Katika hili Mzumbe wana kesi ya kujibu

Kwa muda sasa zimekuwepo shutma (siku hizi zinaitwa kelele nyingi) kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kimetengeneza vihiyo wengi. Ni jambo la kusikitisha kwamba shutma hizi, kadri siku zinavyokwenda zinazidi kushika kasi kiasi kwamba sasa jambo hili limechukua ‘urasmi’ fulani hivi ambao kwa hakika si wa kupuuzwa.


Juzi tu, mzalendo mmoja alikuja na maelezo yakinifu akidai kwamba kwa utafiti wake, kagundua kwamba ‘kuna matapeli’ kibao ambao wanakula kuku serikalini kwa jina la ‘Dakta’ lakini hawana lolote. Wahusika hawakutujibu (na kwa kweli sikutegemea wajibu kwa sababu) msomaji mfuatialiaji wa mambo atakubaliana nami kwamba habari hizi si za leo. Zimeanza miaka kadhaa iliyopita. Na wahusika hao wanaendelea kudunda mpaka leo.

Hivi sasa unaposoma habari hizi, inasemekana baadhi ya ‘madakta’ hawa wamerudi shuleni kwao Mzumbe kurekebisha mambo kimya kimya. Huo ni ushahidi kwamba hata kama wanajidai hawasikii, lakini ‘waimeipata,’ kwamba ujambazi wao wa kitaaluma hatimaye umebainika.

Hofu na mashaka yangu yapo kwenye Chuo hiki cha Mzumbe. Sasa hivi hadhi yake ni wazi imetiwa doa kuuubwa na kashfa ya kumiliki ‘madakta’ feki ambao kimsingi hawana sifa wanazojinadi nazo. Kwa mujibu wa habari zilizozagaa mtaani, inasemekana ‘wanataaluma’ wengi wa chuo hicho ambao awali ilisemekana kuwa wana shahada za uzamifu, sasa hawatambuliki kwa sifa hizo.

Swali kwa menejimenti ya Chuo hicho ambacho zamani kiliitwa Chuo cha Serikali za Mitaa Mzumbe; Mnatufundisha nini? Tutakuwa na hakika gani na ubora wa taaluma yenu?

Huu, ndugu zangu ni ulemavu ambao umesababishwa na hulka yetu ya kusaka vyeti zaidi kuliko maarifa. Tunathamini sana uhitimu wa makaratasi kuliko uelewa wa kweli.

Ndio maana mimi siamini kabisa kwamba ile tu kupitia shule ni sifa tosha ya kuitwa ‘msomi’. Wengi wetu huenda tukawa’wasomaji’ badala ya ‘wasomi’ kama tunavyodhani.

Itashangaza sana kama Chuo Kikuu Mzumbe hakitawataka radhi watanzania kwa upungufu huu ambao sasa umeanza kuonekana kama ‘sifa rasmi ya chuo hicho’ yaani kumiliki wahadhiri vihiyo, na kutengeneza PhD ‘feki.’

Maoni

  1. This is very serious! Kwa kuwa aliyekamatwa na ngozi ndiye mwizi, mzumbe university wanatakiwa kutoa tamko.

    Lakini je wangapi wezi wa mbuzi hawajakutwa na ngozi?.
    Kuna haja ya kujua je hizi menejimenti za vyuo na taasisi nyingine za elimu wanaojihusisha na tunuku feki wanasifa gani na wamezipata kwa njia gani hata zikawawezesha kuwa walipo sasa. Si ajabu nao ni vihiyo.
    Badala ya kuhangaikia dalili za tatizo hebu tujue nini chanzo cha yote haya! Je mfumo wetu wa elimu unawawezesha walengwa kuwa watumishi bora..
    Je sera na mikakati ya elimu iliyowekwa inaweza kuwaondoa wanafunzi wa tanzania katika kujariri hadi kuwa na uwezo wa kutumia elimu yao katika mazingira tofauti?
    Je mitaala yetu hailengi katika kuandaa vihiyo hao? Bila shaka tatizo ni kubwa

    JibuFuta
  2. Mzumbe is notorious for bogus certificates. under normal circumstances one would expect a section of masters students, no matter how small it is, to fail to graduate in their respective years. the story is different with Mzumbe. all graduate successfully , no one is left behind. all you have to have is the much-sought registration with the univ.

    wengi wao wanapitia mikono kama hii kwenye link hii http://issamichuzi.blogspot.com/2009/10/research-consultancy-services.html#comments

    Chuo kituambie

    JibuFuta
  3. Mzumbe wanaumwa ugonjwa wa NJAA

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?