Vitabu 49 Nilivyovisoma Mwaka 2016
Namshukuru Mungu nimeweza kusoma vitabu 49 kwa mwaka 2016. Nimejifunza mengi. Kusoma ni kama kupata nafasi ya kufanya mazungumzo na watu wa kila namna ya uelewa ambao kwa hali ya kawaida usingeweza kuwasikia vijiweni. Msisitizo wangu umekuwa kwenye vitabu vinavyochambua tabia katika maeneo mbalimbali ya maisha. Hata hivyo, vipo vichache vya masuala ya imani, falsafa na dini. Sijawa msomaji wa riwaya/novel. Nikutie moyo wewe mwenye ratiba ngumu kwa siku. Unaweza kufanya maamuzi ya kusoma ikiwa utaamua kuweka ratiba yako vizuri. Nijitolee mfano mimi mwenyewe.