Umaafuru wa kitabu hiki nilianza kuusikia huku Marekani, miaka michache iliyopita.
Ni kati ya vitabu vingi ambayo vinasomwa na hao wenzetu, wakati jamii yetu ya Tanzania inaendelea kuzama katika giza au tunangojea kiongozi wa nchi au serikali ituletee maendeleo, na tukijitahidi sana, tunatumia ushirikina. Tuko tayari kulipa laki nyingi kwenye mambo ya ushirikina, eti tupate mafanikio, badala ya kununua vitabu na kuvisoma.
Sasa basi, pamoja na vibuyu vyetu, wenzetu wa-Kenya, ambao wamezingatia elimu tangu zamani, wanaingia nchini mwetu na kujichukulia ajira au kuanzisha miradi. Sisi bado tunahangaika na vibuyu badala ya vitabu. Tutakoma, maana wahenga walisema kuwa asiyefunzwa na mamake hufunzwa na ulimwengu. Na bora iwe hivyo, labda hatimaye tutapata akili.
Uzembe ulivyokithiri miongoni mwa wa-Tanzania, utawasikia wakilalamika mbona kitabu hiki hakijaandikwa kwa ki-Swahili? Wakishauliza hivi, wanaamini wametoa hoja nzito, badala ya kutambua kuwa wanapaswa wajifunze ki-Ingereza na lugha zingine ili waweze kusoma maandishi hayo. Wao wanangoja tu waandikiwe kwa lugha hii wanayoijua. Dunia itawakomesha, kama nilivyosema katika mahojiano na Radio Mbao.
Hao wenzetu wanaosoma "Rich Dad Poor Dad" hawaendi kwa waganga kutafuta vibuyu, bali wakimaliza kitabu hicho, wanaenda kutafuta kingine. Kwa mtindo huu, hatutaweza kushindana nao.
Majuzi nikiwa kwenye mgahawa mmoja mjini, waliingia watu wawili wanaume waliokuwa wamevalia mavazi yanayoashiria imani yao ya kidini. Wote wawili walipamba vichwa vyao kwa vilemba nadhifu, mmoja wao akibeba mfuko mdogo mweusi. Nyuso zao, kwa hakika zilipambwa na tabasamu pana la kirafiki lililofanya ndevu zao ndefu ziwe na mwonekano wa kupendeza. Miguu yao ilivaa viatu vya wazi na juu yake zilining’inia suruali fupi mithili ya kaptula ndefu zilizojitokeza ndani ya kanzu fupi nadhifu.
YAMEKUWEPO madai kwamba Uislam ulianza tangu kuumbwa kwa dunia. Na wapo watu wanaotuaminisha hayo. Ukweli ni kwamba Uislam ulianzishwa na Nabii Muhammad mwaka 622 BK huko Arabia. Kabla yake, dini zilizokuwepo zilikuwa ni Uyuda ambayo ni dini rasmi ya Wayahudi (Judaism) na Ukristo ambayo ni dini ya mataifa wasio Wayahudi ulioanza miaka kadhaa baada ya Yesu kuwa ameondoka mwaka 33BK. Yesu mwenyewe hakuanzisha Ukristo. Alisali katika misikiti ya Wayahudi. Masinagogi. Maelezo haya yana msingi wa kistoria na sio propaganda za kidini. Ndio ni propaganda kwa sababu dini zote zimekuwa na tabia ya kuonyesha kwamba zenyewe ndizo za kweli kuliko dini nyinginezo hata ikibidi kwa kuichezea historia. Na ni bahati mbaya kwamba Dini zimekuwa na tabia ya kufanana ya kuzima uwezo wa waumini wake kuhoji lolote kwa kuwajengea hofu ya kujitafutia laana. Qur’an inatupa maelezo yanayokinzana kuhusu lini hasa Uislamu ulianza. Baadhi ya mistari katika kitabu hicho zinadai kwamba ‘nabii’ Muhammad ndiye ...
Jana nilikuwa nikitazama kipindi cha kiislamu kwenye televisheni ya Chaneli 10. Suala la mali katika ndoa za dini hiyo lilikuwa likijadiliwa. Kwamba Kiislam, mali katika ndoa si suala la wanandoa kwa pamoja. Kwamba mali anazoingia nazo mwanandoa kwenye ndoa, zinabaki kuwa zake mwenyewe. Na wakiachana, kila mmoja anaondoka na alichokuja nacho. Hata ndani ya ndoa, mali zinapatikana 'separately' kwa maana ya kwamba kila anachopata mwanandoa hicho ni haki yake yeye mwenyewe. Wakitengana, kila mtu anaondoka na vyake. Katika kufakari hayo, nilijaribu kumfikiria mwanamke na nafasi yake katika ndoa. Nikamwona kama kiumbe anayenyanyaswa na dini. Kwa nini? Wanaume wengi hutafuta mali kwanza ndio waoe, na hata wanapooa, huwaoa wanawake watakaowategemea wao. Katika hali hii nini salama ya mwanamke katika dini inayoruhusu talaka? Hizi si dalili za wazi za ukandamizaji wa jinsia ya kike?
WANAUME wengi wanaamini wanawake, kwa kawaida, ‘wanapenda hela.’ Kwamba ukiweza kumhakikishia mwanamke 'uhakika wa kiuchumi' unakuwa umemaliza. Ingawa hatuwezi kupuuza ukweli kuwa uhakika wa 'kiuchumi' ni moja wapo ya mahitaji ya mwanamke, lakini si sahihi kuamini kuwa moyo wa mwanamke unaweza kuthamanishwa kwa fedha. Fikra hizi walizonazo wanaume [kuwa anachokihitaji mwanamke ni fedha] zimeleta matatizo mengi katika mahusiano na ndoa. Kwa mfano, wapo wanaume ambao baada ya kuhakikisha wenzi wao wamepata mahitaji ya msingi, basi wanawatelekeza kihisia. Hali hii husababisha upweke mkubwa kwa wanawake hawa wanaojikuta hawana mtu wa karibu kuwasikiliza isipokuwa vitu.
Dan Brown mwandishi wa kitabu kinachokwenda kwa jina la Da Vinci Code , kafanya kile ambacho binadamu wengine hatuthubutu hata kukijadili. Kaamua kuchokonoa mambo ya kiimani ambayo watu tunakwepa kuyahoji, kwamba hayajadiliki. Ni dogma. Trela ya filamu yake hii hapa . Katika Da Vinci code, Dan Brown anajaribu kuchimbua “kweli” zilizojificha nyuma ya ukristo, “kweli” ambacho zimefunikwa na kanisa ili kuwapumbaza watu waamini kwamba Jeshua alikuwa mwana wa Mungu. Kwa kadiri ya Da Vinci Code, ukweli wenyewe ni kwamba Ukristo ulianzishwa na “nabii wa kawaida” ambaye hastahili kujidai kwamba ana uungu (divinity) wowote. Nabii mwenyewe ni Yesu Kristo. Kwa hakika, alimwoa Mariam Magdalena, ambaye baadaye ndiye aliyemchagua kuliongoza kanisa baada ya kifo chake. Suala hili, kwa mujibu wa Da Vinci Code, liliwakasirisha sana wanafunzi wake na baada ya kusulubishwa kwake, Mariam Magadalena ilibidi atimuliwe, ndipo akakimbilia Ufaransa na mtoto wao waliomzaa na Yeshua “mume” wake. Mwandishi anas...
SAIKOLOJIA, neno lililotoholewa kutoka neno la kiingereza psychology, si elimu inayoeleweka sana katika jamii yetu. Asili ya 'psychology' ni neno 'psyche' lenye maana ya nafsi. Katika makala haya, tunasaili kwa ufupi maana ya saikolojia kama taaluma na kuonesha nafasi ya taaluma hiyo ngeni katika jamii yetu katika kutatua matatizo ya kijamii na hivyo kuharakisha juhudi za watu kujiletea maendeleo yetu.
Napenda kutazama kipindi cha Longa Mwanamume kinachorushwa na kituo cha luninga cha ITV kila Jumatano saa tatu usiku. Mzee Barnabas Maro anakiweza. Pamoja na kwamba mara nyingi wanaume wamekitumia kipindi hicho kuonesha mabavu yao kwenye mahusiano, lakini si kipindi kinachofanana na mavipindi mengine ya nchi za nje yasiyohusiana na utamaduni wetu. Longa Mwanamume ni kipindi kizuri. Jana ulikuwepo mjadala wa ndoa. Swali lilikuwa: Kwa nini ndoa za siku hizi hazidumu? Nilifurahia majadala huo. Wazungumzaji walitaja sababu nyingi ambazo ni za kweli. Nami kama ningeweza kuchangia, ningesema ndoa za siku hizi hazidumu kwa sababu vijana huanza kujuana kimwili kabla ya ndoa. Na kufanya hivyo hujenga tabia ya kutokuaminiana na mwisho wake ni kuvunjika kwa ndoa. Wewe ungesemaje?
Umaafuru wa kitabu hiki nilianza kuusikia huku Marekani, miaka michache iliyopita.
JibuFutaNi kati ya vitabu vingi ambayo vinasomwa na hao wenzetu, wakati jamii yetu ya Tanzania inaendelea kuzama katika giza au tunangojea kiongozi wa nchi au serikali ituletee maendeleo, na tukijitahidi sana, tunatumia ushirikina. Tuko tayari kulipa laki nyingi kwenye mambo ya ushirikina, eti tupate mafanikio, badala ya kununua vitabu na kuvisoma.
Sasa basi, pamoja na vibuyu vyetu, wenzetu wa-Kenya, ambao wamezingatia elimu tangu zamani, wanaingia nchini mwetu na kujichukulia ajira au kuanzisha miradi. Sisi bado tunahangaika na vibuyu badala ya vitabu. Tutakoma, maana wahenga walisema kuwa asiyefunzwa na mamake hufunzwa na ulimwengu. Na bora iwe hivyo, labda hatimaye tutapata akili.
Uzembe ulivyokithiri miongoni mwa wa-Tanzania, utawasikia wakilalamika mbona kitabu hiki hakijaandikwa kwa ki-Swahili? Wakishauliza hivi, wanaamini wametoa hoja nzito, badala ya kutambua kuwa wanapaswa wajifunze ki-Ingereza na lugha zingine ili waweze kusoma maandishi hayo. Wao wanangoja tu waandikiwe kwa lugha hii wanayoijua. Dunia itawakomesha, kama nilivyosema katika mahojiano na Radio Mbao.
Hao wenzetu wanaosoma "Rich Dad Poor Dad" hawaendi kwa waganga kutafuta vibuyu, bali wakimaliza kitabu hicho, wanaenda kutafuta kingine. Kwa mtindo huu, hatutaweza kushindana nao.