Hitilafu ndogo
Kutokana na sababu ambazo ni za wazi, ili kublogu huwa natumia tarakilishi-paja kuandikia na kisha kuja mtandaoni kupesti maandiko yangu. Kufanya hivyo hunipunguzia gharama za muda wa kukaa mtandaoni ambao kwa nchi tajiri kama yetu, unagharimu sana.
Kwa bahati mbaya sana, tarakilishi hiyo imepata UKIMWI siku kadhaa zilizopita! Kuna kirusi kaivamia na ananizuia kufanya chochote. Jitihada za kumtafuta daktari wake zinaendelea.
Kwa bahati mbaya sana, tarakilishi hiyo imepata UKIMWI siku kadhaa zilizopita! Kuna kirusi kaivamia na ananizuia kufanya chochote. Jitihada za kumtafuta daktari wake zinaendelea.
Hawa wadudu wamekuwa hatari kweli,namimi tarakishi yangu imevamiwa,hope leo nitamtoa nina nafasi
JibuFutaPole sana kwa kirusi hiki. Tutaendelea kukusoma kama 'utapona'
JibuFutapole kaka mimi mpia nina jamaa anaitwa trajon horse na adware wananila mwezi sasa nimejaribu program tatu tofauti naona zinamshindwa ninakomaa nao hivyo hivyo nikijaribu kuhamisha mafail muhimu ili nishushe injini. jamaa wamekuwa hatari sana natumia viprogram vya kutuliza maumivu kwa sasa ant vir na avast.
JibuFuta