Salamu kwako mwanablogu mpenzi

Ni mwaka unakimbia ama ni sisi tunakimbia? Masaa yanakwenda. Majuma yanayakatika. Mwaka huo unayoyomea. Bila kukaa sawa, mtu unajikuta mwaka umekatika ukikuacha unashangaa. Kazi ipo. Mwezi wa kumi huu!

Nimeandika kukusalimu ewe mwanablogu. Mie sijambo, nakula asali na maziwa yake kwenye nchi ya ahadi. Ni bukheri wa afya njema.

Maoni

  1. Ni kweli mwaka huu uanakimbia sana na watu tunazidi kuzeeka. Ni furaha kusikia u mzima ni wapi uhuki ulako asali na maziwa....LOL

    JibuFuta
  2. Nashukuru u buheri wa Afya, nami pia afya najivunia.

    Kila mmoja anaweza kutafsiri mda unavyokwenda kulingana na mazingira aliyopo, nchi ya ahadi lazima siku zikimbie tu! tena siku inapokwisha unakasirika,asali na maziwa yake! wacha we!

    Nchi ya kusadikika, daaaa! Siku kama mwezi vile.

    JibuFuta
  3. muda bwana! ikiwa unasubiri jambo jema unaenda taratibu, ukiwa haujafaniskisha ama haujakamilisha jambo fulani unaenda kwa kasi mno.

    inaonyesha orodha ya mambo yako bando ndefu ndio maana muda unakuendea haraka.lakini hapana shaka kwa kuwa huko ulikokuwa kuna asali na maziwa basi nadhani mambo siyo mabaya.

    karibu tena.

    JibuFuta
  4. Mwaipopo umenipa tafsiri nzuri ya muda.

    Kissima, nchi ya kusadikika si halisi. Hii nilimo i halisi na kweli. Inamiminika asali. Mwezi wa asali ulikuwa...

    JibuFuta
  5. Mwaipopo - inaonekana kama vile ndiyo umemaliza kumsoma Albert Einstein.

    Bwaya - hiyo nchi inayobubujika maziwa na asali iko wapi tuhamie? Ni ile nchi ya ari mpya, kasi ....na...?

    JibuFuta
  6. Profesa Masangu, Mwaipopo ni mzee wa nukuzi.

    Nadhani unaweza kuwa umekosea. Hiyo kasi mpya na ari yake sikujua(ga) kuwa ni kula rasilimali za nchi kwa nguvu mpya.

    Nikuja jua, nchi kama nchi ina maziwa tele yanayonywewa na wenyewe hata kama yako kwako mlangoni. Muhimu ni kujinywesha mwenyewe kila unapopata nafasi. Ukisubiri unyweshwe sahau! Wnakimbia na ng'ombe kabisaaa.... Ha ha haaa!

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?