Jua furaha yako iko wapi, itafute

Tofauti ya binadamu na viumbe wenzake wote, iko katika ufahamu. Binadamu anaweza kutumia ubongo wake vizuri zaidi na hivyo kujitofautisha na "wanyama" wenzake wasiojua wanakotoka na wanakoelekea.

Anao uwezo wa kujua anataka nini na afanyaje kukibapata. Wenzake wote, pamoja na Sokwe mwenye Di Eni Ei zinazokaribia kufanana na zake, na hata wengine tukadhani wanachangia babu wa babu, hawana kingine wanachokitafuta zaidi ya uzazi. Wao, kuzaa kunamaana ya kufikia kiwango cha juu cha mafanikio katika kipindi cha maisha yao. Wakishazaa basi, hata wakifa, kwao kifo hicho hakitahesabika kuwa cha hasara.

Nini kusudi la binadamu kuzaliwa? Je, binadamu huyu anatafuta kitu gani katika kipindi cha maisha yake ambacho akikipata hicho basi anaridhika? Anataka nini ambacho akiisha kukipata basi, kwake hayo ndiyo mafanikio katika kilele chake? Je, ni kuzaa kama ilivyo kwa ndugu zetu wanyama? Je, ni kuwa na mke mrembo kuliko wote (kama kweli yupo)? Ni kuwa bilionea nambari moja Bongo yote? Ama ni kuzawadiwa usomi kwa wingi wa shahada? Kwanza inasemekana kadiri binadamu anavyosoma ndivyo anavyokuwa mjinga, kwa sababu anazidi "kusoma mambo machache" mpaka unakuta anageuka mjinga anayejua kitu kimoja!

Kusudi ni nini? Ama ni furaha? kwamba binadamu anapigana vikumbo kutafuta furaha (utoshelevu) wa moyo wake? Kwamba awe Raisi afurahi. Awe na mke mzuri afurahi. Ajulikane. Afurahi. Je, ndivyo ilivyo?

Ukamilifu wa maisha ni kitu gani? Umezaliwa iliiweje? Ule, uzae, ufe? Wote tunajua kamwe hiyo haiwezi kuwa kweli.

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?