Yuko wapi Ndesanjo Macha?

NIMEKUWA msomaji mzuri wa maandiko ya Ndesanjo. Kuna wakati nakumbuka nilikuwa nakesha kwenye mtandao kusoma makala zake motomoto. Nilikuwa 'naumwa' kumsoma. Huyu bwana ni msomi wa kweli kweli. Na lazima nikiri kwamba amekuwa changamoto kubwa katika ufahamu wangu, hasa katika masuala ya utamaduni wetu.

Naandika kusikitika kwamba siku hizi amekuwa kimya. Haandiki tena Gumzo la Wiki kwenye Mwananchi, na zile makala zale za ripway zimepotea.

Nauliza, wapi Ndesanjo Macha?

Maoni

  1. Ni kweli kaka Bwaya, Kaka Ndesanjo kapotea kweli kwani nami nimekuwa nikimsoma kidogo

    JibuFuta
  2. Kaka Bwaya, huyu bwana nammiss kikweli kweli. Ndiye aliyenifanya nijue kuna kitu kublog duniani. Kupitia makala zake katika gazeti la Mwananchi. Namtafuta mtandaoni haonekani, magazetini nako kimya. Kaka mkubwa upo wapi?

    JibuFuta
  3. Nilizoea kusoma makala zake za Masudi Mselle katika gazeti la Mwananchi, na miss sana stori za Masudi mselle....

    JibuFuta
  4. kafariki dunia ua nnoma inamtafuna kama hajawekwa ndani na jimama la maraha!

    JibuFuta
  5. kafariki dunia ua nnoma inamtafuna kama hajawekwa ndani na jimama la maraha!

    JibuFuta
  6. Unaweza kukuta niko karibu na hapo ulipo dakika hii. Nipe namba yako ya simu.

    Unajua blogu ina mzunguko wake: tulianza kublogu kwa kuhamasisha. Watu wakasikia, blogu zikaanzishwa na zinaendelea. Kisha ukaja mzunguko wa kutumia elimu hii kikazi, hivyo kublogu kule kwa kuhamasisha muda wake mdogo sana maana umechukuliwa na mzunguko wa kutumia elimu ya blogu kama ajira kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali, makampuni, serikali, n.k, kuelewa jinsi ya kutumia teknolojia hii. Yaani kutoa ushauri wa kitaalamu.

    Makala za ripway. Unajua ripway wajinga sana. Eti usipoingia kwenye tovuti yao baada ya muda fulani, makala zako zinafungiwa. Makala zote zile na nyingine mpya zitakuwa kwenye Google Docs. Ninahamisha na pia kubadilisha kabisa Jikomboe. Itakuwa kitu kingine, lakini kizuri zaidi.

    Mengine ninayoandika unaweza kuyapata hapa:
    http://globalvoicesonline.org/author/ndesanjo-macha/

    JibuFuta
  7. Ahsante kaka kwa kujitokeza hadharani. Nimefurahi sana. Mungu akubariki sana, kazi yako ni kubwa mno. Nakutakia mafanikio daima katika pilika zako.

    JibuFuta
  8. Ndesanjo karibu tena. Mazoea yana tabu. Mara nyingine huwa naona kama blogu zinapwaya pwaya hivi pasipo wewe.

    Fanya uirejeshe ile mistari ya ufahamu. Lile lilikuwa darasa kamili kwa kila aliyetamani kufikiri.

    Halafu lile gumzo la Wiki ukilifanyia mpango wa ufufuzi utatusaidia.


    Namba yangu haipatikani muda mwingi ila ni ile ile niliyoitundika pale kwenye profile.

    Nimefurahi umejitokeza hadharani.

    JibuFuta
  9. if only we could talk about jumuwata.

    rasta hapa.

    JibuFuta
  10. Asalam Alleikum Bwaya!
    Nimepita kama kawaida kukusabahi!

    JibuFuta
  11. poa kaka hakuna noma lakin mi niko hapa ughaibuni kama nyundo 5 sasa ninamiss makala yako ya kutoka ughaibun sasa ninaweza kuipata vp kwa kila toleo au huitoi tena

    JibuFuta
  12. yaaah hata mimi naimiss tutaipata vp

    JibuFuta
  13. kutoka ughaibun babkubwa tutaipata vp

    JibuFuta
  14. yaaah kweli jamaa hapo juu kutoka ughaibun bab kubwa

    JibuFuta
  15. Kitururu karibu sana. Nimefurahi unanitembelea mara kwa mara.

    Kuhusu ujenzi wa Jumuwata kama anavyodokeza Rasta, nafikiri tupate mawazo ya Ndesanjo sasa...

    Uzoefu wake nadhani utatufaa kwa wakati kama huu.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Uislamu ulianza lini?