Kwa nini miungu ni mingi kiasi hiki?

Hakuna jamii ambayo haijawahi kuwa na wazo la uwapo wa nguvu iliyo juu ya asili ya ulimwengu. Nguvu hii imeitwa majina mengi lakini lililo maarufu ni mungu. Wengi wetu, hata kama hatuna ushahidi wa kujitosheleza, bado hatusiti kabisa kuamini kuwa mungu yupo.

Ukiangalia vyema utaona namna ambavyo dunia inayo miungu kwa maelfu, na kila mungu ana sifa zake tofauti na miungu wengine. India kwa mfano, tunaambiwa kuwa idadi ya miungu inaweza kuzidi hata idadi ya waumini wenyewe!

Na ni makosa kudhani kwamba wingi wa miungu hiyo ni majina tofauti tofauti kwa mungu huyo huyo. Sababu ni kwamba hata mahitaji yao yanatofautiana. Kanuni wanazotoa ili tuwafikie zinatofautiana. Tabia zao zinatofautiana. Kwa hiyo, ni wazi kuwa miungu wako wengi.

Sasa kwa nini dunia inayo miungu mingi hilo ndilo swali ninalotaka kukuachia leo. Inakuwaje kila jamii inavutiwa na wazo kuwa yupo mungu hata kama haonekani? Wapo wanaoamua mpaka kutengeneza sanamu kuhusianisha kile wanachokiamini na kitu kinachoonekana. Je, kuna sababu yoyote inayowafanya watu kuamini katika mungu? Je, asiye amini katika mungu ana tatizo fulani?

Jielewe

Maoni

  1. Mungu, kwa mimi pia inanipa taabu kwani nilidhani kuna mungu moja tu lakini sasa naona kama ulivyosema bwaya je kuna miungu mingapi. Kwani waislam wanamwani Muhamed, huko India sanamu na pia ngómbe. Na kuna wengine wana miungu yao ambayo wao tu wanaiona. Lakini pia kila kitu kinatokana na imani kwa hiyo inaonekana wote tuna imani tofauti.

    JibuFuta
  2. Hiyo sis Yasinta lazima ikupe taabu juu ya idadi ya miungu.Ukweli bila kujali dini gani kuna miungu mingi na hata Yule mungu mmoja wa wa-Kwenye biblia anakiri hivyo.Mungu anajua kuna miungu wengi ndiyo maana yeye anasisitiza kuwa...USIWE NA MIUNGU MINGINE ILA MIMI....au sehemu nyingine tunapo ambiwa kuwa YEYE NI MUNGU WA MIUNGU....hapo la muhimu ni kuwa katika hiyo miungu mingi yupi aliwaumba wenzake?Huyo ndiye atakuwa mkubwa wao.....

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia