Nimemkuta Prof. Mbele Arusha


Awali kuna rafiki yangu aliniambia. Nilipofika Arusha wiki hii na kupita pita kwenye maduka ya vitabu, nikakutana uso kwa uso na kitabu cha Prof. Mbele, "Africans and Americans: Embracing Cultural Differences".

Pale KIMAHAMA mkabala na Golden Rose kinauzwa bei nafuu Tsh. 15,000. Kwa wadau wa Arusha, mnaweza kujipatia kitabu hicho pale mjionee wenyewe.

Maoni

  1. Hivi hakipatikanei hapa Dar?

    JibuFuta
  2. Ndugu Kaluse, mimi kama mwalimu, kazi yangu ni kuwamegea wanadamu kila ninachojua katika taaluma yangu, na ndio maana ninafanya utafiti sana, nafundisha na kuandika muda wote. Furaha yangu ni kuwapata watu wa kusikiliza ninayosema, kusoma ninayoandika, kuyatafakari, na kulumbana nami. Najifunza kutoka kwao, kama vile wao wanavyojifunza kutoka kwangu. Hapo sote tunafaidika.

    Kuhusu suali lako, vitabu vyangu vinapatikana Dar es Salaam, simu namba 0754 888 647 au 0717 413 073

    JibuFuta
  3. Nimekusoma Prof. Mbele.
    Nitamtafuta mhusika na kujinunulia vitabu kadhaa. Nimefurahi kuwa hata bei ya vitabu vyako inamwezesha kila Mtanzania wa kipato cha chini kumudu kununua.
    Ahsante sana kwa kutugawia maarifa yako kwa bei karibu na bure...

    JibuFuta
  4. Ndugu Kaluse, shukrani nawe. Kule kijijini, sisi tunaoenda vilabuni tunajua mila ilivyo. Kabla hujanunua kangara yako au ulanzi, wanakuchotea kidogo uonje. Nami nakuchotea kidogo hapa :-)

    JibuFuta
  5. yaani mimi pamoja nakupenda utamaduni wa kiafrika nilikuwa bado na bado sijafikiria kununua vitabu hivi. najishangaaa! lakini nitavitafuta bwana maana lazima nivisome kwani maarifa hayana mwisho.

    kaluse tuvitafute wote bwana. lakini prof kama vp tuelekeze duka kabisa na siku hizi naona duka la TPH lilmefungwa sijui limehamishwa?

    JibuFuta
  6. Ndugu Kamala, shukrani. Nami nilisikia kuwa TPH pamefungwa. Nilidhani walikuwa katika matengenezo, lakini imekuwa muda mrefu sana. Mkurugenzi wake, Bwana Karugendo, ni mtu makini kwenye masuala ya vitabu. Nilipata fursa ya kuongea naye mara kadhaa pale ofisini. Walikuwa wanauza kitabu changu kimojawapo. Lakini hiki tunachoongelea sasa kinapatikana Sinza, karibu na Kijiweni.

    JibuFuta
  7. Kamala usije ukaenda ukavinunua vyote ili uje utulangue, maana wabongo nawajua kwa usanii.

    Prof. Mbele nitavitafuta kwa bidii kuanzia wikiijayo, kwani wiki hii na sikukuu hizi, naona kama vile bajeti imebana.

    Ahsante kwa kunisikilizisha hiyo link ya Butiama.

    Swali:

    Vipi tukutarajie 2010?
    nadhani umenielewa........

    JibuFuta
  8. Ndugu Kaluse, siamini kama nitaiweza kazi nyingine yoyote zaidi ya ualimu. Moyo wangu uko katika ualimu, tangu nilipokuwa mdogo, sijaanza shule.

    Halafu, mimi hupenda maisha ya mtu wa kawaida. Nilikulia kijijini, na maisha ya wanasiasa wa leo siyawezi, yaani maisha ya ulimbwende katika nchi ambamo wananchi kwa ujumla wana dhiki. Naziheshimu sera za Mwalimu Nyerere za kuzuia haya matabaka.

    JibuFuta
  9. Hiki kitabu kifundisha na kuburudisha. Kinakuelezea mambo ambayo yangekuchukua miaka kadhaa kuyaelewa au usiyaelewe kabisa harafu Prof.Mbele kakiandika with sense of humor utacheka sana.nimekipenda sana.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia

Pay $900? I quit blogging