Kwa nini tunatafuta kasoro zaidi? Mchango wa Nuru Shabani
Tuliwahi kuzungumzia tabia ya kuwaza kupenda kutafuta kasoro. Ilijitokeza michango kadhaa. Hapa ningependa kukuletea mchango mmojawapo uliojaribu kueleza sababu za watu kuwa na tabia hiyo. Namshukuru msomaji Nuru Shabani asiyeishia kusoma na kuondoka. Yeye kuacha maoni yenye lengo la kupanua mjadala zaidi.
Anasema:
"Watu wengi tumelelewa katika kuutafuta udhaifu au makosa ya mtu na ndiyo tunachokina zaidi kuliko uimara wake. Hiyo siyo asili ya mwanadamu ila ni malezi ambayo tumefundishwa na wazazi nyumbani,walimu mashuleni na jamii iliyotuzunguka.
Vitabu vya dini vinatuambia tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, sasa Mungu huyo ambaye ametuumba mbona haangalii kasoro zetu??
"Hii inaonesha kuwa tabia ya kukosoa ni ya kufundishwa na wanadamu wenzetu tena wale wasiojiamini na wenye kutazama mambo kwa upande mbaya.
" Kutizama mambo kwa mkabala hasi ni jambo ambalo tumekuwa tukifundishwa kila siku na watu ambao kwa namna moja au nyingine tumepita katika mikono yao kimalezi,na mbaya zaidi ukipita mikononi mwa wasiojiamini ndiyo hatari zaidi.
Chukulia mfano mtu ameamka asubuhi akajiandaa kwenda kazini akavaa nguo zake safi na akapendeza,njiani anakutana na watu wanamwagia sifa kedekede kuwa kapendeza sana hadi anajisikia vizuri ghafla anatumiwa ujumbe mfupi kwenye simu yake toka kwa mpenzi wake kuwa ameuvunja uhusiano wao, mtu huyu hili jambo la kukataliwa ndilo ambalo litachukua nafasi kubwa sana katika mawazo yake kuliko kule kusifiwa lakini angeweza kufikiria jinsi watu walivyokuwa wakimsifia jinsi alivyopendeza na akapata nafuu,lakini kwa sababu umefundishwa kuwa kukataliwa ni kubaya then ndilo litakalo kuwa kichwani haikuwahi kutokea hata siku moja ukafundishwa kusifiwa nako ni kuzuri zaidi.
Mfano mwingine katika kuelezea namna ya kuangalia mambo kwa mkabala hasi ni pale mtu anaposifiwa kwa kujenga nyumba nzuri,badala ya kusema asante nimejenga nyumba ile nzuri ili nikae pazuri yeye utamsikia akisema kakibanda tu kale,ukweli hatujawahi kufikiri mambo kwa upande chanya.Hatujawahi pia kuambiwa kukosea ni kuzuri zaidi kwani ndiyo unapopata nafasi ya kujifunza,tumeambiwa kukosea ni kubaya sana,mfano tunauona tulipokuwa wadogo siku tukipata maksi nzuri darasani wazazi wetu walitumwagia sifa nyingi na siku tukapata maksi za chini tuliadhibiwa sana hatukuwa kuambiwa kuwa tumefeli labda kwa sababu tumezidisha michezo ila tuliadibiwa,hali hii na nyinginezo za kufanana ndizo zinazopelekea watu wengi tukawa tunatazama mambo kwa mkabala ambao ni hasi"
Wewe unasemaje? Karibu tujielewe.

umetoa mifano mizuri na pia ni kweli sisi binadamu tunataka mazuri tu. Na pia hii ya kupata kikubwa, sifa wengi wanapenda. Tatizo hatuwezi kusema asante na wala hatutosheki na kile tulichonacho. sijui kama nimeeleweka
JibuFutaUmeeleweka vizuri Yasinta. Ni ajabu kwamba binadamu tunapenda mazuri ila hatuwezi kufundisha wanetu jinsi ya kuyafanya hayo tunayodhani kuwa ni mazuri. Badala yake tunatumia muda mwingi sana katika kuwafafanulia watoto wetu "mabaya" yote ya kuepuka. Kanuni. Sheria. Mzazi anasisitiza katika "usi..uki...kiboko...usi...uki...adhabu... usi..." Sentensi hizi zinaonyesha upande mbaya zaidi kuliko ule mzuri tunaoutaka!
JibuFutaTunasahau kuwa hizi "usi" hazifundishi tabia mbadala/yaani ule upande mzuri tunaoutaka. Kwa hiyo matokeo inakuwa kama anavyotuambia Nuru, tunajenga jamii inayotazama mabaya zaidi.
Tunakuwa sugu katika kutizama uzuri haa kwenye maisha yetu ya kawaida.
Hapo ndiko utakapoona udutu wa binadamu: Anataka mazuri kwa kusisitiza kinyume chake!
Nimepata elimu ambavyo sikutarajia kuipata kwa kiswahili.hongereni ndugu zangu
JibuFutagreat post. nuru nakupa big up
JibuFuta