Ethics na somo la maisha yetu

Nimefuatilia kidogo mfululizo wa tamthilia ya 24. Kuna mhusika mkuu anayeitwa Jack Bauwer. Huyu kwake kilicho muhimu ni matokeo ya kile anachokifuatilia. Na katika kuthamini matokeo, huyu bwana hujikuta matatani sana. Kwake mbinu si jambo la maana sana hata ziwe haramu lakini mwisho (matokeo) ndicho kilicho muhimu. Na kweli huzitumia mno hadi kumfikisha kwenye matokeo aliyoyataka ambayo ndiyo yanayokuwa jawabu kwa wote. Kwamba haramu imekuwa halali kwa sababu tu mwisho umekuwa mtamu.

Jack ananifanya nitafakari maisha yetu vile yanavyoelekea kubadilika ghafla. Kwamba kwa nini tunachoanza kukijali kama taifa ni mwisho (matokeo) bila kujali mbinu? Kwa nini tumeanza kuwa watu wa kutizama matokeo kwa mbinu zozote? Why?

Je, ninapopata mafanikio makubwa kimaisha kwa gharama ya uhalifu wa kimaadili kwa jamii, nami tuseme nitakuwa nimefanikiwa?

Vipi ninaposhinda uchaguzi kwa matumizi wa zile zinazoitwa siku hizi "siasa za maji taka" yaani kuwachafua washindani wangu ili nifanikiwe dhamira yangu, je mwisho wa siku ninaweza kudai nimeshinda uchanguzi huo kihalali? Na je, hao (wengi) wanaokubaliana na mbinu za namna hii watakuwa sahihi?

Ninachojiuliza: Je, ni mwisho wa jambo huhalalisha mbinu zilizotumika ama ni mbinu zinazitumika ndizo huhalalisha mwisho wa jambo husika?

Ubebari unatufunza mengi. Moja ni umuhimu wa mwisho wa jambo (mapesa na ushindi) bila kujali namna tunavyofikia mwisho huo. Hili ni janga jipya la taifa letu. The end justifies the means.

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia