Kitafute hiki cha Stephen R. Covey




Kitabu hiki ni kati ya vitabu ambavyo unahitaji kuvisoma kwa faida yako mwenyewe. Sitangazi biashara, natangaza maarifa ya bure ambayo huhitaji kulipia 'tuition fee' kuyapata.

Kama wewe ni kati ya watu wanaopenda kuwa na mafanikio ya kikweli kweli, kitabu hiki cha Seven Habits of Highly Effective People si cha kukikosa.

Nilikipata Moshi kwa Sh. 22,000.00, sijajua bei yake kwa maeneo mengine.

Maoni

  1. Unafanya vizuri kuhamasisha usomaji wa vitabu. Unaonyesha mfano bora kwa kununua kitabu, pamoja na kuwa bei ni sh. 22,000.

    Katika maandishi yangu, ikiwemo kwenye blogu na gazeti la KWANZA JAMII, nawalalamikia sana waTanzania, kwa sababu ni wagumu kununua vitabu au kuvisoma, labda viwe ni vitabu vya udaku. Wakisikia umenunua kitabu hicho cha elimu ya maisha kwa sh. 22,000 watakushangaa. Lakini ukienda baa ukawatwanga "ofa" ya sh. 22,000 watakuheshimu sana. Lakini, usichoke. Uko kwenye njia sahihi.

    JibuFuta
  2. Sijui ni utamaduni au ni uduni umetamalaki maana kununua vitabu visivyo vya udaku au mapenzi imekuwa ngumu sana kwa waliowengi hasa wanafunzi wa vyuo vikuu kama si kwa maagizo ya lecturer au profesa hawanunui vitabu. Lakini ni kwa kiasi gani wanaspend kununua vocha za simu, pombe sigara na "pamba" huwezi amini ankara zao. Asante kwa kutujulishwa nitakitafuta

    JibuFuta
  3. Kaka natumai watu kama wewe ni wachache sana. Kwa Bukoba kukipata imekuwa ni ngumu, hivyo naomba unisaidie kukitafuta ukikapa tuwasiliane nitume fedha. Mawasiliano ni akawamala2007@yahoo.com au +255 715 017 062
    Ahsante sana

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?