Wafilipino Walivyomficha Papa Francis Hali Mbaya ya Haki za Kijamii Nchini Humo
Makundi ya haki za kijamii yalizuiwa na Polisi kukaribia msafara wa Papa Francis. Picha kutoka kwenye ukurasa wa facebook wa Kathy Yamzon
Si kila mmoja nchini Ufilipino aliweza kumwona Papa Francis alipoanza ziara yake ya ki-Papa nchini Ufilipino. Kikundi cha wanaharakati kilichokuwa na mabango yanayopinga ukosefu wa haki za kijamii kinasema polisi waliwazuia kufanya maandamano mbele ya msafara wa Papa. Kadhalika, kuna taarifa kwamba maafisa wa polisi waliwakamata na kuwaweka chini ya ulinzi baadhi ya watoto wa mtaani wakati wa ziara hiyo ya Papa.
Papa Francis alizuru Ufilipino kuanzia Januari 15 mpaka 19. Ziara hiyo, iliyokuwa na kauli mbiu ya "rehema na huruma," ilimpeleka Papa Francis kwenye taifa hilo linaloongoza kwa idadi kubwa ya wa-Katoliki nchini Asia.
Baadhi ya wanaharakati 2,000 walikusanyika jijini Manila kumsalimia Papa kwa mabango yaliyokuwa na ujumbe wa masuala kadhaa yanayowaathiri masikini wa taifa hilo, kama vile njaa, ukosefu wa ardhi, na uvunjifu wa haki. Polisi hata hivyo waliwazuia kuandamana karibu na msafara wa Papa.
Kiongozi wa wanaharakati hao Nato Reyes aliikosoa vikali serikali kwa kuyazuia makundi mbalimbali yaliyotaka kujaribu kumweleza Papa kuhusiana na kile walichokiita "hali halisi" ya mambo nchini Ufilipino. :
Kuanzia Siku ya 1, kumekuwa na jitihada za makusudi kujaribu kudhibiti kile ambacho Papa anatakiwa kukiona na kukisikia. Hilo liko wazi kwa sababu Papa hakuja kuona "ukweli, mema na mazuri" pekee. Papa amekuja hapa kusikia matatizo ya watu masikini na wanaotengwa.
Polisi wakiwazuia kikundi cha wanaharakati kuandamana karibu na msafara wa Papa. Picha kutoka kwenye mtandao wa Facebook wa Southern Tagalog Exposure.
Onesho la wasanii wa Mudwalk, walioonesha waathirika wa dhoruba ya Haiyan, lilizuiwa na polisi kukabidhi barua kwa uongozi wa kanisa. Picha kutoka ukursa wa Facebook wa kikundi hicho.
Polisi wakirarua bendera ya mwanaharakati. Polisi wamesema 'watu waliokuwa na shughuli ya kushangilia' ndio tu waliruhusiwa. Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa Southern Tagalog Exposure.
Baadhi ya wafungwa wa kisiasa waliweza kuning'iniza mabango nje ya vyumba vyao vya magereza. Walimwomba Papa kutazama hali ya haki za binadamu inayozidi kuwa mbaya nchini humo. Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa Kathy Yamzon.
Zaidi ya kuwaingilia waandamanaji, serikali pia inadaiwa 'kuwakamata" na "kuwaweka kizuizini" watoto wa mtaani siku chache baada ya Papa kuwasili. Jarida maarufu la kila siku la Manila Standard Today, lilihoji busara ya sera hii, likisema inamwelekeo unaokaribiana na sera ya Potemkin-Village.
Serikali imekanusha kuwakamata watoto wa mtaani wakati wa ziara ya Papa.
Wakati huo huo, maafisa wa serikali walijenga kwa haraka kizuizi cha kijani pembeni mwa barabara ambazo msafara wa Papa Francis ungepita, kwa lengo la kumzuia Papa na watu wengine waliokuwa kwenye msafara huo kuo mitaa wanayoishi maskini pembezoni mwa kizuizi.
Kizuizi kingine kilichomtenga Papa na watu kilikuwa usalama mkali. Wengi walisema kumwagwa kwa polisi na kuwekwa kwa vizuizi vya chuma jijini humo kulizidi kiwango, na kuwafanya watu washindwe kumwona mgeni huyo maalum wa taifa. Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa intaneti wa ki-Filipino walifananisha ziara ya hivi majuzi ya Papa nchini Sri Lanka, ambapo alionekana akigusa na kubariki mikono ya waumini waaminifu waliokuwa wamesimama barabarani.
Polisi walizidi kiwango? Aquino ni rais wa Ufilipino. Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa kituo cha kazi cha Kilusang Mayo Uno (Vuguvugu la Mei Mosi).[/caption]
Papa Francis! Quirino Ave cor Taft Ave akiwa njiani kwenda kwenye uwanja wa MOA Arena majira ya saa 11 jioni @gmanews pic.twitter.com/LKXJYY3NBA
— Bam Alegre (@BamAlegre) January 16, 2015
Papa Francis! Quirino Ave cor Taft Ave akiwa njiani kwenda kwenye uwanja wa MOA Arena majira ya saa 11 jioni
Pope Francis waving as he passed by Quirino Ave cor. Taft Ave at 1:14pm earlier today. #PopeFrancisPH | @jcansis pic.twitter.com/YPvOVGYqeK
— 9News Philippines (@9newsph) January 16, 2015
Serikali inasema usalama wa hali ya juu ulikuwa ni wa lazima kwa ajili ya tahadhari. Hata hivyo, wengi wanaendelea kuhoji kwa nini serikali haikuheshimu matakwa ya waumini na kuwaruhusu kumkaribia Papa:
Papa Francis akipunga mono alipokuwa akipita akiwa kwenye gari la Quirino. Mkesha ulifanyika saa 7:14 leo.
Sure it's for security purposes but I think the Pope would really like to reach out to the people hidden by hundreds of security personnel.
— Kat De Castro⭐♎ (@KatDeCastro) January 16, 2015
Nonoy Oplas alikosoa vikali "mfumo wa kiusalama wa kijeshi" unaotumiwa na serikali:
Ni kweli kwamba hali hiyo ilikuwa ya lazima kwa usalama lakini ninadhani Papa angependa kuwafikia watu waliokuwa wamefichwa na mamia ya wana usalama.
Kumwona barabarani ni jambo la fahari zaidi ambalo watu wangejisikia kuweza kumwona Papa. Na mfumo unakera wa usalama ulijaribu kufanya iwe vigumu kwa watu kumwona Papa kwa karibu kadri inavyowezekana.Wengi wanatarajia kwamba Serikali itafikiria upya utaratibu wake wa kiusalama katika siku zilizobaki, ili kuwaruhusu watu zaidi kumwona Papa Francis, kabla hajaondoka Januari 19.
Makala haya yalichapishwa awali na Global Voices.
I think it is fair conducted by citizens
JibuFuta