Wingi wa siku ndio lengo lako?

Wengi wetu hufanya jitihada kubwa na kutumia muda mwingi kuhakikisha kuwa tunaishi maisha marefu. Tunaepuka kula baadhi ya vyakula na hata kufanya mazoezi si kuwa na furaha bali kuepa magonjwa fulani fulani. Lengo hasa likiwa katika kuzidisha wingi wa siku za kuishi duniani na wala si ubora wa siku hizo.


Tungefanya vyema kama tungelijishughulisha kutafuta ubora wa siku chache tulizonazo ili tuweze kuziishi kwa furaha badala ya kuhangaika na kuzirefusha siku zetu ziende mbele pamoja na matatizo yake.

Kilichobora si kurefusha siku ambazo zaweza kurefusha matatizo kwa upande mwingine...!

Maoni

  1. Ni kweli kabisa swala sio muda bali ubora wa maisha au kukamilisha kile kilicholeta hapa duniani. Ukiweza kujiuliza maswali kuhusu maisha utangundua hata huo muda mrefu au mfupi ni kipimo cha kibinadamu hakina maana yoyote yenye mashiko.

    JibuFuta
  2. Pembeni kidogo ya swala hilihili!

    Nilishawahi kuongea na jamaa kuhusu mpaka swala la kwanini ni wachache wanaojiua kirahisi kivyao au kidini a.k.a kujialqaida kistaili za kuanza, katika kufupisha maisha.

    Jamaa akanijibu, unauhakika na uendako ukifa?Kesho ikiwa nzuri sana je kuliko leo?

    Akadai hilo ndilo sababu Binladen hajiui kujipunguzia maisha na amfuataye anaweza kujiua aende mbinguni.

    Nitumaini langu sijatoka nje sana na hoja!

    JibuFuta
  3. ubora wa siku chache ukoje, uko wapi na unafananje? SIKU ZISIZOBORA ZIKOJE?
    unamaanisha tule tu na tusijali ieti kwa sababu hatujali kufa? kama ni hivyo kale sumu tuone.

    hatupaswi kula vykjula fulani kwa sababi kimaumbile sio vyetu au hatuvihitaji. siku zote ni bora na msingi wa ubora wake upo kwa sababu ni bora na ilibidi ziwe bora bila kujali nini.

    eti ni jambo gani bora duniani? si sisi ndio ubora wenyewe? maisha baada ya kifo hayatuhusu sana kwani yanategemea yale tuliyonayo sasa (kablaya kifo). kwani kabla hatujazaliwa tuliwahi kuambiwa kuwa tatuazaliwa na kuishi maisha fulani? sisi si ni matokeo tu ya wale wenye uwezo wa kufanya ngono tukawa mimba na sasa ni midume mizima kama bwaya na Kitururu? au unadhani ngono ile ilikuwa takatifu ndo maana ikakuzaa wewe!

    no naishia hapa

    JibuFuta
  4. Kwako Kamala,

    Sikutaka kumaanisha kwamba kazi ya kufupisha siku iwe ndiyo mbadala wa kurefusha. Nilichokuwa nataka kukisema ni je, lengo la mwanadamu ni kutafuta ridhiko na furaha kwenye siku anazoziishi (hata kama ni chache)ama ni kujibidiisha katika kuzirefusha (hata kama hamletei furaha kamilifu na ridhiko, ambalo ndilo hasa kiini cha mahangaiko yote ya maisha?)

    Kwa nini watu wanalazimika (kujitesa) kwa kuwa na miiko ya kula baadhi ya vyakula kwa lengo la kurefusha siku?

    Kwa kadri ya maoni yangu, harakati hizo hazina maana kama mtesekaji husika hatafuti kufurahia kila dakika ya maisha yake nayojaliwa kuipata.

    Halafu kuhusu vyakula. Kibaolojia, hakuna chakula ambacho hakihitajiki. Vyote vinahitajika kwa UWIANO UNAOTAKIWA. Kutokuhitajika kwa vyakula fulani fulani ni suala la kiimani zaidi ambalo laweza kutafutiwa maelezo ya kisayansi.

    Nakubaliana na wewe kwamba siku zote ni bora, kama tutazifanya kuwa bora kwa utashi wetu. Anayezifanya kuwa bora ama za kitumwa ni sisi wenyewe.

    Kufa kupo hata kama tutakwepa sana kufa kwa matesho ambayo hatima yake yatatufanya tushindwe kufurahia hata tusiku tuchache tulivyonavyo. Uamuzi wa maisha yepi tunaishi ni wetu sisi wenyewe hata hivyo. Kwamba ninaweza kuamua kuteseka kwa hiari yangu, na isiwe kosa ikiwa yote yanafanyika kwa utashi.

    JibuFuta
  5. Mungu alikua na maana sana kujificha. angekuwa anaonekana angesumbuliwa na maswali mengi sana, moja ya maswali ambalo lingekuwa kwenye top ya FAQs ni ' Hivi mimi ntakufa lini?'

    Duniani tunafanya mambo kwa imani. tungalijua lini tutakufa tusingalikuwa tukisoma, tukijenga nyumba ama kufanya jambo lolote lile. au tungefanya kwa vipimo vya urefu wa maisha tuliobakia nao kama vile badala ya kuwekeza katika kupanda (plant) miti ilituvune baada ya miaka 15 au 20 tungewekeza katika kilimo ha mchicha endapo tungejuea hatuishi zaidi ya mwezi!

    vivyo hivyo ndio maana watu hujitahidi kuboresha maisha yao ili waishi miaka mingi. na hii ndio falsafa ya kuifanya siku uliyopo kuwa ni bora kuliko jana. kwa matumaini tu. Mungu ndiye muumbaji. na pengime muumbuaji pia. wanaafya hutuambia tusitumie vitu hatarishi eli tuishi miaka mingi. mfano sie wavuta tumbaku huwa tunaonekana kituko kwa kuwa tu eti hatuogopi 'kufa'. lakini wangapi hawavuti tumbaku na wanakufa kwa maradhi mengine ama kwa ajali? haya wengine wana maradhi ambayo hayatibiki lakini hawafi kwayo bali kwa vitu vingine kama ajali na kurogwa na watu wengine wenye vijicho nao.

    Leo ni bora kuliko jana lakini ni bora zaidi kuliko kesho. nani kaiona kesho.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia