Teknolojia ya simu kwa maendeleo ama kuongeza upuuzi?
Siku hizi kila mtu ana simu ya mkononi. Na kama huna simu unaonekana kama mshamba flani hivi. Kijana gani huna simu? Na si tu kuwa na simu bali ughali wa simu yenyewe.
Tunaambiwa asilimia karibu 35% ya watanzania wanamiliki simu za kiganjani. Pengine hayo ni maendeleo.
Chukulia Tanzania ambayo ni nchi fukara kuliko hata zile zinazoitwa za ulimwengu wa tatu eti nayo katika hili la simu za mkononi unaambiwa ni kati ya nchi wateja wazuri wa teknolojia hii. Hapo unaona uhusiano wa simu hizi na akili za kimaskini.
Sasa tuachane na hayo. Tuje katika matumizi yenyewe ya hizi simu. Kusema kweli wengi wa watumiaji simu hizi, wanazitumia katika mambo ambayo kuainisha faida zake hasa si kazi rahisi. Simu ni mapenzi. Simu ni ngono. Simu ni kuongea upuuzi tu kwa mamia ya dakika. Na ni ajabu sana kwamba waathirika wakuu ni wanafunzi wa vyuo vikuu. Wasomi. Kama vile intaneti zinavyotumika kwa mambo ya kipuuzi na wasomi hawa, ndivyo simu nazo zinavyoendeleza kasumba ile ile: Matumizi wa teknolojia kuongeza upuuzi.
Simu zimekuwa zikiwakamua watu fedha bila ridhaa yao. Watumiaji wengi wa simu hawali kama zinavyokula simu wanazomiliki. Simu zinaongeza umaskini. Na ndio maana makampuni ya simu tunaambiwa yanapata faida kubwa ya kutisha hata kama wateja wao wengi wanaishi katika ufukara uliopitiliza viwango vya ufukara. Hii ni ajabu na kweli.
Imefika mahala tujipime upya kuhusiana na matumizi ya simu hizi. Kama hatuwezi kuzitumia kwa faida, bora kuishi kwa mtindo wa enzi za ujima. Si lazima ukubaliane nami katika hili. Ila jielewe kabla hujapiga simu.

Simu, mimi binafsi sijali kama mtu ananiita mshamba kwani hata nikiwa na simu ya shilingi moja si yangu yeye inamuhusu nini. Na pia kwa nini watu wanawasikiliza sana watu. Utawezaje kuwa na simu ya shilingi milioni moja halafu hujui utakula nini na utalala wapi kama si upuuzi ni nini? na pia kwa nini ununue simu kama unajua huna uwezo wa kunununua vocha. Ila wengi YOTE hii ni kutaka SIFA tu. Lakini hawajui kama sifa ni mbaya.Kweli simu ni upuuzi kuanzia leo nitatupa simu yangu au anayetaka anaweza kuipata.
JibuFuta