Padre Karugendo kakosea kipi hasa?
Mwandishi machachari na mwanafalsafa anayeheshimika kwa uchambuzi makini, Padre Privatus Karugendo (pichani) amevuliwa daraja la Upadre. Habari hizi si njema na ni za kusikitisha sana. Yeye mwenyewe amenukuliwa akisema kuwa hautambui uamuzi huo ambao anaamini umefanyika kwa misingi ya chuki za watawala wa kanisa hilo.
Nimeshtushwa na habari hizi kwa sababu kwanza nimekuwa mfuatiliaji wa makala zake kwa maika mingi tangu enzi za Rai ya zamani, na sasa Raia mwema pamoja na Tanzania Daima.
Na kwa majuma kadhaa Padre Karugendo amekuwa akiandika mtazamo wake kuhusu namna kanisa la Katoliki (hasa la Afrika) linavyoendeshwa. Yeye anasema watawala wa Kanisa wanatutawala badala ya kutuongoza.
Kama na wewe ni msomaji mzuri wa makala zake utakubaliana nami kuwa Padre Karugendo mara zote ameonyesha wazi kuwa Padre anayetaka mabadiliko. Mara zote amejitahidi kuwa yeye zaidi kuliko 'kuigiliza' misimamo asiyoiamini yeye. Si mara moja nimesoma akitofautiana na wakuu wake wa dini kwenye mambo ya msingi anayodhani yana faida kwa kanisa na jamii kwa ujumla wake. Japo simfahamu uso kwa uso, lakini namwona kama mtu asiye mnafiki, mkweli na muwazi. Ni tabia yake hiyo (huenda) ndiyo imemfanya ajijengee maadui katika kanisa lake.
Mimi nadhani tukio hili linatusaidia kujua namna kanisa Katoliki linavyoendeshwa. Yeye mwenyewe hajasita mara zote kueleza namna chuki na vinyongo vinavyotumika zaidi kuliko busara (hata za kawaida). Ni wakati wa dini zetu kutambua kuwa ukiritimba wa maarifa unafikia mwisho wake. Na watu kama Karugendo enzi hizi idadi yao ni kubwa. Haidhibitiki. Na ndio watu hao hao wanaouliza, hivi Padri Karugendo kakosea kipi hasa kiasi cha kuadhibiwa kiasi hiki? Je, ni kweli kwamba Kanisa Katoliki ni safi kiasi kwamba kamwe haliwezi kukosea?
tatizo anawaambia ukweli ukizingatia kukubali kwake matumizi ya kondomu kwa waumini ili kujikinga na ukimwi ilikuwa mwaka 1998. Lakini kingine nadhani kanisa linashindwa kwenda katika mazingira mapya. Mapadre wanaishi katika maizngira ya ajabu kabisa, pia maaskofu hujuiona wao ndiyo kila kitu. Jimbo la mbinga kuna ufisadi umefanyika hapa kijijini kwangu Lundu, jamaa wa ughaibuni walitoa fedha nyingi kuikarabati hospilati yetu ili iweze kutoa huduma kama ya huko mjini kwenu Muhimbili lakini salaaaale askofu katimba zote mwanawane, nakumbuka niliwahi kutofautiana na mtawa mmoja hivi sista ambaye alikuwa rafiki yangu sana. akataka nijitolee kama waumini wengine katika ujenzi, nikamwambia najua nitakuudhi lakini niambie zile fedha mmepeleka wapi? duu alinuna mtoto wa kike, nikasema poa tu na iwe hivyo kwani mimi siyo muumini wa makanisa ya GAZA wala ukingo wa magharibi huko mashariki ya kati.
JibuFutaKwa Karugendo nadhani kuna siasa katika kanisa tokana na falsafa zake. jamaa wanapenda kusujudiwa sana bila kuweka ukweli hadharani. unadhani kwanini wengine tulitolewa mkuku enzi hizo za purii seminari mkuu! mmm nimepotea njia nipo nje ya mada. KWAHERI
Mimi ni Mkatoliki lakini napenda kukiri kwamba sijatia mguu kanisani kwa muda mrefu sana japo nasali binafsi kila siku.Tatizo kubwa kabisa linalolikabili kanisa katoliki ni unafiki.Sote tunakumbuka harassment alizopewa Fr Nkwera na wafuasi wake.Kosa lake kuu ni kuwa na karama kama alokuwa nayo Bwana Yesu ya kuponya wagonjwa.
JibuFutaNi dhahiri kwamba mwelekeo wa Kanisa hili sio mzuri lisipobadilika.Hawataki kukosolewa.Huu ni ufisadi wa kiroho
Evarist,
JibuFutaKaribu TAG ambako karama ya kuombea wagonjwa ni kitu cha kawaida.
Mtanzania,
tmajaliwa@yahoo.com
Huyu Bwana huwa nasoma makala zake sana kwenye gazeti la Raia Mwema.
JibuFutaZamani alikuwa akiandikia Rai na ndipo nilipokuwa nikisoma makal zake.
Kwangu mimi namuona kama mtu asiye mnafiki na asiyeyumba kimsimamo, Baada ya kusoma Theolojia na kuifahamu vizuri alijitambua na kujua kwamba hayuko kwenye njia sahihi.
Huo ndio uzuri wa kujitambua.
Naamini hiyo haitamfanya aache kuandika makala zake kama kawaida kwa kuwa sasa yuko huru, hafungwi na kitu chochote
Bwaya, kwani ile mada ya akukosoaye na akusifiaye si ndio mambo yake haya? Kumkosoa mtu tena ukibaki ndani ya milki yake ni kuonesha kwamba uko tayari kushiriki mabadiliko yahitajiwayo. Nadhani Padre Kalugendo angeweza kuhama kanisa na kisha kuwasema apendavyo maana sio tu muelewa wa kile asemacho, lakini anaweza kukijengea hoja. Sasa aliamua kubaki maana aliamini kuwa angeweza kuwa sehemu ya suluhisho. Lakini kwa kuwa upande mwingine wanaliona tatizo toka pembe tofauti na kulitatua kwa namna tofauti, nadhani ndio maana wameamua iwe hivyo. Lakini turejee kwa maoni ya mmoja juu ya alichowahi kuandika Da Koero (na naomba anisamehe kwa kurejesha mjadala alioufunga) kuwa ni "ajali ya kijiografia" na watu wanataka kuiendeleza ikiwa ni pamoja na kuendeleza yale ambayo si sahihi kwa kuwa tu "tumeyakuta yakitendeka hivyo" Ndio maana tunashindwa kuwafikia wenye uhitaji kwa kuendelea kung'ang'ania kauli na mbinu zisizoendana nao, mfano kuwaambia kwa YESU NI MKATE WA UZIMA ilhali wao wanapata mkate wakati wa Krismans na ni kipande kimojakimoja kwa kuwa ni "chakula cha anasa". Unadhani hawatodhani kuwa Yesu si type yao? Kuwa ni wa watui wa mjini na wenye fedha? Kuwa ni wa msimu?
JibuFutaNaacha maana wala si mjuzi wa mijadala ya Imani.
Blessings
namfahamu karugendo na nilifanya naye kazi katika mradi mmmoja wa benki ya dunia mwaka 2003/4 mkoani kagera. ni mtu mwema na rafiki mzuri bila kujali tofauti za umri.
JibuFutamengi kayasema mpangala. kama lengo lao ni kujifanya wanamiliki funguo za mbingu na mungu na hivyo kila atakaye lazima awasujudiye, harafu karugendo anaanza kusema ukweli, maanake nini?
nampongeza fadha kwani ananafasi nzuri ya kuelimisha jamii badala ya kuwa mnafiki.
Maoni haya yameondolewa na mwandishi.
JibuFutaHuko kanisani kuna watu wanajiona Miungu watu.Nilipata bahati ya kukaa nao na kupiga nao stori mapadre wengi mzee wangu alikuwa mshikaji wao sana.Jimbo la Rulenge ndio nyumbani wengi nawafahamu.
JibuFutaPadre karugendo anawapiga mawe kisawa sawa.
Askofu Niwemugizi bado ana skendo kama mnakumbuka hii hapa chini
Date:
Wed, 15 Feb 2006 02:00:45 -0800 (PST)
From:
"Antiparth Martin"
Subject:
Mkunde!
To:
niwemugizi@iwayafrica.com
CC:
nunzio@cats-net.com, nyumba@cats-net.com, tec@cats-net.com
HTML Attachment [ Download File Save to Yahoo! Briefcase ]
Mtumishi wa Mungu, Askofu Severine Niwemugizi, Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.
Tumsifu Yesu Kristu.
Mtumishi wa Mungu,
Pole sana kwa kazi nyingi ya kuchunga kondoo. Bwana akubariki na kukuzidishia moyo mkuu. Ninakuandikia ujumbe huu kukumbusha jambo moja:
Unakumbuka siku chache kabla ya kuchaguliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge, ulizaa mtoto na Consolata Kyala, dada yake na Padri..... wa Jimbo Kuu la Dar-es-salaam. Padri huyo alikutunzia siri, na sisi tukanyamaza! Mtoto wako Mkunde, anaendelea kukua na sasa anasoma shule Maji ya Chai Arusha.
Ili Consolata Kyala, akae kimya, ulimjengea nyumba kule Maji ya Chai Arusha. Sasa hivi anaishi kwenye nyumba hiyo na mme wake Antiparth Martin. Hapo hapo anaendesha biashara ya Bar ijulikanayo kwa jina la Holiday Inn.
Tumesikia tetesi kwamba hivi karibuni utateuliewa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora. Tunafikiri ni jambo la muhimu na la lazima, viongozi wa Kanisa kufahamu kwamba wewe una mtoto. Ofisi ya Askofu Mkuu ni kubwa na yenye kudai maadili ya Kanisa Katoliki.
Viongozi wa kanisa wanaweza kupuuzia jambo hili. Nawe pia unaweza kupuuzia jambo hili. Kwa vile siku hizi sayansi imepiga hatua, tutasisitiza ipimwe DNA yako na ya mtoto Mkunde. Tunataka watanzania wajue ukweli huu na ulimwengu ujue ukweli huu.
Ni matumwaini yetu kwamba utaupokea ujumbe huu na kuwajibika ipasavyo.
Tunakutakia moyo mkuu.
Kwa niaba ya waumini wenye upendo na kanisa katoliki wa Maji Chai-Arusha.
Ni, wako katika Upendo wa Kristu.
Antiparth Martin
Ukipata muda pitia comments hapa http://tinyurl.com/create.php
could u add a google translator on your page? I may catch a little about another culture.. thanks
JibuFutaNaona kaka Egidio kaamua kumwaga mtama hadharani.
JibuFutaHaya we! mimi yangu macho.
Naomba mwenye email ya huyu Padri Karugendo anipatie ili niwasiliane nae, kuna jambo moja nataka kujifunza kupitia kwake.
Musinielewe vibaya jamani, nataka anipe darasa kidogo.
Mwenye email hiyo aiweke hapa kwa kaka Bwaya nitaipata au anitumie kwenye email yangu inayopatikana kwenye blog yangu.
Mlango mmoja ukifunga mingi hufunguka!
JibuFutaE-mail ni pkarugendo@yahoo.com kama sikosei. Simu: 0754 633122,
JibuFutaEdigio unamaanisha kwamba Askofu Severine Niwemugizi anayemsulubu Padre Karugendo kazaa kinyume na wito wake? Lakini sishangai kuna mafaza wengi wametotoa halafu eti wanajidai kuwa hawaoi! Unafiki wa kupindukia.
JibuFutaBado nina hamu sana. hivi mapadre wangapi wamezaa hapa ulimwenguni? Nimejaribu kudurusu sana kuhusu askofu Niwemugizi kuna nadhani kuna mengine zaidi, au akanushe yale anayoyasema Karugendo leo na akanushe kwa hoja siyo vitisho na kelele za kunukuu kitabi toka huko mashariki ya kati wanakochinjana halafu tuna hamu ya kwenda yerusalem ha ha ha ha nicheke mimi jamani someni makama za uatafiti katika blogu Jikomboe ya ndesanjo zinahusu UWONGO WA KANISA pengine kuja haoja tunaweza kujifunza jambo , halafu mjadala wa dini uliofungwa kwa dada Koero nina usongo nao yaaaaaaani hadi najsikia kulia, kushoto na pembeni
JibuFutaKoero na Mtingwa hii ishu nimeimind kichizi.Wengi wa "watakatifu" hawa ni wanafiki wa kutupwa.Hii ndio ilinifanya nikakataa kusoma seminari.
JibuFutaPadre Karugendo kaahidi kutoa kitabu kuhusu ishu hizi,nakisubiri kwa hamu kubwa.
@Simon dah!
Hizi dini za wazungu nishai sana.
time will tell bro, bora kuwa kimya kuliko kuongea bila ya busara na kushirikisha akili.
FutaBhart am working on your request. Thank you for visiting.
JibuFuta**********
Kwa yeyote anayejua namna ya kuweka google translator anisaidie.
Kuna wadau wengi wamechangia vizuri sana, na mimi naungana nao kabisa. Kuna kitu kimoja cha kufahamu kuwa, Catholic Church wana maadili yao and Utii kwa wakuu, nadhani huyu father alijua hili vizuri wakati akiwa kwenye malezi ya Upadri.... kwa kweli wote humu hutujui kosa gani kafanya, lakini nachoweza kusema kuwa hajafukuzwa Upadri, ameondolewa madaraka ya kusoma Misa and practices nyingine, lakini Upadri wake ni wa milele... wakati amepakwa mafuta basi yeye ni Padri forever kwa mfano wa Melicizedeki.... kwa wakatoliki mtajua nasema nini
JibuFutaSijui nimejipotezea wapi hata nimekosa mambo motomoto.
JibuFutaWashasema waungwana. Mi nawanukuu wanafalsafa wawili.
Bob Marley alisema, "truth is an offence"
Lucky Dube akaongeza, "when you stand for the truth, you always stand alone."
Ni hayo tu!
ig2wptry
JibuFutajdv20ab0
f54yewr4t536
drzl7j6u
v6f24zyz
kanisa ni utii, kama hili likikushinda mfumo unakutoa, kanisa katoliki lina nafasi kubwa sana ndani na siyo nje, utaona wote ambao wanatoka kama padri nakuwa wa kawaida mfumo umemtema, please tuacheni tunaoendana na mfumo tubakie huku, na ukiona panakushinda uondoke ila usianze kubwabwaja haito saidia, tambua UTII NDO MFUMO WA KANISA, haya mengine unatafuta laana tupu.
JibuFutakanisa katoliki lipo kwa misingi na siyo kwa fashion, ni lile lile juzi jana na jatya milele.