Urafiki unawezekana bila ngono?

Habari za siku mbili tatu ndugu msomaji. Nafurahi kwamba umeendelea kuwa mtembeleaji wangu kwa kipindi chote nilipokuwa mwituni. Nimerudi na vijiswali hivi vidogo kuhusu suala la urafiki na ngono. Naomba kuyaweka mezani:

Je, rafiki ni nani? Ili mtu awe rafiki yako mambo gani ni ya msingi kutimia?

Je, rafiki wa jinsia iliyop tofauti na yako ana tofauti gani na rafiki wa jinsia yako?

Je, kuna uwezekano wowote wa kuwa na urafiki na mtu wa jinsia nyingine bila ngono?

Je, urafiki upi unauwezekano wa kudumu zaidi, ule wenye kuhusisha ngono ama ule usio wa kingono? Kwa nini?

Na je, inawezekana kufanya uamuzi wa kuishi bila ngono kabla ya ndoa?

Maoni

  1. Urafiki unajumuisha yafuatayo;

    1. Kila mmoja kumkubali mwenzake kama alivyo.

    2. Common interests and goals.

    3.Wanaoweza kuziondoa tofauti zao pale zinapotokea bila ugomvi, bali kwa majadiliano na kufikia uamuzi wa pamoja pasipo mawazo ya mmoja kutawala.

    3. Mwisho,ni yule ambaye atakuwa karibu nawe wakati wengine wakiwa wamekukimbia.

    Mimi nafikiri asilimia kubwa ya maswali yanayofuata nimeshayajibu.

    Hivi nimefanikiwa kuona,kuangalia au kutazama?,mh!

    JibuFuta
  2. Namuunga mkono kisima.

    JibuFuta
  3. swali la kwanza ni kwamba rafiki ni bwaya, nuru na kissima. kila mtu na kila kitu ni rafiki na ndio maana tunahitajiana kwanjia moja au nyingine!

    ndio kuna urafiki wa kuwa na rafiki wa jinsia nyingine bila ngono. kwa mfano, koero ni rafiki yangu na sina hata mpango wa kumtongoza hata kama ni mzuri kivvipi. tutaendelea kuwa marafiki bila mpango wa ngono wala busu.

    urafiki unaweza ukadumu. japo wewaza kubadilia kutoka kwenye ikufanya ngono kuelekea kwenye kutofanya na kutoka kwenye kutofanya kwenda kwenye kufanya (onyo; wangu nakoero hauelekei popote hapo!! na hivyo urafiki woote unadumu. bwaya jiulize ukutanapo na demu wako wa zamani huwa unatema mate? unamtusi? au mnasalimiana na kuanza kukumbukia upuuzi wenu wa enzi zile kwa furaha ya kichizi kama vile unatamani enzi zenyewe zirudi lakini hata zikirudi hazitakuwa kama zile?

    ukisema uwezekano wa kuishi bila ngono kabla ya ndoa sikuelewi, ndoa ninini? ya padre, bomani au mtala? si mkitongozana na kukubaliana mmeoana? unaweza kuvua nguo na kumuingiza mtu bila kumwoa? ndoa ni suala binafsi na hivyo sijui kabla ya ndo unamaanisha nini

    FIKIRI-TIKSABICHWA-CHEKA-TAFAKARI.......

    JibuFuta
  4. Kamala, nimetafakari vyema mchango wako.

    Aidha baada ya kutafakari, nimeona kuna umuhimu wa kuliangalia hili suala la ndoa kwa mapana yake.

    Labda pa kuanzia ni hapa: Hivi ndoa ni nini? Je, ni suala 'binafsi' kwa maana kwamba kule kukutana kimwili na mtu wa jinsia nyingine kutatosha kusema hiyo ni ndoa?

    Hebu tuliangalie vyema suala hili.

    JibuFuta
  5. KAMALAAAA...!!!!????????::::;;;;

    DUH............

    JibuFuta
  6. Rafiki ni yule ambaye anaweza kuwa badala yako kimawazo. Yule mliye na mnayeshirikiana katika mengi kiuaminifu. Sasa hapa nasema unaweza kuwa na mzazi asiwe rafiki na mwingine mzazi akawa rafiki pia. Unaweza kuwa na mke ama mume na asiwe rafiki na wapo wasio na waume wala wake wakawa marafiki. Kwa undani wake utakuta urafiki hujengwa na hauchaguliwi. Unatumia muda mwingi saana kuujenga na unahitaji zaidi ya salamu na matembeleano. URAFIKI ni kama kubadilishana majukumu muhimu na yawezekanayo katika maisha. Mwenye kuweza kufanya hayo atakuwa na rafiki. Sasa tunachanganya saana urafiki na wafanyakazi wenza, wanafunzi wenza, wana-blog wenza na wenza(s) nyingine.
    Kuhusu URAFIKI na jinsina naamini tafsiri yake inaenda zaidi ya nani ni nani. Urafiki unakuja kwa majukumu na si mahitaji. Kwa hiyo kuwa na rafiki wa jinsia nyingine yawezekana.
    Juu ya udumu wa urafiki basi hapo ni kuangalia tafsiri pia. Lakini kama unadumu kwa ngono nadhani ni ulafi na kama haudumu kwa ngono lakini kwa pesa ni ulafi pia. Kama ni urafiki unaodumu kwa kuwa anakuangalizia mwana unapokuwa kazini ni ulafi na kama ni urafiki kwa kuwa ukiwa na shida una kimbilio na hilo ndilo pekee likuwekalo kwake ni ulafi na yote haya nu UBINAFSI.
    Kuishi bila ngono kabla ya ndoa. Inawezekana japo sitapenda kuulizwa kivipi. Lakini najua inawezekana. Kumbuka nguvu ya fikra inaongozwa na matamanio ya mipango yetu. Ukipanga ngono utaipata na usipopanga kuipata ama ukiamua kuipuuzia hutaathirika kwa kutokuwa nayo.
    Suala ni kwamba ni fika ngapi zaendeshwa na mioyo yao na si macho? Tumefikia hatua ya kumuona mtu akiwa amevaa overall tukamu-imagine akiwa mtupu. Ndio uone nguvu ya fikra inavyoweza kukua kutokana na udhaifu wa kuyaacha macho kuwa na maamuzi ya mvuto wa kila uonacho.
    Lakini INAWEZEKANA BILA NGONO as long as URAFIKI UMETANGULIZWA na KUJENGWA kabla ya faida na hasara za urafiki.
    Nimefurahi kuwasoma nyote
    Blessings

    JibuFuta
  7. Kuhusu swali la ndoa Kaka Bwaya niseme kuna mapitio matatu makuu. Kuwaza, kunena na kutenda. Sasa sioni kama kuna ndoa zaidi ya yenye vitu hivi vitatu. Yaani nimuwaze me wangu pekee, nimwambie yeye pekee na nimtende yeye pekee hata kama sijaenda kanisani, msikitini ama bomani si nitakuwa naiheshimu ndoa kwa mila, desturi, katiba, imani na maandiko yote?
    Ndio ndoa. Kwangu haijalishi umeifanyaje, umefuata taratibu gani, umemualika na kumshirikisha nani. As long as hayo matatu makuu ni nguzo yenu wawili, basi mtajiona kama mu-wamoja na hiyo ndio ndoa. Mengine ni ushahidi, umaarufu, hasara / faida na pilika zisizosaidia undani wa maisha ya kindoa na kifamilia.
    Blessings

    JibuFuta
  8. Kamala, katika mjadala ukiweka "labda" tunashindwa kuendelea zaidi ya hapo.

    Mzee wa changamoto, nimefurahi kukusoma. Ama kwa hakika umekoleza munyu mjadala huu.

    Tafsiri yako ya urafiki imeunganika vyema na hoja ya urafiki wa jinsia mbili. Umeweka msingi mzuri sana wenye hadhi ya kuwa maoni-rejeo. Asante sana.

    Aidha, kuhusu tafsiri ya ndoa naona kuna haja ya maelezo ya kiada. Wewe umeyaweka mambo matatu kama msingi wa ndoa yaani umuwaze yeye pekee, umwambie yeye pekee na umtende yeye pekee. Binafsi nayaafiki. (wapo watu hawaamini katika hayo)

    Hata hivyo, ninaona kama upo umuhimu wa ushahidi wa nje katika kuyafanya hayo matatu yahadhike kuwa ndoa inayokubalika katika mazingira yetu ya Kiafrika.

    Vinginevyo nionavyo mimi ni kwamba matatu hayo yanaweza kubaki kuwa na maana ya urafiki mzuri bila kumaanisha ndoa pasipo suala la ushahidi.

    Na ikiwa hivyo, yaani bila ushahidi, muunganiko huo unakuwa katika uhuru uliopitiliza kwa maana ya kurahisisha anguko lake pasi na uwezekano wa jamii kuhusishwa.

    Ushahidi hapa haimaanishi mambo ya kisheria, la bali kule kuwaarifu wengine (jamii hasa wazazi) kuhusu nia ya wawili hao ya kutaka kuishi pamoja.

    Sababu ni kwamba katika mazingira ya Kiafrika, ndoa ni jambo lisilokwepa hadhira nyingine zaidi ya wawili hao.

    Ninachojaribu kukuiingiza katika hayo matatu ni hiki kinachoitwa tangazo la ndoa. Kwamba kuna mtazamo kwamba ndoa ni tangazo la watu wawili kwa jamii kwamba wawili hao wanayaishi hayo matatu uliyoyataja wewe.

    Tangazo hilo linahalalisha nia ya watu wawili wanaoiomba jamii kuwa wanandoa.

    Kwa meneno mengine, ndoa bila jamii (ushahidi) haiwezi kubeba maana halisi ya ndoa (katika mazingira yetu.

    Unasemaje katika hili?

    JibuFuta
  9. Kaka Bwaya,hili swala la ndoa unaliangalia kwa kujali utamaduni au? Kwani kwa maelezo yako hapo juu,ume-refer mazingira ya kiafrika,yani utamaduni wetu. Ni dhahiri shahiri kwamba,kulingana na utamaduni wetu,ukimchukua mwenzi wako na mkaishi naye bila kuhalalishwa kanisani,msikitini,mahakamani,ndoa za mkeka n.k. Uhusiano wenu hautatambulika.

    Kutokutambulika huku hutokea pale wawili hawa mnapokumbana na matatizo ambayo yanahitaji msaada wa kisheria,kidini,kijamii n.k. Mifano halisi ya matatizo haya ni kama talaka,swala la mgawanyo wa mali endapo mtaachana, swala la mirathi n.k

    Hivi kwa ndoa ambazo hazijahalalishwa(kulingana nataratibu zetu sisi wtz pengine na afrika kwa ujumla) swala la talaka litakuwepo?
    Pengine labda tujaribu kuangalia nchi za wenzetu wanapotaka kuingia ktk maisha ya ndoa huwa wanahalalisha kwa namna gani, au kama huwa hawana utaratibu wa kuhalalisha ,pia tujue.Wale mlioko mamtoni kazi kwenu.

    JibuFuta
  10. bwaya, nimesema labda kutokana na ukweli kwamba mitizamo yetu haiendani. unaonekana kuwa mwanadini mzuri wakati mimi najitahidi kutokufungwa na upande wowote na ndio maana nakwambia ndoa ni suala binafsi sio janamii, dini nk kwa sababu ni lazima uamue binafs harafu uende kwenye jamii. jamii haiweze kukuamulia, lazima binafsi uamue harafu uende kwa jamii kama unaona umuhimu!

    JibuFuta
  11. Kissima, Ndio suala la ndoa ni la kiutamaduni. Linafanyika kwa misingi ya kijamii. Na kwa kuwa sisi tu sehemu ya jamii, tunalazimika kuzingatia taratibu za jamii hiyo (ambayo sisi wenyewe ni sehemu yake) Hilo moja.

    Pili, kutambulika kwa ndoa ni jambo linaloihusu jamii nzima. Si jambo la watu wawili pekeyao, hata kama linaanzia kwao. Tukitaka iwe vinginevyo hapo tutakuwa tunaunda utamaduni mwingine kabisa (jambo ambalo sidhani kama ndiyo kazi ya elimu).

    Halafu kuhusu 'kuhalalishwa' unakokuzungumzia ndiyo hiyo nafasi ya jamii inayowazunguka hao wapenzi wawili. Nadhani ni kweli vilevile kuwa halali hiyo inawasaidia wawili hao.

    Kwa hiyo, kwangu mimi sidhani kama tuna haja ya kuangalia sana wanavyofanya huko ulikokuita 'mamtoni' kwa sababu kama waafrika tuna taratibu zetu zilizotofauti na za kwao. Ni wajibu wetu kuzitetea kwa nguvu zetu zote.


    Kamala, kupishana kwa mawazo ni faida. Aidha, ninachokizungumza hakihusiani na dini. Sijahusisha dini na ndoa japo najua pia dini ni sehemu ya jamii tunayoizungumzia. Msimamo wangu uko katika taratibu za jamii yetu. Kumbuka kuwa kila jamii yenye watu wanaojiamini inayo mambo (values) ya msingi ya kushikiliwa na kuendelezwa kwa faida ya wanajamii kwa ujumla wao. Mambo haya ndiyo yanayojenga jamii za kistaarabu zenye utaratibu katika utekelezaje wa mambo.

    Kusema hivi simaanishi kuwa suala la ndoa si la kibinafsi (maana ni wazi kuwa jambo hili huanzia kwenye nafsi ya mtu/watu wawili).

    Maana yangu ni kwamba hoja ya ndoa isipopelekwa kwenye jamii haiwezi kutambulika (kwetu Afrika). Na hapo si tu pale unapoona umuhimu.

    Wamagharibi kwao binafsi inamaliza yote na ndio maana unapozungumzia ngono kabla ya ndoa kimagharibi inakuwa ngumu kuamua ukweli wa mambo. Sina hakika kama nimeweza kujieleza ipasavyo.

    JibuFuta
  12. Nimefurahishwa sana na wachangiaji wote.
    Kwa mtazamo wangu suala la ndoa ni suala la kibinafsi zaidi na ni makubaliano ya wawili lakini lazima awepo wa kuanzisha suala hilo.
    Baada ya wawili hao kuelewana ndipo linapokuja suala la jamii,wawili hao watapenda watambulike na jamii kuwa sasa wanaishi pamoja.Hii inamaana kwamba utaanza kutambulisha kwa watu kwa sasa ninaishi na fulani au fulani ndiyo mwandani wangu.
    Mambo ya msikitini au kanisani au kwa mkuu wa wilaya ni kutokana na mfumo tulio nao wa kijamii,na sisi kama wana jamii kuna wakati tunalazimika kuifuata jamii kile inachokipenda.

    Amani.

    JibuFuta
  13. bwaya vitu vingine vimepitwa na wakati ujue hakuna maadili jumla ambayo kila mwanajamii analazimika kuyafuata. jamii zipo lakini wawza usizifuate. mimi sio mkristo wala muislamu japo jamii ninayoishi inafuata dini hizo mfano tu.

    mambo ya kanisani, msikitini, bomani ni ya kimali zaidi kwa sababu inalenga kumsaidia mmoja wao ndoa ikivunjika ili apate mgawo saswa

    JibuFuta
  14. Maadili ni kitu gani? Na hicho kinachoitwa maadili kinahusianaje na watu mmoja mmoja na jamii yao?

    Na kitu kinapopitwa na wakati kinakuwaje? Tunatumia vigezo gani kujua ikiwa kitu/tendo fulani limepitwa na wakati?

    JibuFuta
  15. siamni kabisa kwamba hujui kipitwacho na wakati chafananaje wala hujui mnachokiita maadili.

    pwee

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?

Pay $900? I quit blogging