Mambo ya Kufanya Unapotafuta Kazi
INGAWA inafahamika kuwa wapo wahitimu, tena wengi tu, ambao hufanya maamuzi ya kutumia ujuzi na maarifa waliyoyapata darasani kujiajiri wenyewe, kwa maana ya kubadilisha maarifa na ujuzi walionao kuwa bidhaa pasipo kumtegemea mtu aitwaye mwajiri, bado tunajua kuwa wahitimu wengi, kadhalika, huchagua kutafuta ajira. Kwao, huona ni rahisi kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao kwa njia hiyo. Makala haya yanasaili mambo yanayoweza kumsaidia mhitimu anayetafuta ajira kupata taarifa zinazohusiana na namna bora ya kuwasiliana na mwajiri kwa matumaini ya kupata ajira anayoitegemea.