Kuvunjika kwa koleo...



Hivi kama watu mnapendwa na wananchi, mabango haya yote ya kazi gani? Kama kweli ninyi ni chaguo la wananchi, inakuwaje mnatumia mapesa mengi hivi kuwashawishi wananchi hao hao?

(picha kutoka Kijiji cha Mjengwa)

Maoni

  1. i dont think km ugonjwa ndio sela.huyo mtu kaishiwa sela ndio maana kasema hivyo isijekuwa ukienda kumpima yeye ataoneka mgonjwa kuliko huyo anayemsema.

    JibuFuta
  2. Mimi natafakali sana, hivi kama mimi nimefanya kazi ipasavyo kwa kutimiza ahadi zangu, kuna haja gani la kutumia nguvu na ahadi mpya nyingi huku mabango makubwa yakiuuza sura!!! Wewe tulia tumia nguvu kidogo kwa kuwa umelitumikia taifa kwa miaka mitano kwa mafanikio.

    JibuFuta
  3. Mpondela, hawawezi kutulia wanajua wakitulia imekula kwao.

    JibuFuta
  4. Padre Karugendo ameandika haya (kwenye Tanzania Daima) kumhusu huyo jamaa kwenye hilo bango


    Naandika kutoa ushauri na hasa maoni yangu ambayo ni ya nia njema kwa taifa letu la Tanzania.

    Hii ni aina ya barua ya wazi kwa wale wanaotamani kuendelea kutawala wakati miaka ya kustaafu inakaribia. Labda kuna haja ya kuongeza miaka hii ya kustaafu. Miaka sitini ya sasa watu wanakuwa bado wana nguvu na kutaka kuendelea kutumika au kula “utamu” wa uongozi.


    Hakuna haja ya kusubiri kuzomewa na kugomewa hadi kufikia hatua ya kukulazimisha kujitoa. Hakuna haja ya kusubiri kufanyiwa maandamano na vikao vya kukujadili kama unafaa au hapana. Ni kweli kwamba Watanzania ni wasahaulifu; wengine hawakumbuki yaliyotendeka jana.

    Lakini si kweli kwamba wote ni wasahaulifu; wachache hao wanatosha kuchochea moto kiasi cha kukufanya kujuta ni kwa nini hukujikalia kimya na kufanya mambo yako.

    Vidonda bado ni vibichi, hata watoto wadogo bado wanaimba Richmond na wengine kwenda mbali na kuibatiza Rich Monduli. Atakaye kuambia hili limesahaulika, atakuwa hakupendi.

    Kwa vile umekubalika kwa mzee wa kimila, tosheka! Washauri na kuwaelekeza ndugu zako huko na kuingia kwenye mtandao wa wazee mashuhuri ndani ya taifa letu.

    Nakubali kabisa kwamba tulifurahi pamoja, tukadhalilishwa, tukaonewa na kusikitika pamoja, sasa tusonge mbele: Ushindi ni wetu! Sina matatizo na hili. Na kama ushindi wenyewe unalenga kumhudumia Mtanzania na kumsaidia kupiga hatua kuelekea maendeleo;

    Kama hautakuwa ushindi wa kujilipiza kisasi, kuchota rasilimali kiasi cha kutosha na kuwatajirisha marafiki, ndugu na jamaa. Labda mimi ningesema hivi: Tulifurahi pamoja, tukadhalilishwa, tukaonewa na kusikitika pamoja, sasa tupumzike!

    Tusifikiri kwamba bila sisi hakuna kitakachofanyika. Tutoke kwenye ndoto na malengo haya ya kutaka kufika tulikolenga miaka mingi bila ya mafanikio. Sote tuna malengo, lakini si yote yanafanikiwa.

    Hata hivyo tunamshukuru Mungu, na kutosheka pale tulipo! Hata wale waliostaafu na kupumzika wana mchango mkubwa katika kuliendesha taifa letu la Tanzania. Si lazima mtu uwe rais, waziri, waziri mkuu au spika wa Bunge, ndio utoe mchango wa maana.

    Binafsi ningeifanya kauli mbiu hii mpya iwe hivi:Tulifurahi pamoja, tulisikitika pamoja na sasa tusonge mbele hadi ushindi, na kuishi ya maisha ya hekima, busara na ushauri zaidi ya kuwa kauli mbiu ya siasa za kiwendawazimu.

    Siasa zisizo soma alama za nyakati na kukubali mabadiliko yaliyosukwa na Vision, historia na bidii ya kufanya mabadiliko hayo; siasa za ili liende, heshima na utukufu na kuendelea kuutukuza umasikini kana kwamba sisi tuliumbwa tumelaaniwa.

    Kaulimbiu mpya inahitaji watu wapya, mazingira mapya na ‘vision' mpya inayochimbuka ndani ya historia ya Taifa letu; historia inayokusuta pale unapotaka kujichanganya kuendeleza ndoto zako zisizo tekelezeka.

    Lakini pia ni muhimu kwamba wale unaotaka au kutamani kuwaongoza wakukubali na kukupenda vinginevyo, itakutesa wewe na kuwatesa wale unaotamani kuwaongoza.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?