Hasira ina maana gani kwetu?

Hasira si kitu kigeni. Kama hujawahi kuwa na hasira maishani mwako, basi bila shaka mwenzetu unacho kitu fulani ambacho binadamu wenzako wote hawanacho (kasoro?). Hasira ni jambo la kawaida kututokea sisi kama binadamu. Waweza kusababishiwa hasira na watu wengine, vitu ama wewe mwenyewe ukajikasirisha.

Bila kujali chanzo chake, ukichunguza vyema utaona ya kwamba karibu mazingira yote yaliwahi kukusababishia hasira yanafanana –fanana kimsingi. Yaani kila jambo fulani akilini mwako lilipoguswa, uliwaka moto kwa hasira. Ulifura.

Sasa ningependa tujiulize: Hasira hasa ni nini na ina maana gani kwetu? Inahusianaje na namna tunavyojifikiria? Pengine sijielezi ninavyotaka. Hebu tujaribu hivi: Je, kuna tofauti gani ya kujifikiria wewe mwenyewe kama wewe kabla na wakati wa hasira? Je, kuna tofauti gani ya kuwafikiria wengine (wanaotusababishia hasira) kabla na wakati wa hasira? Je, kwa nini kuna watu hasira huyeyuka kirahisi ilhali wengine hasira ikiacha makovu ya kudumu? Hasira ni kipimo cha kujielewa.

Maoni

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?