Kuna haja yoyote ya kutokuwa na dini?

Tumekuwa tukijaribu kujadili masuala ya dini. Hili ni jambo jema sana kwa ukombozi wa fikra zetu. Mwaka juzi tulifanya hivyo pale kwa Ndesanjo. Unaweza kubonyeza hapa kuusoma mjadala huo uliohusu dini na imani. Hivi karibuni, Koero aliufungua na kuufunga mjadala wa aina hiyo hiyo. Naomba sasa tujadiliane kwa kina suala hili kwa minajili ya kupeana changamoto pamoja na kuelimishana inapobidi.

Je, dini chimbuko lake ni nini? Je, dini inayo uhusiano wowote ule na Mungu?
Je, bila dini hatuwezi kumwona Mungu? Na je, kutokuwa na dini kunawezekana?

Angalizo: Mipaka ya tafsiri ya Mungu katika mjadala huu, inabaki kuwa maoni ya mchangiaji husika.

Maoni

  1. Nanukuu): "je dini inayo uhusiano wowote ule na mungu? Je bila dini hatuwezi kumwona mungu" Je kutokuwa na dini kunawezekana?" mwisho wa kunukuu

    Bwaya ubarikiwe umenileta ninapotaka elimu,ninapotaka kuelimishwa ni hay maswali.Yaani nashukuru nimekuwa wa kwanza ili wenzangu wakija wanisaidie mimi lbada mwana mpotevu. ASANTE nawasilisha hoja yako kakangu!

    JibuFuta
  2. Pengine inabidi kuanza kwa kuitafsiri Dini ambayo itatafsiriwa ki-Imani. Sasa Imani yenyewe ni "kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo. Ni bayana ya mambo yasiyoonekana" Hapo tayari ushaambiwa ama kuwekewa ka-condition ka nini waweza kuhoji maana kuwa na imani katika dini ni kuwa kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo na yasiyoonekana. Na hapo ndipo anapokuja Mungu ambaye watu wana hakika ya kumuona japo hakuna aliyewahi kufanya hivyo. Kwa hiyo kwa namna yoyote ile ya kuamini, Dini inayoaminika inakupa TARAJIO la kwenda upendako na huko unaamini utakutana na yule uaminiye kuwa ni Mungu wako. Kwa hiyo kuwa na dini tayari kwakuweka katika mazingira ya kuamnini ambacho hakuna aliyewahi kukiona na hilo latufanya tuamini kuwa TUKO KWENYE DINI NA NDIO NJIA PEKEE YA KUMUONA MUNGU. Ndio maana wahitaji Imani kuwa na dini na ni imani itakayokufanya uamini kuwa utamuona Mungu. Sijui naeleweka? Maana nami kwa kujikanganya sijambo.
    Naacha ili kina Luta-wa-Imani wanisaidie hapa.

    JibuFuta
  3. Inaaminika kuwa hapo zamani mababu zetu walikuwa na imani zao,wakipatwa janga fulani walikuwa wakiomba kwa namna yao na hali inakuwa vizuri.Baadae wazungu wakaleta dini zao ambazo hazikuwa na lengo zuri(kulingana na historia)kwani zilitumika ktk kuwalainisha mababu zetu na kuweza kututawala na kutukandamiza kirahisi.Kwa mtindo uleule ambao wazungu waliweza kubadili utaratibu wetu wa kubadilishana bidhaa,kwa mfano mtu akitakaka mahindi anaweza kubadilishana na maharagwe,hivyohivyo waliweza kuwashawishi wazee wetu kukana imani walizokuwanazo na kuwapandikiza IMANI nyingine na kuona imani walizokuwa nazo ni za kishenzi na ambazo hazifai.
    Kuna wakati nilikuwa naongea na wazee fulani,basi niliamua kuwagusia kuhusu dini.waliniambia kuna kitabu kimoja cha wakatoliki walichokuwa wanakitumia ktk kusali,kitabu hiki kilikuwa kinaitwa "misale ya waumini" kuna sala ambayo walikuwa wakiisali,na ktk hiyo sala kulikuwa na maneno yaliyokuwa yanasema "tuwaombee na washenzi wote wa bara la Afrika".Watu walishituka na kulalama kuhusu mistari hiyo na hatimaye kitabu kile kilipitiwa na kutoka edition nyingine maneno hayo yakiwa yameondolewa.(hakika ningepata kitabu hiki leo hii nikaiona mistari hii mi ningeachana na dini kabisa!kwani wanaotukanwa ndio waliokuwa wanatamka sala hii kika wasalipo.).Hii ingenipa uhakika wa 100% kuwa dini hizi tulibambikiwa.kwani kama nitaweza kuamini vitabu vinavyoitwa vitakatifu,vile vile nisingeshindwa kuamini kilichoandikwa kwenye ile misale,kuhusu maneno yaliyokuwa yanatudhalilisha sisi waafrika.
    Siku hizi tunaambiwa kama hutaatend kanisani na jumuiandogondogo za kikristu basi tukifa hatutazikwa na padre.(hapa unajifunza nini?).
    Mimi binafsi naamini hivi,kila kitu kinaishia hapahapa duniani,namaana kwamba,ninachotakiwa kufanya ni kuishi na watu vizuri,kusaidia wenzangu pale wanapohitaji na pale ninapoona nahitaji kutoa msaada,natakiwa kuwa chanzo cha amani,upendo na mkemeaji wa maovu.nk,kwani naamini haya naweza kuyafikia bila kuwa na imani ya dini yoyote.(itakuwa na maana gani kama kiongozi mkubwa wa dini analalamikiwa kwa kuwapa mimba wasichana?ujambazi,inamaana gani dini inayomwamini Mungu huyu mmja kukubali mapenzi ya jinsia moja?kila kukicha watu wanakuja na dini zao wenyewe na wanapata waumini wa kutosha tu! Lengo hasa ni nini!).mimi ninapoatend ibada sizingatii utaratibu wa ibada,bali yanayofundishwa na huwa najiuliza mafundisho haya yananisaidiaje ktk kukabiliana na changamoto za dunia hii?
    Mtizamo wangu ni kwamba haitakiwi mtu kusema kwamba dini yake ni ukristo,uislamu,nk au fulani ni thehebu gani,hiyo haitakiwi kwa sababu kama wote tuliumbwa na Mungu,kwa nini tuwe na tofauti za kidini?viongozi wa dini wamejikita ktk kusisitiza taratibu na kanuni za dini zao na siyo kumtayarisha muumini ktk kuweza kukabiliana na changamoto za dunia.Mifumo ya dini mbalimbali ipo ktk mazingira ya vitisho,yaani utendaji wa mambo mema unapandikizwa kwa waumini kwa njia za vitisho.Kwa mfano,kuambiwa kuna jehanamu,kwenye moto ambao unawaka si mchezo!na huku ni kwa wote watendao maovu!Hivi ingetokea taasisi au asasi itakayojikita ktk kufundisha mema,yani kila wiki mara moja na bila kuwa na vizuizi vyovyote wala kufuata taratibu zozote,yani ikifika hiyo siku unakwenda,unasikiliza mambo ya maadili mema,na wala sio lazima,unafundishwa mbinu mbalimbali za maendeleo yako na ya jamii nzima ambazo hazitamkwaza yeyote,ni watu wangapi wangekuwa wanahudhuria,?sio kwamba watu wangekuwa wanaisubiria hii siku kwa hamu kubwa?pengine wangeomba siku ziongezwe,,kwa haya unajifunza nini? Dini ni tija kweli? Ukiweza kuishi na watu vizuri,upendo,amani,kukabiliana na maovu,kusaidia,na mengine mengiambayo hayamkwazi yeyote,bila kuwa na dini,mwisho wake ni nini?da ! Najaribu kuhitimisha lkn nashindwa! ......,

    JibuFuta
  4. sir lucky,
    kwa taarifa yako sisi tunayo asasi ya kufanya unayoyaongelea na tunahiita elimu ya utambuzi. kwa sasa iko Dar na baadaye tutafungua matawi maeneo lukuki ya nchi hii.

    mtwiba,

    wewe unmenipa changamoto juu ya tunachofikiria na tunachokifanya. kwa nini usubilie kufa ndo umwone Mungu? wengine humwona mungu au nguvu kuu kia wakitaka. kuna wanaotoka kwenye miili yao na kwenda huku mahali pa juu na kurudi kwa njia kadhaa. ukiwauliza watakwambia huyu sie mungu bali kitu kingine ambacho ukuu wake, ubora wake, uzuri wake, upendo nk, havielezeki kwa maneno ya kawaida.

    waweza kumwona Mungu hata bila kulazimika kufa. lakini labda ndio maana sayansi inasema hamna mungu bali kuna nguvu. huwezi kumwona mungu kwa majaribio ya kisayansi bali kwa kufanya sayansi ya roho (sayansi of th soul)

    bwaya,

    maswali yako juu dini ni mazuri. dini ina definition kadhaa. kuna wanaosema dini ni njia ya kuunganisha na chanzo kikuu tulichotengana nacho. lakini wengine hudai dini ni ule woga au deni alilonalo mtu au ahisilo (labda baada ya kutishwa) juu ya uwepo wa nguvu fulani ambayo yaweza kufanyia vibaya any time.

    chanzo cha dini kinasemekana ni uwepo wa vitu viogopeshavyo vilivyokuwa nje ya uwezo wa mwandamu kama vile tetemeko la ardhi, radi, vimbunga magonjwa makali nk,na mwanadamu akaanza kushtakiwa na dhamira kwamba labda kuna vitu kamkosea mtu mwenye vitu hivi hatari na labda yambidi kujipendekeza ili asamehewe na ndiyo maana vitabu vitakatifu vinabaadhi ya maandiko yasemayo kuwa hizo ni laana kwa dhambi. kumbuka vitu kama sodoma/gomora, jangwa nk.

    lakini baada ya maarifa kukua na watu wakagundua kuwa hivi havina ishu wala sio adhabu, ndo maana watu wenye kufikiri vizuri na kujiamni wanaasi dini.

    nadhani kutokuwa na dini hakuwezekani sana kutokana na jamii zetu. mimi nilidhani sina dini lakini sasa nadhani dini zote ni zangu. sielewi sana hapo.

    hata hivyo kuna mifumo ndani ya jamii yetu ambayo tunalazimika kuifuata na ni yakidini na hivyo kujikuta tukiwa sehemu ya dini hizo


    DINI HAZINA UHUSIANO WOWOTE NA MUNGU BALI UOGA NA NJIA ZA KUTAWALA WATU KIMWILI, KIROHO NA KIAKILA.

    naishia hapa

    JibuFuta
  5. Ndio kwanza naandaa makala inayohusianan na hii mada.
    Naomba kesho asubuhi wadau munitembelee pale kibarazani kwangu.

    Nimeamua kujilipua maana mikwala ya wazee ilinifanya nisite kuendeleza ile mada ya DINI, lakini sasa uzalendo umenishinda mwenzenu sasa nimeamua kuweka mambo hadharani.

    Naomba mnilinde.

    JibuFuta
  6. naona wenzangu walionitangulia wamesema mengi, sina cha kuongeza.

    dada Koero nimekutembelea na nimeona jinsi ulivyojilipua.
    Hongera kwa kuonesha msimamo wako.

    JibuFuta
  7. Je, kuna ukweli wowote kwamba eti kuna watu hawana dini? Je, ni sawa kumwita mtu mpagani kwa sababu tu haamini dini unazozijua wewe?

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Kama sio utumwa ni nini hiki?