Ujumbe wa Juma: Wapiga kura waumbueni REDET

"...Wapiga kura wasianze kukata tamaa kuwa CCM wataiba kura. Of course wataiba lakini ili 'kura zitoshe' watalazimika kufanya wizi wa 'mchana mweupe' (day light robbery) jambo ambalo sio rahisi sana,japo linawezekana.Wanaweza tu kuchakachua matokeo kama,kwa mfano Dokta Slaa akipata asilimia 51 na Kikwete asilimia 49.Hapo watarejea uchakachuaji kama ule wa Zanzibar.Lakini kama ni tofauti ya double digits,wanaweza kupatwa na kigugumizi katika kufanikisha ujambazi huo.

Ni muhimu kutovunjwa moyo na hujuma hizi.Yatupasa kufahamu kuwa Kikwete na CCM yake ni kama mgonjwa mahututi ambaye yuko tayari hata kuning'inia kwenye uzi ili asalimike.Tutashuhudia vituko zaidi ya huo uchakachuaji wa REDET..."

Kwa makala nzima bonyeza hapa. Asante sana Ndugu Evarist Chahali wa kulikoni Ughaibuni.

Maoni

  1. Kabla sijaenda kwa kaka Chahali niseme tangu ilipoanzishwa REDET sijawahi kusoma wala sitarajii kusoma tafiti zao, nawaju,nawafahamu,naelewa kiasi fulani dhana ya utafiti huo. tumekaa tunajadili REDET na wasomi wetu hao wanakaa na kutusimulia sisi wachovu akina markus tusiojua kitabu wanatuletea takwimu.

    KAKA BWAYA nakuchia swali;
    HIVI KUJUA CHAMA CHA MAPINDUZI KITASHINDA AU MGOMBEA WAKE ATAKUWA NA ASILIMIA KADHAA INAWAWEZESHAJE WALE WANAOJIFUNGULIA PORINI? INAWASAIDIAJE WALE WANAUGUA HATA POLIO? nilidhani REDET watakuwa wanaendesha tafiti za kukabiliana na majanga ya mafuriko na mambo mengine ya msingi. samahani mimi huwa siamini maoni hususani tafiti za namna hii kuakisi hali halisi. labda kura za maoni za kupiga wenyewe wananchi lakini hizi za kuuliza swali uchwara na kukamilisha tafiti siamini. REDET wanatumia pesa kibao kutafiti eti fulani anaongoza ktka uchaguzi....... ha ha ha ha ha ha kalaghabaooooooo REDET ni mchezo wa rede au kombolela tu

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?