Kanuni za maumbile na ufahamu wa mwanadamu

Hewa (ambayo nayo tunaambiwa it just happened) ina mchanganyiko wa gesi mbalimbali ambazo zipo kwa uwiano maalumu. Oksjeni lazima iwe kwa asilimia kadhaa, hewa-ukaa nayo iwe asilimia kadhaa na kadhalika. Uwiano huo ukiharibika kwa nukta chache sana, lazima madhara yatokee. Hoja yangu hapa ni iweje hewa hizi ambazo tunaambiwa zilitoke-ga ziwe kwa mpangilio ambao hautakiwi kabisa kuvurugika? Kama ni kwa habari ya by chance, kwa nini itokee kwamba uwiano huo uwe namna ile tu ulivyo?

Niliachana na Fizikia miaka kadhaa iliyopita pengine ningekuwa na mifano mingi katika eneo hilo. Lakini hiyo hainifanyi nisahahu kuwa mwenendo wa dunia yenyewe unaonesha kutawaliwa na nguvu ili kuu zaidi. Mfano rahisi ni namna dunia inavyozunguka kwenye mhimili wake. Hakuna kukosea. Njia ni ile ile miaka nenda miaka rudi. Kama dunia ingekuwa imetokea-ga tu basi lingekuwa jambo linalowezekana kuwa siku moja dunia ingepotea njia na kwenda kusikojulikana. Kanuni zinazoongoza mzingo wa dunia zinaonekana kuheshimu mwongozo ulioziweka. Hata wagunduzi wa kanuni hizo hawawezi kutenda kinyume cha kani hizo. Nafasi yao pekee ni kudadisi tu utendaji wake.

Kwa maelezo yote hayo niliyoyatoa, ni wazi kuwa msomaji atakuwa amenipata kwa kiasi fulani hiki ninachojaribu kukisema; kwamba sayansi imetusaidia kubaini kanuni za maumbile zinazotawala utendaji wa maumbile yenyewe na namna kanuni hizo zinavyofanya kazi. Mara nyingine watu wenye maarifa hayo wameweza kuiga kanuni hizo kwa minajili ya kurahisisha maisha ya mwanadamu na viumbe wenzie hata kama hawezi kabisa kutenda kinyume cha kanuni hizo za msingi.
Lakini ajabu ni kwamba baada ya mafanikio yote hayo, watu hawa wanataka tuinue shingo na kujiaminisha kwa bidii kabisa kwamba hakuna Mwasisi wa kanuni hizo.


Niliwahi kumsikia Daktari mmoja wa Baolojia baada ya kuwa amefaulu sana kuelezea namna sayansi inavyoweza kutumika ‘kumtengeneza’ mwanadamu asiye na wazazi akaamini hiyo ni tiketi ya kuwa atheist . Kiburi chake kilikuwa ni kwa sababu inawezekana kutumia seli moja ya mwanadamu, kuikuza na ‘kumfanya’ mwanadamu mwingine. Akasahau kwamba huo ulikuwa ni ‘uigaji’ wa kanuni za maumbile ambao hauendi zaidi ya hapo. Maarifa hayo hayana tofauti na Wanafizikia walioiga jicho kutengeneza kamera. Hayo yote ni sawa na kujua kutoa kopi ya karatasi yenye maandishi halafu ukadai haki miliki ya karatasi halisi. Kumbe ulichofanya ni kujifunza kanuni na kuzitumia na sio kuzivunja.

Ni wazi kuwa sayansi inatupa ushahidi wa moja kwa moja kuimarisha imani zetu kwamba Muumbaji wa vyote hivi anao uwezo usioelezeka kwa lugha inayoeleweka. Na usemi kwamba '...mpumbafu amesema hakuna Mungu...' unathibitika.


Nikirudi nitajaribu kuangalia namna gani dini na sayansi vinaweza kufanya kazi pamoja.

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?