Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2016

Mbinu Sita za Kukumbuka Maarifa Unayojifunza

Picha
Mafanikio ya kitaaluma, kwa kiasi kikubwa, yanategemea namna unavyoweza kusoma na kukumbuka kile ulichokisoma. Kusoma kwa bidii na kuelewa unayoyasoma ni muhimu. Lakini kama huwezi kukumbuka ulichokielewa, itakuwa vigumu kufanikiwa. Mitihani, kwa mfano, hupima uwezo wako wa kukumbuka kile unachokijua. Hiyo, hata hivyo, haimaanishi uishie kukumbuka. Unahitaji kuelewa unayojifunza kwa kina lakini pia uwe na uwezo wa kukumbuka.

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Picha
Kama tulivyoona katika makala yajuma lililopita , usaili ni hatua ya mwisho kuelekea kupata kazi. Sehemu kubwa ya usaili ni maswali na majibu yanayolenga kupima uwezo wako wa kukabiliana na changamoto halisi za kazi. Ingawa yapo maswali yanayoweza kukupa wasiwasi wa nia ya mwuulizaji, fahamu kuwa hakuna swali linaulizwa kwa nia mbaya au kwa bahati mbaya. Kila swali linaloulizwa linalenga kutafuta uthibitisho kuwa wewe ni mtu sahihi kwa kazi unayoomba.

Mambo ya Kuzingatia Unapojiandaa na Usaili wa Kazi

Picha
Kuitwa kwenye usaili wa kazi ni hatua ya mwisho kuelekea kupata ajira uipendayo. Mara nyingi, kazi inapotangazwa waombaji wa kazi hiyo huwa ni wengi. Baada ya kupokea maombi ya kazi, shughuli inayofuata ni kufanya uchambuzi wa kuwatambua waombaji wanaokaribia vigezo vinavyohitajika. Matokeo ya uchambuzi ni kupatikana kwa orodha ya watu wachache wanaoitwa kwa hatua ya mwisho ya uombaji wa kazi.

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Picha
Katika mchakato wa kuomba ajira baada ya kuona tangazo la kazi, mambo matatu ni dhahiri. Mosi, huombi kazi hiyo wewe mwenyewe. Wapo watu wengi wanaoandika maombi na hivyo kuongeza ushindani wa nani atapata. Pili, nyaraka unazotuma kwa mwajiri mtarajiwa ndizo zinazojenga utambulisho wako kabla wewe mwenyewe hujafahamika. Tatu, afisa mwajiri hatatumia muda mrefu kusoma maelezo yako. Katika hali ya kawaida, atatumia dakika moja kuamua ikiwa amevutiwa na maelezo yako ama la.

Jinsi ya Kukuza Umahiri wa Lugha kwa Mtoto

Picha
Tunahitaji lugha katika maisha yetu ya kila siku. Tunapofikiri mambo yaliyopita, yaliyopo na yajayo, tunatumia lugha. Tunapowasiliana na wengine, tunahitaji lugha. Lugha, katika mukhtadha huu, ni nyezo muhimu inayotuunganisha na watu wanaotuzunguka. Ingawa wataalam wa namna mtoto anavyojifunza lugha hawana jibu moja, ni wazi zipo kanuni za matumizi ya lugha ambazo mtoto huzaliwa nazo. Lakini pia mazingira anayokulia mtoto, nayo yana nafasi kubwa ya kujenga uwezo wake wa kutumia lugha. Ndio kusema, kama mzazi unahitaji kuelewa kuwa unao wajibu mkubwa wa kumsaidia mwanao kuwa mahiri katika lugha. Kujifunza lugha kunafuata hatua kadhaa.

Mpe Mtoto Wako Fursa ya Kujifunza Maisha Halisi

Picha
Katika mazingira yetu, si wazazi wengi wanaweza kuwa tayari kuona watoto hawawezi kufanya kazi za nyumbani kama kupika, kufua nguo, kusafisha vyombo na kutandika kitanda. Lakini kutokuweza kufanya kazi hizi, wakati mwingine kunatokana na mitazamo ya wazazi kuwa kazi za ndani hufanywa na mama peke yake au msichana/kijana wa kazi na hivyo watoto hawaruhusiwi kushiriki kazi ‘zisizo zao’.

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke -2

Picha
Katika makala iliyopita , tuliona kuwa mwanamke anahitaji kujua anavyopendwa na mwenzi wake kwa maneno na vitendo. Kadhalika, tuliona mwanamke anatamani kuwa na uhakika wa nafasi ya kwanza kwa mwenzi wake. Hatamani kuona akishindana kwa umuhimu na chochote kile kinachoweza kuchukua nafasi yake kwa mwenzi wake.

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Picha
WANAUME wengi wanaamini wanawake, kwa kawaida, ‘wanapenda hela.’ Kwamba ukiweza kumhakikishia mwanamke 'uhakika wa kiuchumi' unakuwa umemaliza. Ingawa hatuwezi kupuuza ukweli kuwa uhakika wa 'kiuchumi' ni moja wapo ya mahitaji ya mwanamke, lakini si sahihi kuamini kuwa moyo wa mwanamke unaweza kuthamanishwa kwa fedha. Fikra hizi walizonazo wanaume [kuwa anachokihitaji mwanamke ni fedha] zimeleta matatizo mengi katika mahusiano na ndoa. Kwa mfano, wapo wanaume ambao baada ya kuhakikisha wenzi wao wamepata mahitaji ya msingi, basi wanawatelekeza kihisia. Hali hii husababisha upweke mkubwa kwa wanawake hawa wanaojikuta hawana mtu wa karibu kuwasikiliza isipokuwa vitu.

Jinsi ya Kumsaidia Mtoto Aweze Kushirikiana na Wenzake

Picha
Kushirikiana ni uwezo wa mtoto kuelewa watu wengine wanatarajia nini kwake. Mtoto mwenye ushirikiano na watu, ni mwepesi kutoa alichonacho, ni msikivu, hufanya kazi na wenzake, hucheza kwa ushirikiano na wenzake na huwa na uwezo wa kutafuta suluhu pale anapojikuta katika mazingira ya ugomvi.