Unavyoweza Kukuza Tabia Njema kwa Mwanao -4
Katika makala yaliyopita tumejifunza aina mbili za misukumo ya utovu wa nidhamu. Kwanza, tumeona mtoto huweza hufanya ukorofi kutafuta kusikilizwa. Anaposumbua na hata kudeka bila sababu, mara nyingi, anajaribu kutuambia kuwa hatujampa muda wa kuwa karibu naye. Anafanya hivyo kutafuta usikivu wetu. Pia, tumeona wakati mwingine mtoto husukumwa na hisia za kutaka kulipiza kisasi. Kama ilivyo kwa mtu mzima, mtoto naye anazo hisia. Anaweza kuumizwa na kauli na matendo anayoyatafsiri vibaya. Jitihada za kupunguza maumivu yake huishia kuwaumiza na wengine. Namna gani tunawasaidia watoto kuondoa tafsiri hizi potofu, huamua aina ya tabia watakazojifunza. Katika makala haya tunaangazia malengo mengine mawili yanayotengeneza msukumo wa kukosa nidhamu.