Mbinu za Kutafuta Ajira Mtandaoni
Changamoto kubwa inayoweza kukukabili unapotafuta kazi, ni taarifa zitakazokusaidia kujua uelekeze wapi maombi ya kazi. Zamani, ili kupata taarifa za kazi, watu walitegemea radio, magazeti, televisheni na taarifa za marafiki wanaofahamiana nao. Mambo yanazidi kubadilika kwa kasi. Sasa hivi, kwa mfano, matumizi ya mtandao yamerahisisha namna tunavyoweza kupata taarifa hizi. Hata hivyo, pamoja na uwepo wa mtandao, bado kuna changamoto ya wapi hasa waweza kupata taarifa sahihi. Mbinu zifuatazo ni matokeo ya uchambuzi wa tafiti mbalimbali na zinaweza kukupunguzia changamoto ya kupoteza muda na nguvu nyingi kutafuta kazi mtandaoni.