Kwenda mbele kunahitaji kugeuka nyuma?

Ningependa leo tuone ikiwa inatulazimu kuikumbuka jana ili kuweza kuendea kesho. Maana yapo mawazo kwamba ili tuweze kwenda mbele kwa ufanisi, ni vyema kugeuka nyuma kutathmini tulikotoka. Kwamba ni kwa kutumia historia twaweza kubashiri mwelekeo wetu.

Tunaambiwa historia hutuelimisha kuhusu mwenendo wetu na namna mwenendo huo ulivyoweza kutufikisha hapa tulipo. Ni kwa kutumia historia hiyo, inasemwa, twaweza kupata maarifa yatakayotusaidia kujikosoa ama kujizatiti kwa faida ya kesho na kuendelea.

Wenye mtazamo huu, wanaamini katika nguvu ya historia katika maisha ya mwanadamu. Kwamba maisha yajayo, hayana miujiza. Ni mwendelezo wa mambo yale yale kwa namna isiyotofautiana sana na haya tunayoyajua. Kwamba maisha yatarajiwayo ni kama mwendelezo wa tamthilia ndefu yenye vipande vingi. Vipande hivi vinategemeana. Tukio la kipande kimoja cha tamthlia, hutupa bashiri ya simulizi za vipande vinavyofuata –pamoja na kwamba badiliko dogo laweza kutokea.

Katika kujaribu kutanabaisha hiki kinachosemwa, hebu tuangalie mifano michache ya karibu: Umasikini wa familia nyingi, inasemekana unatokana na historia ya familia husika. Kwamba kwa kuwa masikini, haimaanishi kwamba mtu hakujibidiisha katika ukwamuzi wa makusudi kutoka katika ufukara huo. Zaweza kufanyika juhudi za hapa na pale, lakini ‘tamthilia’ ya umasikini ikaendelea japo kwa kasi inayobadilika.

Ndio maana wanaoamini hivi, wamekuwa wakiomboleza kwamba bara letu halitaweza kuendelea kwa sababu tu ya makovu ya historia.

Kwamba hata tabia zetu zimefinyangwa na historia zetu –mwizi hazaliwi mwizi isipokuwa kwa historia ya ukuaji iliyomfinyanga awe mwizi. Fisadi hageuki kuwa fisadi ukubwani – Je, unakubaliana na dhana hiyo? Au labda wewe ni kati ya wale wasioona umuhimu wa kuichunguza jana, hebu na tuone.

Wapo wanaosema kuwa historia haina nafasi kubwa ‘kihivyo’ katika kutuamulia tuendako. Kwa kuangalia nyuma, inasemwa, tunajikuta tukipoteza muda mwingi usioweza kuirekebisha kesho yetu. Kuangalia nyuma hakutupi mabadiliko tuyatatarajiayo. Sababu ni kwamba kuangalia nyuma huweza kutafsirika kama juhudi za kujaribu kujiondolea ‘dhana ya uwajibikaji’. Kuyawajibikia maisha yetu sisi wenyewe. Kwamba kwa kugeuka sana mtu hujikuta akizielekeza lawama zote kwa watu na hali nyinginezo ambazo kimsingi hazipaswi kulaumiwa ‘kihivyo’.

Jana huweza kutuumiza kiasi cha kutukosesha matumaini. Jana hutukumbusha makovu tuliyopaswa kuyasahau ili tuweze kuenda mbele. Jana huweza kutugombanisha na watu wengine. Jana hutuongezea uwezekano wa kuwa na msongo wa mawazo. Jana huweza kutupa ‘kibri’ kisicho cha lazima. Jana huweza kutuharibia kesho. Wenye mawazo haya wanaiona jana kama isiyo na tija zaidi ya kutupa mwendelezo ambao unaonekana kutuvuruga zaidi ya kutusaidia.

Wenye mawazo haya wanaamini kwamba katika kwenda mbele, hatulazimiki kutizama tulikotoka. Wao wanasema (ashakumu si matusi) mavi ya jana hayanuki. Kuyakagua mavi yaliyokauka, ni kutafuta harufu ambayo ni wazi haipo. Wengine wanasema yaliyopita si ndwele. Ganda la muwa la jana sijui halifanyaje...alimuradi zipo semi nyingi zinazojaribu kutusahaulisha yaliyopita.

Wewe unasemaje kati ya haya mawili: Tugeuke nyuma tuione jana ilikuwaje ili tubashiri kesho itafananaje, au tuachane na jana, tufikirie zaidi kesho? Je, ni kweli kwamba kwa kuangalia nyuma sana tunaweza kusonga mbele kwa uhakika na kwa kasi? Je, inawezekana ukakimbilia mbele kwa kupapasa wakati unaweza kuwasha kijinga kikakusaidia kupunguza giza?

Uwe na siku njema unapoamua kimoja: Kuithamini ama kuipuuza jana katika mipaka ya umuhimu wake kwenye ujenzi wa kesho yako.

Maoni

  1. asante Bwaya kwa kunitembelea na maoni mazuri. Tushikamane

    JibuFuta
  2. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  3. Nashukuru Yasinta, nitashikamana. Tafadhali karibu tena na tena.

    JibuFuta
  4. [url=http://firgonbares.net/][img]http://firgonbares.net/img-add/euro2.jpg[/img][/url]
    [b]purchased software, [url=http://firgonbares.net/]vista oem software[/url]
    [url=http://firgonbares.net/][/url] buy cheap software discount coupon coreldraw jobs in scottsdale az
    windows vista oem software [url=http://firgonbares.net/]Enterprise 2007 Retail Price[/url] soft sales oem software
    [url=http://firgonbares.net/]linux software downloads[/url] buy a software to
    [url=http://firgonbares.net/]discount adobe software for[/url] adobe creative suite 4 production premium student
    coreldraw maps [url=http://firgonbares.net/]ecommerce store software[/b]

    JibuFuta
  5. [url=http://hopresovees.net/][img]http://bariossetos.net/img-add/euro2.jpg[/img][/url]
    [b]of photoshop to buy, [url=http://bariossetos.net/]adobe photoshop cs3 for mac student version[/url]
    [url=http://vonmertoes.net/][/url] purchase adobe software cheap pc software
    adobe software suppliers [url=http://vonmertoes.net/]store creation software[/url] coreldraw 12 trial
    [url=http://vonmertoes.net/]microsoft publishing software[/url] office email software
    [url=http://bariossetos.net/]college software discounts[/url] software for academic research
    adobe photoshop cs4 upgrade [url=http://hopresovees.net/]buy discounted software[/b]

    JibuFuta
  6. [url=http://hopresovees.net/][img]http://bariossetos.net/img-add/euro2.jpg[/img][/url]
    [b]discount software dreamweaver, [url=http://bariossetos.net/]adobe photoshop cs for mac[/url]
    [url=http://bariossetos.net/][/url] adobe acrobat pro 9 free training software market discount
    filemaker pro 6 download [url=http://vonmertoes.net/]buy microsoft windows software[/url] buy software licenses
    [url=http://bariossetos.net/]pirated software shop[/url] free mac sketch plugin for photoshop
    [url=http://bariossetos.net/]get oem software[/url] office 2007 enterprise will not install
    price check software [url=http://hopresovees.net/]sell used computer software[/b]

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia

Uislamu ulianza lini?