yaliyofanywa kule kisiwani Madagasca.
    Kwa nini,nimependekeza uamuzi huo mzito uchukuliwe?.....

    Haiwezekani kwamba kulikuwa na Jumuiya na baadhi ya wanablog hawaifahamu, hii inaonesha ni kiasi gani uongozi uliokuwepo hauna watu makini na wabunifu.

    Huu sio wakati wa kupiga soga ni wakati wa kutenda, kwani sisi kama wanablog tumekuwa mstari wa mbele kuikosoa jamii na serikali lakini tumeshindwa hata kujiongoza wenyewe, sasa tunakosoa nini?
    Hii inanifanya nikumbuke hadithi ya Biblia ya kibanzi na Boriti, tumekuwa wepesi sana kuona vibanzi kwenye macho ya wenzetu il-hali tuna Boriti machoni kwetu.

    Nadhani tunahitaji mawazo mapya.
    Viongozi waliopo nawaheshimu sana, na ninawapongeza sana kwa kuindesha jumuiya mpaka hapa ilipofikia, sasa nawaomba wawapishe wengine ili waje na mawazo mapya.

    Kusema ukweli kama sio kaka Bwaya kuuweka huu mjadala hapa sidhanai kama tungefahamu juu ya hii jumuiya, na huu ni uzembe.

    Ndugu wajumbe naomba nisijengewe chuki juu ya mtazamao wangu huu..
    naomba kuwasilisha.

    JibuFuta
  43. Koero uko sawa. Tunajua kuchonga sana lakini tunachofanya hakionekani. Kwa nini kiongozi usubiri kukurupushwa eti ndio uje na 'taarifa'? Huu si muda wa kuambiana oh mimi ni mwanzilishi sijui mwasisi. Wizi mtupu!

    JibuFuta
  44. Nimesoma maoni mpaka naona kizungu zungu.

    Kwa kifupi naomba viongozi watupe mikakati yao na sera za kuimaerisha umoja, wasikae kimya kuna hoja nzito za kujibu humu, lakini naona wako kimya.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?

Pay $900? I quit blogging