Kulikoni JUMUWATA?


WENGI wetu tunakumbuka namna ambavyo vuguvugu hili la blogu lilikuja kwa kasi kama miaka mitatu hivi iliyopita. Na Ndesanjo Macha akiwa mhamasishaji mkuu katika ukuzi wa Teknolojia ya blogu katika kiswahili kwa kujitolea. Kampeni zake zilitufikia wengi wetu kupitia ukurasa wake wa gumzo la wiki katika gazeti la mwananchi. Nina hakika kwamba kazi hiyo hakuifanya kwa malipo. Alijitolea muda wake na matunda yake yalikuwa wazi. Bila yeye, bila shaka blogu maarufu kama Michuzi, Bongo celebrity, Kijiji cha Mjengwa, Haki Ngowi, Now and then na nyinginezo nyingi bila shaka zisingekuwepo. Narudia neno bila shaka. Historia ya Blogu Tanzania haiwezi kukamika bila kumtaja yeye.

Basi. Kasi ya blogu iliendelea kukua kwa kasi mno kiasi cha kufikia kuundwa kwa Jumuiya ua Wanablogu Tanzania. Wakachaguliwa viongozi tarehe 29 Juni 2007. Tukafurahi.

Hata hivyo, lazima tuwe wazi kwamba kasi ya ukuaji wa blogu imeendelea kuwa ndogo kwa karibu mwaka sasa. Jeff Msangi aliwahi kuzungumzia suala hili. Soma maneno yake hapa alipokuwa akisherehekea siku ya Blogu kwa ukiwa. Binafsi niliguswa sana na maoni ya Freddy Macha katika makala hiyo akisema (namnukuu): "Jambo lolote la kutuunganisha watanzania liwe dogo au kubwa ni la kupigiwa makofi. Hatuna umoja: Tunasemwa Afrika nzima kwetu tuna amani lakini hatuungani. Imechosha". Mwisho wa kunukuu.

Ni kweli mwaka jana maadhimisho ya siku ya blogu hayakuwa na shamrashamra zilizotegemewa kama alivyosema Jeff. Labda ni kwamba kila mtu alisubiri maelekezo kutoka kwa watu fulani ambao hata hivyo walikuwa kimya.

Hapa unaweza kuona posti ya mwisho ya blogu ya Jumuiya yenye umri wa karibu mwaka sasa.

Namshukuru mwanablogu muwazi Rasta Luihamu kuja na wito wa wazi bila kutumia anonimasi. Kuifufua Jumuiya yetu. Namuunga mkono. Nadhani hata wewe msomaji unamuunga mkono katika hili. Ni jambo la faida. Ni jambo la umoja. Umoja ni nguvu sio?

Basi tuitikie wito wake huu, ili hatimaye tuwe na siku ya Blogu Tanzania mwaka huu tarehe 18 Novemba. Tusiendeleze jadi ya mipango isiyotekelezeka. Nina imani na moyo wa kujitolea walionao viongozi wetu pamoja na majukumu mengi waliyonayo. Tuwatie moyo.

Shime.

Maoni

  1. Kumbe hata sikujua kama kuna siku ya blog TZ. Kwa kweli kama hivyo tukazani ili iyo siku iwe ila binafsi nitashindwa kuhudhuria.Wanablog oyeeeeeeeee

    JibuFuta
  2. Yasinta huwezi kushindwa kuhudhuria siku hiyo. Ukumbi wa sherehe huwa ni mtandaoni.

    JibuFuta
  3. basi kama hivyo poa tena poa sana. mchana mwema na kazi njema

    JibuFuta
  4. Yasinta mwambie na mwingine kwa habari ya siku hiyo. Itapendeza tukishikamana.

    JibuFuta
  5. Great work!
    Congratulations!!!
    Have a nice weekend.

    JibuFuta
  6. TATIZO LA BLOG KUZOROTA NI NDESANJO MWENYEWE KUTOKUWA KIONGOZI RASMI.MIMI NILISHAJUA MWANZONI KABISA HAYA YANGETOKEA KWA SABABU YA YEYE KUGOMA KUWANIA NAFASI YA UNGOZI.UHAI WA JUMUIYA HAIWEZI KUJA KWA JUHUDI ZISIZONAMWELEKEO KAMA NDESANJO ATAENDELEA KUWA KIMYA KTK MASWALA HAYA.WE FIKIRIA MWENYEKITI MWENYEWE AMEWAHI KUSEMA NINI KUBORESHA JUMUIYA?KAMA SI KILA KITU KUFANYWA NA VIONGOZI WENZAKE?NINI MAANA YA KUWA NA MWENYEKITI ASIYEJUA WAJIBU WAKE?HAPO KUNA TATIZO NDUGU ZANGU

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia