Nitautambuaje udhaifu nilionao?

Hivi karibuni tulijadili kwa ufupi kuhusu dhana ya ukosoaji na kusifiwa. Ninafurahi kuona namna watu wanavyotoa maoni mazuri tofauti tofauti ambayo ukiyasoma yanakupa uelewa mkubwa zaidi. Kwa hakika, maana hasa ya blogu ni majadiliano. Ule mtindo kongwe wa mwandishi kuandika kwa fikra kwamba anachokifikiria ndicho sahihi na kinachopaswa kumezwa na wasomaji, hapa si mahala pake.

Blogu inatuweka karibu waandikaji na waandikiwa (ambao kimsingi inakuwa kama hawapo maana wote wanajadili kilicho mezani). Kwa hiyo, blogu ni majadiliano ndio maana binafsi sipendi kuandika kwa mtindo wa hitimisho. Hata kama mjadala utakaojitokeza unaweza usifikie hitimisho, bado huamini kuwa huko mbeleni, hitimisho husika laweza kufikiwa na wasomaji.

Katika mada hiyo, kuna msomaji mmoja alinipigia tukajadili kwa muda mrefu. Ninawapongeza wasomaji wanaopenda kuendeleza mijadala tunayoianzisha katika blogu zetu hata kwa njia ya simu. Basi. Kilichojitokeza katika majadiliano hayo, ni namna tunavyoweza kuubaini udhaifu wetu wenyewe.

Kinachoonekana ni kwamba, mtu kuubaini udhaifu wake si kazi rahisi. Kimsingi, karibu kila mtu huamini kuwa yeye ni mtu kamili. Hakuna mtu hujiona mwenye mapungufu. Ila kinachotokea ni kuwa watu wengine ndio huyaona mapungufu yetu ambayo mara nyingi kwetu mapungfu hayo sisi hatuyachukulii kama mapungufu. Ndio maana, kwa mfano unapotokea ugomvi, kila mmoja (katika hao wagombanao) huamini kuwa mkosaji ni mwingine na kwamba anayestahili kuombwa msamaha ni yeye(yaani kila mmoja hutegemea kuwa yeye ndio wa kuombwa msamaha). Suluhu ya ugomvi ni kwa mmoja wapo kuamua "yaishe" hata kama bado anaamini kuwa hajakosea.

Sasa katika mazingira kama haya, msomaji wangu anauliza: mtu huutambuaje udhaifu wake? Inawezekanaje mimi kuujua udhaifu nilionao?

Maoni

  1. Nakushukuru sana bwana bwaya kwa mjadala huu mzuri ambao unayagusa sana maisha yetu ya kila siku.


    Ukweli ni kwamba udhaifu kwa watu wengi umekuwa ni tabia kiasi kwamba kuugundua imekuwa ni vigumu sana.

    Self assessment ni njia ya kwanza kabisa ya kuweza kuugundua udhaifu ulionao.Ukiweza kufuatilia mwenendo wako mwenyewe nadhani utaweza kugundua sehemu ambazo unahitaji kujirekebisha.

    Kuwa mtu wa kupokea ushauri pale unaposhauriwa. Kuna msemo mmoja niliupata kwenye kitabu kimoja kinachoitwa "impossible is possible" mtunzi ni John Mason,msemo huu unasema "a mirror reflect a man's face, but what he is really like is shown by the kinds of friends he chooses".Kama Bwaya alivyosema mtu binafsi kuugundua udhaifu ni vigumu sana,hivyo ni vizuri sana kama tutakuwa wapole pale tunapokosolewa na ni vizuri pia kupata namna ya kuondokana na ulichokosolewa nacho kutoka kwa mkosoaji.

    Ishi na watu vizuri.Mtu anayejiona mbabe,mwenye hali ya uonevu,mtu asiyependa kujumuika na wengine itakuwa vigumu sana kugundua mapungufu yake.Kuwa mtu wa kukubali mabadiliko na tusisahau kumwomba Mungu atupe uwezo mkubwa wa kuyagundua madhaifu yetu na atuzidishie hekima ktk kukabiliana nayo.
    Kabla sijasahau ,naomba niliweke wazi hili "mimi,wewe na yule tunachangia sana ktk kufanya wengine washindwe kutambua madhaifu yao ,kwa sababu,wengi wetu huwa tunashindwa kabisa kuwaeleza wenzetu pale wanapokosea halafu tuna uwezo mkubwa wa kuongea pale muhusika anapokuwa hayupo.da! Mi kwa leo naishia hapa!!

    JibuFuta
  2. Mzee naona umerudi kwa kasi,maana unakimbiza ile mbaya.
    Kila nilkipita hapa nakutana na post mpya inayohitaji tafakuri.
    tatizo siku za hivi karibuni nimetingwa sana na shughuli za watu, hivyo nina muda mfupi sana wa kupitia vijiwe vya wenzangu ili kupata hekima.
    kama nikipata muda nitapita tena kuchangia, lakini naona bwana alienitangulia kanisemea kile nilichotaka kusema.

    Hata hivyo nitapita baadae.

    JibuFuta
  3. kaka Bwaya nimepita hapa ili kujifunza.
    Ukweli ni kwamba nazifagilia kazi zako, kwani zimetulia na wakati mwingine zinahitaji utulivu wa hali ya juu katika kuzichambua, ndio sababu sikurupuki kutoa maoni.
    Najifunza mabo mengi sana, kwa hiyohata kama sitoi maoni lakini amini kwamba najifunza kupitia Blog zenu,na nadhani ndizo zilizonipa changamoto ya mimi kuanzisha kibaraza changu ili kuendeleza darasa hili la wanblog ambalo rafiki zangu wanadai ni ujinga mtupu!!!!!
    mimi sijasema.
    hata hivyo huwa baadhi yao huwa hawakosi kusoma huun ujinga wetu.

    JibuFuta
  4. Duuh dada Koero wala usiwaache hao komaa nao mapaka ipo siku watabaini wakaosa UHONDO wa mambo matamu ya kujadili. kuna wengine chuo nikiwaeleza nina blogu ya kinyasa wanashangaa sana wanasema sina kazi! nami nikasema poa mbona mnajaza maktaba kusoma na kuriri akina faulani na kujiaminisha mnajua halafu mkiingia maisha ya mtaani mnachemka mmmmm BAHATI mbaya sina HAMU ya kurejea tena MLIMANI sijui mtaniinua kwa JEKI maana naona huu sasa ujinga mtupu nitarudi shule 2010 kuanza upya.

    Kuhusu mada za Bwaya yaani kwani ni darasa ndiyo maana nashindwa kuchangia maoni yale ya kiufundi kwani bado najifunza toka kwake. mimi najua udhaifu wangu ila siwaambiii mtacheka sana ngoja nianze kucheka mimi haha ha ha ha ha ha ha ha ha mmmmm Markus mwoga sana yaani hajiamini sana mmm ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha

    JibuFuta
  5. Kwa mada ntarejea baadae, ila kwako Da Koero. Wala usishangazwe na hao maana walisema "every truth goes through three stages. First will be ignored, secondly violately ridiculed and then will be accepted" Hao wako kwenye hatua ya kwanza. Kuna moja nyingine kabla hawajautambua ukweli na umuhimu wahuo Ujunga. By the way huo waweza kuwa ni udhaifu wao.

    JibuFuta
  6. Hakuna kitu ambacho nakipenda kama chakula changu kinachoitwa blogu hata mimi hapa kazini huwa ninaambiwa na watu wengi kuwa ninapoteza muda kwa kitu ambacho hakina faida kwangu lakini huwa najua kuwa hawajui nini maana ya kublogu.

    Wakati mwingine hata mhariri wangu huwa ananiambia nisiblogu lakini huwa ninamjibu kwa heshima na tahadhima kuwa siwezi kuacha chakula changu.

    kwahiyo dada Koero usijali.

    kuhusu mada hii ya Bwaya kwakweli watu wengi hatujui kasoro zetu ila kama tunataka kuzijua yatupasa kujifunza kutoka kwa wenzetu.

    Hoja za kutukosoa tuzifanyie uchunguzi na kuzibaini ukweli wake kisha kuufanyia kazi ni hayo tu kaka Bwayi

    JibuFuta
  7. listerning is better than talking. if that was not true, God would have not given man two ears with one and only one mouth... Robert Kiyosaki katika kitabu cha rich dad poor dad

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?

Pay $900? I quit blogging