Je, hatuwezi kuishi bila ngono?

Siku hizi ni kawaida watu kukutana kimwili  bila ndoa. Ndio maana neno tendo la ndoa halitumiki. Ni ngono. Na hata hivyo inaonekana pia chaweza kufanyika bila mapenzi, kwa hiyo wakabatilisha kukiita kufanya mapenzi. Hiyo ndiyo hali halisi.

Mjadala wenyewe ulikuwa katika kuhoji ikiwa kijana wa kisasa anaweza kufikisha miaka zaidi ya ishirini na tano bila kuonja ngono(na kijana mwenyewe asiwe mgonjwa, kwa maana ya hitilafu katika mfumo wake wa uzazi) Je, anaweza kuahirisha kuanza ngono hata kama mwili wake unamshawishi kufanya hivyo? Maana inasemekana kwa mujibu wa wadau hawa, katika siku za leo, ngono haikwepeki!


Wewe unasemaje? Ngono ni kama chakula? Kwamba usipoipata utaumwa? Na je, haiwezekani kuwa na mahusiano ya karibu (mno)lakini 'no' ngono? Na kwamba huu mtindo wa kuanza ngono mapema kwa vijana wengi unasababishwa na nini? Ni mwili tu ama ni tatizo la kisaikolojia zaidi? Kwamba ni kujilemaza fulani hivi kuwa aah kila mmoja anafanya bwana?
Jielewe

Maoni

  1. Bro mambo niaje? Hyo mada mkuu iko juu kimakini kweli,kwa hapo sina cha kujibu wala kuongezea .

    JibuFuta
  2. DUU kaka hii kitu ipo makini sana nafikiri ni jambo bora mtu kujiuliza namna gani unaweza kuishi bila ngono. hivi inawezekana japo siku moja kubanjuka tu? labda inawezekana hebu soma maelezo ya daktari mmoja wa Cape Town labda mimi sielewi.
    "Three or more orgasms a week are beneficial to your healthy. Ejaculation does reduce prostatic congestion and usually improves the symproms of chonic prostatitis"
    By Dr Werner Botha
    Capte Town.

    mimi sielewi mistari yake hebu nipeni somo kwanza hata nilikoipata nako taabu kwelikweli.

    JibuFuta
  3. kufanya ngono au kufanya mapenzi kama wengi tulivyozoea kuita,ukweli ni kwamba wengi tunafanya bila ya kujiuliza.Sehemu kubwa ya jamii inajitumbukiza katika kufanya ngono si kwa sababu ya uhitaji wa kimwili bali ni utashi na ni kama fasheni. Na ndiyo utakuta mtu amalizapo kufanya hiyo ngono huwa kuna kujuta sana na mawazo yanakuwa mengi na kuichukia hiyo ngono.Hii inaonyesha wazi kuwa wengi hufanya si kwa hitaji la mwili bali kwa tamaa ya mwili.Nakumbuka kuna mada aliwahi kuiandika lui ikisema Kijana tunza mbegu zako,ktk mada hiyo lui aliwasihi sana vijana waache kumwaga mbegu zao hovyo kwenye vijishamba bali wasubili wazimwage kwenye mashamba yao halali,ili waweze kuzitunza na kutoa mazao mazuri.
    Ukweli wetu hufanya ngono kwa kufuata utashi wa mwili tu na si vinginevyo.Hakuna ushahidi wa mtu ambaye hajafanya ngono muda mrefu akawa ameathirika kilichopo ni maneno ya vijiweni tu ambayo wengi huwa tunadhani yana ukweli wowote.
    Kwa mtazamo wangu tunaweza kuishi bila kufanya ngono kwani kufanya ngono sio lengo kuu kama wengi tunavyoamini na kufikiria.

    JibuFuta
  4. @ Shayo, Karibu sana.

    @ Mpangala, kwamba ngono ina faida kiafya, hilo ni suala la mjadala. Maana hawa wanaoitwa wataalamu mara nyingi huzisemea hisia zao kwa lugha ya kisayansi! Si mara zote kauli zao ni za kuaminika.

    @Nuru, kama ngono ni utashi, mbona kampeni za UKIMWI zinakwama? Utashi maana yake tungeshafanikiwa siku nyingi kuutokomeza! Mbona pamoja na kusambaza elimu ya kujikinga nayo, na kusema kweli kila mmoja anajua walau kwa sasa, bado UKIMWI unasambaa kwa kasi ya kutisha?

    Mimi hili linanifikirisha: Kwamba hata huyo anayeendesha kampeni ya kupambana na UKIMWI bado yeye mwenyewe anashindwa. Unaelezeaje hali hii kwa kuhusianisha na utashi ngono?

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Pay $900? I quit blogging

Uislamu ulianza lini?