Kamwe usikate tamaa
Haya tena. Siku zinakimbia kama nini vile. Ni juzi tu mwezi umeanza. Leo eti masaa machache yajayo mwezi unakatika hivi hivi. Mwaka ndio usiseme. Mwezi wa kumi na moja huu. Bado mwezi tu na mwaka ukatikie mbali.
Sijui kinachosababisha siku kukimbia namna hii. Muda ni mfupi kuliko matarajio. Mambo mengi kuliko dakika zilizopo. Kazi kweli kweli.
Binafsi mwezi huu umepita vizuri pamoja na changamoto za hapa na pale. Nafurahi nimeweza kuzitazama changamoto hizo kwa jicho la kujisahihisha.
Nawe ndugu msomaji bila shaka mwezi umekuendea vyema. Hata kama inawezekana umekumbana na changamoto mbili tatu hakuna haja ya kukata tamaa. Usikate tamaa. Kuna mtu aliwahi kuniambia picha nzuri kusafishwa kwenye chumba cha giza. Giza ni muhimu ili kusafisha picha. Maana yake yake unapojikuta kwenye hali inayofanana na giza vile, kwa maana ya changamoto, kukatishwa tamaa, chukulia hiyo kama mchakato wa kukutengenezea picha nzuri mbeleni.
Usikate tamaa. Pigana kiume. Songa mbele. Anza mwezi wa kumi na moja kwa mtazamo mpya. Jisahihishe. Tutafika.
Sijui kinachosababisha siku kukimbia namna hii. Muda ni mfupi kuliko matarajio. Mambo mengi kuliko dakika zilizopo. Kazi kweli kweli.
Binafsi mwezi huu umepita vizuri pamoja na changamoto za hapa na pale. Nafurahi nimeweza kuzitazama changamoto hizo kwa jicho la kujisahihisha.
Nawe ndugu msomaji bila shaka mwezi umekuendea vyema. Hata kama inawezekana umekumbana na changamoto mbili tatu hakuna haja ya kukata tamaa. Usikate tamaa. Kuna mtu aliwahi kuniambia picha nzuri kusafishwa kwenye chumba cha giza. Giza ni muhimu ili kusafisha picha. Maana yake yake unapojikuta kwenye hali inayofanana na giza vile, kwa maana ya changamoto, kukatishwa tamaa, chukulia hiyo kama mchakato wa kukutengenezea picha nzuri mbeleni.
Usikate tamaa. Pigana kiume. Songa mbele. Anza mwezi wa kumi na moja kwa mtazamo mpya. Jisahihishe. Tutafika.
Oh aise kumbe! nilijisahau kabisa kwa hiyo baada ya miezi miwili tunaingia mwaka mpya 2009. Mm kazi kweli kweli. Ila hata mimi nashukuru Mungu amenilinda mpaka leo ingawa siku haijaisha lakini nasema leo. Napumua na nimefanikisha yote niliyopanga karibu yote. Asante kwa kutukumbusha wengine
JibuFutaBwaya ahsante kwa ukaribisho wako na sasa nimeiongeza blog yako na Yansinta kwangu.
JibuFutaYansita usiwe na wasi wa kumshukuru Mungu kwamba bado unapumua kwani yawezekana kabisa kwamba kutokupumua ni kuzuri kuliko kupumua.
lakini nimependa msemo wako kwamba umefanikisha yote uliyoyapanga kwani kuyapanga tu tayari nimafanikio na unaelekea kuyatenda.
Yasinta na Kamala ni Mungu yupi manamzungumzia? Allah? Brahman? Wa Israeli? Ama yupi?
JibuFutasikujua kuna miungu yote hivi. Nilijua kuna mungu mmoja tu na haya ni majina tu ambayo watu wameamua kumwita
JibuFutaKama ni majina tu dada Yasinta mbona hata matakwa yao yanatofautiana? Yaani anachokitaka Mungu huyu, yule mwingine(jina lingine) anakikataa! Kwa maneno mengine makatazo ya huyu ni matakwa ya huyu!
JibuFutaNi imani tu kama unaamini mti ni mungu basi utaamini au nguruwe ni haramu basi
JibuFutaMungu, kwa maana hiyo, anabaki kuwa Mungu hata wapo miungu wengine wanataka kutuchanganya kwa kujifanya wanafanana nae. Changamoto yangu ni kuwatazama hawa miungu waliotapakaa kila kona kwa uangalifu mkubwa. Asante Yasinta. Siku njema
JibuFutamimi niliongelea Mungu kwa mustakbari alioongelea Yasinta, yaani Mungu wake. Vinginevyo kwangu mimi simjui Mungu aliyemaarufu, siju Mesish, sijui nani. mimi naijua Nguvu kuu (supreme being), nature maumbile etc.
JibuFutakimsingi ile nguvu ninayoiamini mini ni ile isiyokuwa na hasira na wala hamna siku itakapokuja kumhadhibu mtu. sio Mungu wa wakoloni a.k.a wazungu
mpo hapo?
Kamala,
JibuFutaKwa nini unafikiri kuna nguvu iliyo kuu? Na hizo sifa ya nguvu hiyo umezipataje pataje? Kwamba haina hasira na haiwezi kuadhibu mtu, umefikiaje hitimisho hilo?
kwa vyovyote kuna nguvu inayoendesha haya mambo, kuna nguvu ambayo ni ya ajabu katika hufanyaji kazi wake.
JibuFutanguvu hii wakristo huuita Mungu na waislamu huiita Allah, kila mtu hujiona yuko sahihi lakini wanasayansi ndio basi kwani wao huiita Nguvu tu kama ilivyo. siku zote wanasayansi hukataa kuwepo kwa mtu anayeitwa Mungu lakini hukubali kuwepo kwa nguvu na wanasema kuwa nguvu haiwezi kubadirishwa wala kuharibiwa na wala kupindishwa!
uwepo wa nguvu unaonekana tu wenyewe, biblia inasema tumeumbwa kwa mfano wa Mungu kwa hiyo basi na sisi ni nguvu au Roho kama ilivyo hiyo Mungu.
sisi kama binadamu mawazo yetu, maneno (kauli) yetu, yananguvu kuliko tunavyofikiri na hubadirisha na kutupangia maisha yetu. kwamfano, Tanzania sio nchi masikini na wala watanzania sio masikini bali ni nguvu ya Hoja ya watu fulani na sisi kuipokea na kukubali ndivyovinatufanya kuonekana masikini - Nguvu hizo!
Dini nyingi huamini kwamba nguvu hiyo (Mungu) inahasira na inachukia baadhi ya watu wanaofanya kinyume na maneno ambayo kimsingi ni mapendekezo ya watu waliopita, hii sio kweli!
nguvu hii ipo na inapenda kila mtu na kila kitu na haihitaji chochote kutoka kwa yeyote isipokuwa ipo kupenda na kupenda tu.
iko sawa na umeme wa pale Mtera, ukifika mtera huwezi kuona umeme kwa macho na hukuna aliyewahi kuuona umeme japo tunautumia kila siku. wala mtera haijui hasi na chanya, mpaka short ikitokea na kudhuru, yenyewe haijui! inajua kuendelea kuwepo! muifuate mtera na kuileta kwa nguzo mijini msiifate, yote sawa ila nyie msioifuata mdo mmnaopoteza! (mtalala gizani etc)
nguvu hii ufikiwa kwa upendo kwani asili yake ni upendo usiowamasharti wala wa kulipiza! hufikiwa kwa sayansi ya Roho (science of the soul)
wanasayansi wetu wanasema hakuna mungu na hii ni kweli kwani Mungu hawezi kupatikana kwa majaribio ya kisayansi, bali kwa majaribio ya sayansi ya roho na hapa ninamaanisha "tahajudi/taamuli-meditation! ambayo hutumika kutuunganisha na Nguvu kuu kama zifanyavyo nguzo na nyaya kwa kuunganisha Nyumba zetu, miji yetu viwanda vyetu nk na chanzo cha umeme yaani mtera
ni hayo kwa leo
Bwaya,kamala na yasinta hongereni sana kwa michango yenu.
JibuFutaNingependa kuungana na Kamala kuwa hakuna kitu kinachoitwa Mungu,kama wengi tulivyoambiwa.
Zamani kabla hawajaja wakoloni(wazungu na waarabu) hakukuwa na kitu kinachoitwa Mungu,wao waliamini ktk Nguvu kuu.Ndiyo maana utakuta wengine waliamini ktk miti wengine katika majabali,na kikubwa ndugu zangu ieleweke wengi wa watu wa zamani waliamini zaidi katika kanuni za kimaumbile ndiyo ilikuwa msingi wao.
Kwa mtazamo wangu wengi hatumwelewi mungu sana tunachofanya ni kujenga hofu kwa Mungu,linapokuja suala la kutaka kumjua huyo mungu kwa undani utaambiwa unakufuru,sasa mi huwa ninajiuliza iweje utake kujua asili za aliyetuumba uambiwe unakufuru?Haingii akilini umuulize mzazi wako asili yake wapi akuambie unakufuru.
kwa kukazia mchango wa kamala kuna wakati mtu akishindwa jambo husema ni mpango wa mungu,lkn ukichunguza utagundua kuna baadhi ya kanuni za kimaumbile hazikufutwa ndiyo maana likashindikana hilo jambo.
ninaweza kukubaliana na wanasayansi kila kitu kinaendeshwa na kanuni za kimaumbile na kanuni hizo zinaratibiwa na nguvu kuu ambayo wengi tunaiita ni mungu.
Mi nimejaribu sana kuongea na watu wengi ambao tunaona wamefanikiwa kikubwa wengi ukiwachunguza utaona walifuata kanuni za kimaumbile zaidi ingawa wengi husema mungu amenisaidia kufika hapa.
pia hata ukienda makanisani na misikitini hafundishi ukweli kuhusu huyo mungu wengi tunamuoona ni mungu wa hasira mungu wa kulaani mungu wa kuwapa mikosi,mungu wa kuadhibu.Hivi jamani ni nani ambaye anaweza akaumba kitu na kisha akakiaadhibu?sanasana atakuwa anakifanyia marekebisho kionekane ni bora zaidi.Tumeona wagunduzi wa vitu mbalimbali duniani huzidi kuviboresha vile vitu walivyovivumbua.Huku unaambiwa ameadhibiwa na Mungu,mi nadhani kuna haja ya kulitazama upya suala la mungu.
Nuru, Kwa nini unafikiri kuna nguvu inayoratibu kanuni za maumbile?
JibuFuta