Nini maana ya muda?

Kuna rafiki yangu mmoja kanitumia ujumbe mrefu wa barua pepe akinipa vidonge vyangu kwa kuitelekeza blogu hii kwa muda mrefu. Yeye hana blogu, ila ni mfuatiliaji wa wenye blogu akifatilia yupi yuko wapi ana ansema nini.

Basi, kupata ujumbe ule kunanikumbusha nadharia ya muda (kosmolojia): Muda ni nini hasa? Unaposema muda unaenda, unamaanisha nini hasa? Ili kujibu vidonge vya huyo rafiki yangu huyo hebu tuone muda maana yake nini.

Muda unatokana na mabadiliko. Huwezi kuhesabu muda kama hauna mabadiliko. Dunia inahesabu masaa kwa sababu kuna mabadiliko. Inakuwa mchana inakuwa usiku. Inakuwa kiangazi inakuwa masika. Mabadiliko. Yasingekuwapo mabadiliko hayo pasingekuwapo na kitu kinachoitwa muda.

Aidha, muda unatofautiana kati ya desturi na desturi, mtu na mtu, kazi na kazi na kadhalika. Kwa mfano, kwa mtu alikufa kwake muda ni sifuri kwa sababu mwili wake hauna mabadiko ya aina yoyote kwa vigezo vya kiumbe hai. Na pia katika jamii ambamo mabadiliko ni ya haraka, kwao muda unakuwa mdogo. Lakini kwa jamii zile ambapo madadiliko ni ya kinyonga, pole pole, kwao muda hauhesabiwi hata kama saa zinazoupiama ni zilezile!

Kwa hiyo utaona kuwa ni makosa sana yalifanyika kwa hawa jamaa waliotutengenezea saa za kutuhesabia muda kimakenika kwa spidi ile ile, ilihali tunatofautiana sana katika namna ya kuhesabu muda.

Ni kwa kusema hivyo ndipo tunapofika mahala pa kusema kuwa blogu hii haikupotea kwa vigezo vya mwenyenayo. Muda wake ulikuwa sifuri, kwa sababu hapakuwa na mabadiliko yoyote humu ndani. Hivyo muda wa blugu hii uhesabiwe kwa vigezo tofauti na vile tulivyovizoea vya kalenda ya Gregori.

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?