Jana nilikuwa nikitazama kipindi cha kiislamu kwenye televisheni ya Chaneli 10. Suala la mali katika ndoa za dini hiyo lilikuwa likijadiliwa. Kwamba Kiislam, mali katika ndoa si suala la wanandoa kwa pamoja. Kwamba mali anazoingia nazo mwanandoa kwenye ndoa, zinabaki kuwa zake mwenyewe. Na wakiachana, kila mmoja anaondoka na alichokuja nacho. Hata ndani ya ndoa, mali zinapatikana 'separately' kwa maana ya kwamba kila anachopata mwanandoa hicho ni haki yake yeye mwenyewe. Wakitengana, kila mtu anaondoka na vyake. Katika kufakari hayo, nilijaribu kumfikiria mwanamke na nafasi yake katika ndoa. Nikamwona kama kiumbe anayenyanyaswa na dini. Kwa nini? Wanaume wengi hutafuta mali kwanza ndio waoe, na hata wanapooa, huwaoa wanawake watakaowategemea wao. Katika hali hii nini salama ya mwanamke katika dini inayoruhusu talaka? Hizi si dalili za wazi za ukandamizaji wa jinsia ya kike?
labda! shabaan Robat alituandikia kwamba, usione ukadhani.
JibuFutandio maana siku huzi huwezi kumuuoa mtu mpaka muonajane kwa sababu anaweza kuonekana hendisamu au biutifulu, kumbe kusini mwa jangwa la majani hakuedeki hata kidogo, sasa wewe ukiona sura tu na maumbile unadhani umeona!\
ofcourse, usichokiona chaweza kuwa muhimu saana kuliko unachodhani unakiona. ndio maana huwezi kumuona mungu. eti kizazi cha leo kinamuona kristo wakati alikufa kabla ya video na kamera kuzaliwa, usipende kuamini jua majamaa yanakupiga changa la macho tu! pweeeeee
usipende kumwona papa kavaa nguo nyeupe ukadhani na roho yake ni nyeupe, usiende kuona padri haoi ukadhani hajui utamu wa ngono hasa zile za wizi wizi!!!!
usipende kuona dini zinajifanya kumjua mungu kumbe ndo chanzo cha machafuko duniani.
usipende kuona bwaya anablogu ukadhani ni mwandishi wa habari. usipende kuona kamala naandika hapa ukadhani yu pamoja nawe
usipend kuona kikwete anaendeshwa kwenye magari ya fahara ukadhani karidhika, usipende kuona, usipende kuona, usipende kuona, we ona to, lakini kila ukionacho, usione ukadhani na wala usikose kutazama.
bora kuwa na jicho moja ukaona ya maana kuliko kuwa na mawili ukaanza kuziba moja ili ule chabo kwa .....
thanx, sipende kuona, napenda kutazama
@Bwaya &Kamala: Siutani!:-(
JibuFutaKamala, una kichwa kinachofikiri.
JibuFutaBwaya umenikumbusha sana mwl.wangu wa kemia,alikuwa akipenda kutoa swali ubaoni kisha akasema wale wenye macho ya ndani ndiyo wenye uwezo wa kuuona mtego.Hapa ana maana ni kwa wale wenye kutafakari tu.
JibuFutaNi kweli wengi huamini kwa kile tukuonacho bila ya kutafakari.
Kamala umenena.