Uhai na mashaka ya chanzo chake

NILIWAHI kujadili kuhusu suala la mkinzano uliopo kati ya sayansi na dini. Sayansi siku hizi haina mvuto kwa vijana wa leo. Unahitaji kuwa mwehu kuijadili.

Kimsingi, tangu zamani binadamu amekuwa akijaribu kudadisi asili yake yeye mwenyewe na viumbe wengine. Hilo limekuwa ni mjadala wa binadamu wengi. Kujua hasa ulipotokea uhai na kisa cha kuwa na viumbe wengi kiasi tukionacho leo.

Suala hili limejaribu kushughulikiwa kwa njia za kiimani, ambapo wanadamu mwanzoni kabisa waliamini kuwa uhai umeasisiwa na nguvu iliyojuu ya ufahamu unaoelezeka, yaani Mungu. Wafuasi wa imani hii hawahesabiki katika sayari tunayoishi. Ni wengi hata kama si wote katika hawa wanasadiki kiukweli kweli hicho wakiaminicho.

Katika hao wachache walishindwa kusaidiki kwa dhati dhana ya uumbaji, jumlisha maendeleo ya ukuaji wa maarifa yenye juhudi za kujua yanayohisiwa kujulikana, wapo binadamu ambao walianza kusita kukubaliana na ‘imani’ hii kwa madai kwamba ‘inalirahisisha mno’ suala gumu kwa maelezo ambayo yanaonekana kukimbia tatizo. (Wapo binadamu hupenda majibu magumu kwa suala lolote wakidhani huo ndio usomi.)

Hawa, kwa kutumia maarifa na mpangilio mkubwa wa hoja zenye kutafuta ushahidi, nao wamefanikiwa kuwa na ufuasi wa haja katika dunia ya leo. Kwa kadiri ya maelezo yao, inasemekana uhai, haukuumbwa kama inavyoaminiwa na halaiki, bali umetokana na mabadiliko ya kimaumbile ya vitu mbalimbali.

Watu hawa hawakuanza moja kwa moja kama wanasayansi. Ilianza kinadharia, kwa maana ya mpangilio wa hoja za kuhoji uhalali wa kukubaliana na urahisishaji wa majawabu kwa swali gumu. Ndiposa, zikaja hizo zinzoitwa tafiti za kiuchunguzi ambazo baadaye zilikuja kusimamisha hicho kinachoitwa ukweli kwamba uhai ulitokea na wala haukuumbwa.

Nadhani sasa ni wakati muafaka kulijadili hili kwa uzito unaostahili.

Je, nini chimbuko la uhai? Kwa nini viumbe wenye uhai wanatofautiana?

Haya ni maswali yaliyopembezoni kabisa mwa upuuzi. Yakifikiriwa kwa uzito mujarabu, yanaweza kutuongezea changamoto ambazo si lazima zitusaidie.

Itaendelea

Maoni

  1. Hivi kwani uhai nini?Tunauhakika waliokufa hawajisikii wako hai?

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia

Pay $900? I quit blogging