Ni kukosa muda ama kukosa kipaumbele?

Kimya cha blogu hii hakikutarajiwa ila huenda ni matokeo ya uzembe. Ni wazi bado sijaweza kushika mbili bila kuponyokwa na kimoja. Na nasikitika sana kwamba kinachoniponyoka mara kwa mara ni blogu.

Nimekuwa nikifikiri inakuwaje huwa sikosi muda wa kula (na kwa kweli napenda kula) hata kama nimebanwa na vitu kedekede? Kwa nini 'sikosagi' muda wa kuzungumza na marafiki zangu kwa kusingizio cha kubanwa?

Hitimisho likawa, huenda ni suala la kipaumbele tu na tabia ya kutokujitimizia ahadi ninazojiahidi. Kwamba inakuwa vyepesi kutimiza ahadi ya nje (na watu wengine) badala ya kutimiza ahadi niliyojiwekea na nafsi yangu.

Kwamba kwa nini nisithamini ahadi na nafsi yangu kwanza, ndipo nithamini ahadi na wengine? Kwa nini mtu mwingine akinipa kazi ya kufanya ambayo nina uhakika ina maksi, ninakuwa mwepesi wa kuifanya kwa mazingira yoyote yale (hata ikibidi kujinyima mengineyo kwa uchu tu wa alama za mtihani) and yet nashindwa yale yangu binafsi yasiyo na shinikizo lolote la nje (hiari)?


Ninafanya jitihada za kufikia mahali pa kuweza kupangilia vyema masaa ishirini na manne ili niweze kukidhi hamu yangu ya kublogu kwa furaha.

Maoni

  1. Ni kweli kaka bwaya umepotea sana. Ni furaha kuwa umerudi tena na ni kweli usemavyo kuna wakati mtu hujisikii kublogu au kufanya chochote. Kwa hiyo ni lazima ufuate moyo wako usemavyo/utakavyo. Asante kwa ujumbe na pia kwa kujua u salama.

    JibuFuta
  2. Nilitaka kutoa jibu kulingana na MTAZAMO wangu lakini nikawaza na kutambua kuwa maana pekee ama umuhimu wa jibu ungekuwepo kama lingekuwa linasaidia kuleta suluhisho.
    Kwa bahati nzuri yaonesha unalo suluhisho, hivyo ninaloweza kusema ni kuwa haijalishi kama ni MUDA ama KIPAUMBELE, kinachoonekana sasa ni kuwa unataka kutoa KIPAUMBELE KWA VYOTE hivyo umeamua KUPANGA MUDA KWA VYOTE
    Na hilo ndilo lililo kuu
    Baraka kwako na kwa mipango yako myema.
    Blessings

    JibuFuta
  3. Kuna wakati unaweza kukosa muda hata kwenye vitu ulivyovipa kipaumbele

    JibuFuta
  4. Yasinta, sijawahi kujisikia kutokublogu. Moyo wangu unataka kublogu sana ila najikuta nashindwa kufanya hivyo! Mara nyingine najipa sababu zinazoeleweka, lakini bado sipati amani na hali hiyo ya kutamani kublogu bila kuweza kublogu kwa sababu nisizozitaka!

    Tatizo ninalopigana nalo hivi sasa ni namna ya kuweza kupangilia vyote viende kwa uzito unaotakikana.

    Anachokisema Chib kimenitafakarisha. Mwanzoni nilidhani ni kipaumbele, lakini sasa ninadhani ni suala linalozidi hapo. Huenda lipo ninalotakiwa kulifanya zaidi.

    Mube bila shaka uzoefu wako utanisaidia zaidi.

    JibuFuta
  5. Yameongewa mengi, na yamegusa karibu kila kinachostahili kuongewa.
    Kuna wakati unaweza kushtu kia tu mda umepita na hakuna cha maana kilichofanyika. Naona ni vema sana kama tutakuwa na ratiba nzuri ya yale yatuhusuyo na tunayoona yanahitaji uwepo wetu.

    JibuFuta
  6. Tatizo si muda, wala tatizo si mvuto tatizo ni kwamba "sisi" hatuna malengo ya mbele sana, hupenda kupanga malengo ya muda mfupi yanayoonesha matokeo ya haraka, kukosa tabia ya kustik katika malengo binafsi na kujali zaidi external presure. Ur not determined to fulfil ur mision. Ndio chanzo hata cha ufisadi. Plz wajibika ipasavyo

    JibuFuta
  7. Tukumbuke Blogu si muhimu ukitafakari.:-(

    Na kama una njaa kumbuka KUBLOGU si muhimu kama kama kunya.:-(

    Samahani KUMBUKA hizi kweli si lazima ziwe NI kweli zako!:-(

    JibuFuta
  8. Mdoti nimepata vyema ushauri wako. Nitajitahidi kuwa determined zaidi ya ilivyo hivi sasa.

    Kitururu pengine umuhimu wa kublogu unategemeana na anachokisema Mdoti. Mwanablogu akiwa determined kublogu kwake kutakuwa muhimu kuliko yule asiye determined.

    Huu unaweza kuwa ukweli kwa kadiri ya kanuni na si kwa kadiri ya maoni. Nadhani.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?