Ni kujielewa si kujitambua tena

Haya. Nilipotea. Kwa vigezo vyenu nakubali.

Sasa nimerudi. Kurudi kwangu kumekuwa kwa jina jipya. Blogu hii tuliita Jitambue lakini baada ya kupitia pitia kumbukumbu, tukafahamu kuwa ipo blogu ambayo inaitwa kwa jina hilo ingawa imekuwa mapumzikoni tangu elfu mbili na tano. Hatujui itarejea lini ila tunaamini itarejea.

Sasa ili kumrudisha ukumbuni mwenye blogu hiyo, tumeona ni vyema sisi wa hapa tujitambulishe kwa jina jingine ambalo maana yake inabaki kuwa ni ile ile.

Mengi ya maudhui yetu yatakuwa yamejikita katika kujielewa. Tutajaribu kuzungumza kwa muhtasari sana habari ya sisi kama binadamu kujielewa wenyewe kazi ambayo ni muhimu sana.

Watu wengi wamekuwa na kazi ya kuelewa mambo mengine, wakati wao wenyewe hawajijui. Tunadhani kwamba kuyaelewa mambo mengi bila kujielewa mwenyewe ni hasara na kujilisha upepo.

Unapotembelea blogu hii, usitazamie kusoma siasa. Kwa sababu siasa haikusaidii kujielewa. Tazamia kusoma maswali yanayoweza kukufanya uongeze tafakari kukuhusu wewe mwenyewe na jirani yako.

Karibu kujielewa mpendwa mwana blogu.

Maoni

  1. hongera kwa kurudi tena kijiweni. ila ninini? kilikusibu kaka ukaamua kukitelekeza kijiwe?
    tupo pamoja. karibu tena

    JibuFuta
  2. Kaka, nilikuwa msituni kuchemsha bongo ili nijielewe.

    Tutakuwa pamoja sasa.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia