Nuru anakuuliza: "...Sura yako hasa ni ipi?"

Kuna kitu ambacho huwa ninajiuliza kila mara, hivi mimi sura yangu ni ipi?
Huwezi ukakubali kwa haraka hadi utakapojifanyia uchunguzi ndipo utakapogundua hauna sura moja.

Unapokuwa unaongea na mpenzi wako unakuwa na sura gani?
Unapokuwa unaongea na wazazi wako unakuwa na sura gani?
Unapokuwa umefurahi unakuwa na sura gani?
Unapokuwa umekasirika unakuwa nasura gani?
Unapoongea na bosi wako Je?
Unapoandika email au kuchangia maoni je?
Haya ni maswali ambayo huwa ninajiuliza mara kwa mara.
Je sura yangu ni ipi na nifanye nini ili niijue sura yangu halisi?

(c) Nuru Shabani, 2009

Maoni

  1. Mwonekano wa sura yako unategemea na hali uliyonayo na wakati mwingine mtu mwenyewe huamua sura yake ionekane vipi.Kwa mfano unaweza kuwa ktk hali ya hasira na ukaamua kuonyesha uso wa furaha.
    Kumbuka kwa mpenzi mathalani, si lazima kumuonyeshea sura ya furaha, upole n.k. vile vile hata kwa marafiki, wazazi n.k.unaweza kuonyesha sura yoyote kulingana na hali na wewe utakavyoamua, kama nilivyoelezea hapo juu.

    JibuFuta
  2. hii segment nimeipenda sanaaa bcoz inauliza maswali ambayo yana kudefine you as a person..una morals,principle na msimamo gani kimaisha..one may ask ni kweli kwamba huwa tunasura nyengine wakati twaongea na wazazi wetu but inategemea na malezi na mazingira..ulaya for instance pia inategemea ulaya upo nchi gani unaweza taniana na bosi wako na kuongea nae km kawa as long as everybody knows their roles..i think these questons are absolutly fantastic n everybody ajiuilize haya maswali kujielewa..ahsante

    JibuFuta
  3. sura yangu labda ni yako. unaweza kumouna mtu ukajua jinsi unavyomfahamu japo humkubuki na wala hukumbuki mlionana wapia ila unamfahamu.

    swali zaidi, unakuwa na sura gani wakati unaelekea, uko na unapotoka chooni ikifananishwa najikoni au hotelini

    JibuFuta
  4. fredkatawa14/4/09 9:02 PM

    sura yangu halisi inaweza ikajulikana mara tu baada ya kuzaliwa kabla ya kufundishwa lipi ni jambo baya na lipi ni zuri.Kabla sijaambiwa sura nzuri ikoje na mbaya inafananaje.kabla sijafundishwa kukasirika au kufurahi.

    Kwa mtu mkubwa sura yake halisi inaweza kujulikana kwa mtu aliyejikubali na kujipokea yaani anayejua kusamehe na kupuuzia mambo yanayokasirisha,sura halisi ya mtu huyu itatokana na matendo mema.

    JibuFuta
  5. mimi sura yangu imejaa tabasamu na bashasha.......

    JibuFuta
  6. mimi sura yangu imejaa tabasamu na bashasha.......

    JibuFuta
  7. Koero unataka kuniambia mimi na wasomaji wengine kuwa hata ukikasirika mwonekano wako haubadiliki? Sasa mtu atajuaje kuwa umekasirika? Au huwa kukwaziki?

    Ukiwa na furaha je? inakuwa zaidi ya tabasamu na bashasha au vipi?

    JibuFuta
  8. sura yangu ni kama nilivyo haijabadilika tangu nizaliwe.

    JibuFuta
  9. Duh!! Swali gumu na ndio maana nikaishia kupata swali wakati nikisaka jibu. Nami wakati ninafikiri hapa nimepiga chafya (almanusura nijikimbie) maana nimegundua kuwa nina sura nyingine tofauti. Sura ya kupiga chafya, kuchomwa sindano, kumeza krolokwini, kukamatwa ugoni, kubarikiwa, kufunga ndoa, kumuona mwanao kwa mara ya kwanza, kushinda bahati nasibu. Hivi ni kweli kuwa hazifanani eeeeee?
    Labda sura yakjo ni ile uliyonayo kwa wakati uliopo.

    JibuFuta
  10. Kisima, sasa huniamini?
    Mimi sura yangu iko kama ilivyo, na haibadiliki........

    JibuFuta
  11. Kama ndivyo, hongera sana dada Koero, hicho ni kipaji cha pekee kabisa.

    JibuFuta
  12. Kama ndivyo, hongera sana dada Koero, hicho ni kipaji cha pekee kabisa.

    JibuFuta
  13. MBELE YAKO NI NYUMA YANGU
    ndiyo maana ya sura, kwani ni matendo yako na yangu katika mazingira tofauti

    dada NURU nawasilisha hoja, matumizi ya lugha ni muhimu ndugu yangu, eeeheee usije ukanichapa kofiii bureeee.

    SURA yako ni ipi? ni ile ambayo ina jicho chongo au ile tumaanishayo ni tabia na mwenendo wako katika mazingira au matukio???
    Koero umejaa tabasamu????? mmmmmh ngoja nitakuhoji baadaye.

    lakini hii mada sijui inanikumbusha kitu au la lakini inafundishi kitu muhimu sana nacho ni SURA kwa maana ya tabia na mwenendo wa binadamu siyo sura nzuri ya kuongea na mpenzi wako.

    Ile sura ambayo daima inakabiliana na matukio mazuri au mabaya kwa nia ileile isemekanayo kuwa hufanywa na wanadamu. lakini tujiulize maana ya SURA zetu ni kupendeza kwetu au matendo yetu? nini hasa tulichokielewa katika mada hii. Maana nazama mbali na hapa kwani Bwaya kaleta jambo muhimu sana.

    Ikiwe ukiwa na mpenzi wako unaweza KUJAMBA? au unaweza kula msosi kwa kufakamia kama jamaa asiyekula miaka kdhaa au ulapo na washkaji??

    SURA yako nipi hasa??? jamani tutafakari kwa umakini sana hii mada nadhani kuna zaidi ya sura tuzionazo kwa mikogo na tabasamu marishi.

    Bwaya mada hii irudiwe tena kwani naona watu wanajibu ipasavyo kama nianavyo mieeeee

    JibuFuta
  14. Sura ni mwonekano wa mtu au kitu.
    Nikirejea kwa mtu ambaye ndiye muhusika mkuu ktk makala hii; mwonekanano ninaomaanisha hapa si namna mtu alivyovaa, uso wake ukoje n.k, namaanisha mwonekano wake ktk mazingira tofauti kulingana na namna ambavyo mazingira haya yamemgusa, pia hali tofauti anazokumbana nazo mtu ambapo namna ambavyo hali hizi zinamgusa huonyeshwa na mwonekano wake.

    Kwa hiyo sura ya mtu hutegemea na mazingira na hali aliyonayo mtu na ni namna gani mambo haya mawili yanamgusa.

    Kaluse, Kulingana na makala ilivyowasilishwa, kuna sehemu inaelezea tabia na mwenendo wa mtu, kwa mfano swali lililouliza "ukiwa na mzazi wako je" (sina hakika kama nimenukuu kama ilivyo) pia kuna sehemu inayomaanisha mwonekano wa uso, kama kwenye swali la internet cafe. Kwa mtizamo wangu mimi naona yote mawili ambayo Kaluse umeyaongelea(sura na uso) yanaweza kuhusishwa kwa kuzingatia hali pamoja na mazingira.

    Bila kuzingatia makala hii, je kuna tofauti kati ya sura ya mtu na uso wa mtu au inategemea na sehemu ambapo maneno haya mawili yalipotumika na kwa malengo gani?

    JibuFuta
  15. Samahanini, kwenye swali la intanet cafe , nilimaanisha swali lililouliza ,unapoandika e mail au kutoa maoni je?

    JibuFuta
  16. Nilipokuwa shule, kuna mwalimu wetu mmoja alikuwa akitufundisha mambo ya uigizaji, yaani namna unavyoweza kucheza na sura yako na kujenga hisia tofauti tofauti (facial expresion and gestures). lilikuwa ni zoezi gumu sana, kwani tulitakiwa kujenga sura ya huzuni, furaha, hofu, dharau,kulia, kutahamaki, kutulia na kuonekana kama unawaza kitu chenye kufurahisha na labda chenye kuhuzunisha pia. ni zoezi ambalo kila mtu alitakiwa atengeneze sura zote kwa wakati mmoja. Hili zoezi lilikuwa ni gumu na lenye kuhitaji uzingativu. Hapo ndipo nilipokuja kugundua kwamba sisi wanaadamu tunazo sura nyingi sana kutokana na namna tunavyolipokea tukio.......

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?

Pay $900? I quit blogging