Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2017

Thamani Yako Inategemea Namna Unavyowasaidia Wengine

Picha
PICHA: Lifehack KUNA ukweli kwamba katika harakati za kutafuta mafanikio, unahitaji kuwa na uhusiano mzuri na aina fulani ya watu. Hawa ni watu wanaokuzidi kile unachotaka kukifanya na kwa namna moja au nyingine wanaweza kuwa msaada kwako kwa kukupa mtaji wa kutekeleza wazo lako, kukunganisha na nafasi za ajira zisizotangazwa hadharani au kukusaidia mawazo yatakayokupeleka mbele kimaisha.

Je, Walimu na Wazazi Wanazungumza Lugha Moja Kujenga Maadili ya Watoto?

Picha
PICHA: Godot13 SUALA la maadili limezua mjadala mrefu katika siku za hivi karibuni hasa baada ya wanasiasa kupinga wasichana wajawazitokuendelea na masomo yao kwa sababu ya ujauzito. Kauli hizo zilipingwa vikali na wanaharakati wenye msimamo wa kuwatetea watoto wa kike . Hoja yao ni kwamba kumnyima msichana fursa ya kupata elimu kwa kosa la kuwa mhanga wa mfumo holela usiomjenga msichana kimaadili ni kutokuyatazama mambo katika upana wake.

Madhara ya Kumpeleka Mtoto Shule ya Bweni

Picha
PICHA: Daily Maverick Moja wapo ya sababu nyingi zinazowasukuma wazazi kuwapeleka watoto wadogo kusoma shule za bweni ni mafanikio ya taaluma. Mazingira ya shule yanaaminiwa kuwa bora zaidi katika kuwasaidia watoto kufanya vizuri zaidi kuliko wanapokuwa nyumbani.

Kitabu Kipya cha Malezi na Makuzi

Picha
Malezi ya sasa yamekumbwa na changamoto nyingi na kusababisha watu kushindwa kuwasaidia watoto na vijana wao ili kufanikiwa. Mmomonyoko wa maadili umekuwa chanzo kikubwa cha matatizo yanayomkumba kijana na jamii kwa ujumla. Matatizo hayo ni kama vile ukosefu wa ajira, kushindwa kufikia ndoto za maisha, migogoro katika familia, pamoja na watu kushindwa kuwa na utulivu na amani.

Kukosa Ajira Kusikufanye Ukose Kazi

Picha
Inakadiriwa kuwa kati ya watu 800,000 na 1,000,000 hapa nchini wanaingia kwenye soko la ajira kila mwaka. Hawa ni vijana wanaomaliza masomo yao kwa ngazi mbambali za elimu au wale wanaokosa nafasi ya kuendelea na masomo katika mfumo rasmi wa elimu.

Je, Shule za Bweni Zinafaa kwa Malezi ya Watoto Wadogo?

Picha
PICHA: SOS Schools Ongezeko kubwa la shule za bweni kwa watoto wadogo ni kiashiria kimoja wapo cha mabadiliko ya kijamii yanayoendelea kuathiri desturi za malezi. Pamoja na changamoto zake, mzazi anapofanya maamuzi ya kumpeleka mwanae shule ya bweni huamini anafanya hivyo kwa faida ya mtoto.

Chuki Unakuumiza Wewe Kuliko Unayemchukia

Picha
PICHA:  PM Notes MIAKA kadhaa iliyopita nilikosana na mtu ambaye awali tulikuwa karibu kikazi. Nilimwamini kama rafiki tuliyefanya kazi pamoja. Sikufikiri angeweza kujitafutia sifa binafsi kwa kunihujumu. Kilichoniumiza si tu kutendewa osa la makusudi, bali kuona mtu niliyemheshimu akijaribu kufikia malengo yake kwa kujaribu kuniharibia kazi yangu.

Kwa nini Wazazi Huwapeleka Watoto Wadogo Shule za Bweni?

Picha
PICHA: The Citizen Miaka kadhaa iliyopita, wakati huo nikiwa mwanafunzi, nilishangazwa kusikia mtoto wa ndugu yangu, wakati huo akiwa na miaka sita, alikuwa anasoma shule ya bweni. Sikufikiri jambo hilo lingewezekana.                                                                                     Nakumbuka mara yangu ya kwanza kwenda shule ya bweni nilikuwa na umri wa miaka 17 nikisoma kidato cha 5. Kwa kuwa haikuwa rahisi kwangu kuzoea maisha ya mbali na nyumbani, nilishindwa kuelewa inawezekanaje mzazi kumpeleka mtoto mdogo kiasi hicho kwenda shule ya bweni.

Upendeleo wa Wazazi Unavyoweza Kuchochea Uadui kwa Watoto

Picha
PICHA: Aim Lower Journal KUNA kisa kimoja kwenye biblia kinachoweza kutufundisha jambo muhimu kama wazazi. Kisa chenyewe ni kile cha Yusufu, mtoto wa mzee Yakobo, aliyejikuta kwenye mtafaruku mkubwa  na ndugu zake. Ugomvi wa Yusufu na kaka zake ulikuwa mkubwa kiasi kwamba kaka zake waliazimia kwa pamoja kumwuuza Misri kama adhabu. Jambo la kuzingatia ni kwamba ugomvi huu wa Yusufu na ndugu zake haukutokea kwa bahati mbaya. Chanzo cha yote hayo ni upendeleo.

Mambo ya Kutafakari Unapoanzisha Uhusiano wa Kimapenzi Kazini

Picha
PICHA: Shalinii Choudhary   Sehemu kubwa ya maisha yako kama mfanyakazi unaitumia kwenye eneo la kazi. Ingawa inategemea na aina ya kazi unayoifanya, ni wazi muda mrefu kwa siku unaoutumia kutekeleza majukumu yako unakuweka karibu zaidi na wafanyakazi wenzako kuliko hata familia na marafiki. Mazingira haya ya ukaribu wa kikazi, wakati mwingine, yanatengeneza uwezekano wa uhusiano wa kimapenzi baina ya wafanyakazi.

Kipimo cha Uadilifu Wetu ni Namna Tunavyopambana na Mimba za Utotoni

Picha
PICHA:  Huffington Post NINGEPENDA kuamini, katika mjadala unaoendelea kuhusu mimba za utotoni, kila mchangiaji bila kujali mapendekezo yake, anatamani kuona tunamaliza tatizo hili. Hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kutetea watoto wa kike kupata ujauzito katika umri mdogo.

Tunavyoweza Kuboresha Vituo vya Malezi

Picha
PICHA: John-Paul Iwuoha MALEZI katika vituo vya kulelea watoto hayakwepeki. Katika mazingira ambayo wazazi wanafanya shughuli zao mbali na nyumbani kituo cha malezi kinakuwa msaada. Tafiti za malezi zimekuwa zikijaribu kuangalia namna gani huduma hizi zinavyoweza kuboreshwa. Moja wapo ya mashirika maarufu katika eneo hili ni   Taasisi ya Marekani ya Mtandao wa Afya ya Mtoto na Maendeleo ya Utafiti wa Malezi ya Watoto (NICHD) .