Huu si udhaifu wa kiume?

WANAUME wengi wanapenda kuoa wanawake wanaowazidi sana umri. Ni nadra kukutana na mwanaume aliyezidiwa umri na mke wake.

Kama hiyo haitoshi, wanaume wengi wanapenda kuoa wanawake wenye elimu ndogo zaidi yao. Ushahidi ni wewe unayesoma hapa. Ha ha haaha!

Vilevile, wanaume wengi wanapenda kama ingewezekana, basi wapate wanawake watakaowategemea wao kiuchumi. Au wawe na ujira mdogo kuwazidi wao.

Ni mara chache sana imekuwa kinyume.

Swali: Je, hizi si dalili za kutokujiamini? Je, huu si ushahidi kwamba wanaume ni dhaifu, ndio maana wanatafuta mbinu za kujihami?

Maoni

  1. Mambo vp brother bwaya,mimi kwa mtazamo wangu nafikiri kwa sisi wanaume tunapenda kuowa wanawake tulio wazidi kiumri au kielimu,mimi sioni kama huo ni udhaifu ila tu mwanaume anataka kuendeleza ile kitu alichopewa mamlaka ya kuwa yeye ni kichwa na mwanamke atabaki kuwa mkia,kwahyo kwakufvata hyo ndio maana tunapenda kuoa wanawake tulio wazidi kiumri na kielimu,ndugu wadau ni hayo tu na kwa mtazamo wangu muwe na wakati mzuri
    barikiweni.

    JibuFuta
  2. kwani bwana shayo ngoja nikuulize,kama mwanaume kama unavyosema inabidi atumie power au mamlaka aliyonayo kuongoza mwanamke,kwamba ye ni kichwa,sasa kwa mwanamke akiwa na elimu ya juu zaidi yako,huo utawala unapotea ama?kama mwanaume yy ni kchwa from geness,inakuaje akizidiwa kiumri au kielimu na mwanamke,kichwa kinakuwa kinakatika au?na kama mwanaume tunajifanya si ni vchwa kwa mwanaume mmbona tunakuwa waoga kwa wanawake waliotuzidi? mi nadhani mzee bwwaya upo sahihi....nionavyo

    JibuFuta
  3. Kweli, kaka bwaya uliyoyaongea yapo,na yalianza zamani sana.Vizazi na vizazi vimepitia ktk hali hii.

    Mawazo haya ni potofu.Mimi naamini kuwa naweza kumwoa mwanadada aliyenizidi umri lakini si kupita kiasi na naweza kumwoa mwanadada aliyenizidi elimu.

    Itashangaza sana kama utampenda mwanadada kwa dhati alafu ukatae kumwoa ati kwa sababu amekuzidi elimu au kwa sababu amekuzidi kwa mwaka mmoja.

    Mimi nadhani huu si udhaifu wetu sisi wanatme, bali udhaifu tulionao ni kushindwa kukubali mabadiliko.Mimi nadhani hii ni mifumo ya kizamani na sisi vijana lazima tufike mahali tuweze kuyafanyia kazi yale tunayodhani hayawezi kufikirika na kuyapatia suluhisho.

    JibuFuta
  4. kwa mtizamo wangu nadhani Shayo yuko sahihi. Mimi nikiwa kama mama, sioni kama mwanaume ambaye nimemzidi ki-elimu na ki-kipata anaweza kuwa free kutoa maamuzi yake nyumbani kama kichwa cha nyuma.
    sasa mama ndo mwenye pesa wewe baba utatoa maamuzi yeyote utakavyo bila mama kua-fiki?
    Haitawezekana!!! so baba lazma awe yuko fresh kishule kuliko mama achilia mbali pesa

    JibuFuta
  5. kwa mtizamo wangu nadhani Shayo yuko sahihi. Mimi nikiwa kama mama, sioni kama mwanaume ambaye nimemzidi ki-elimu na ki-kipata anaweza kuwa free kutoa maamuzi yake nyumbani kama kichwa cha nyuma.
    sasa mama ndo mwenye pesa wewe baba utatoa maamuzi yeyote utakavyo bila mama kua-fiki?
    Haitawezekana!!! so baba lazma awe yuko fresh kishule kuliko mama achilia mbali pesa

    JibuFuta
  6. Ngoja, mnasemaje jamani. DUH!

    JibuFuta
  7. Mama anon, kama baba mwenye fedha kuliko mke ndiye mwenye sauti, na yule asiye na fedha hana sauti; na kama mwanaume kama mwanaume hajabadilika, ila kilichobadika na ile hali ya kuwa/kutokuwa na fedha, je kichwa hapo ni baba mwenyewe ama ni hela zake?

    JibuFuta
  8. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  9. Wacha nami niweke MTAZAMO hapa. Hili la umri laenda mbaali sana. Namaanisha miaka mingi iliyopita ambapo mwanamke alikuwa "akitumikishwa"kikazi na hili lilimfanya achakae na kuzeeka kabla ya mumewe. Sasa badala ya kupunguza suluba kwa wapendwa Mama zetu wanaume wakaona wa-compasate hilo kwa kuoa dogodogo ambaye akimaliza uzazi na kuanza kutegemea nguvu za wanawe, basi muonekano wake utakuwa sawa na ule wa mumewe. Kwenye kipato hapo pana issue nyingine. Mara zote aletaye kipato kikubwa (kwa namna moja ama nyingine) anakuwa na karata ya mwisho katika nini cha kufanya na pengine vipi. Hii ni hata kama ni kwa njia ya majadiliano. Na kuna ukweli kuwa kama unakuwa na last say kwa namna yoyote ile unakuwa na nguvu. Kwa hiyo kuna chembe ya alilosema Kaka Shayo.
    Lakini hii ni dhana na kwa maisha ya sasa kama mna mpangilio mzuri wa kusaka na kutumia pesa na pia hakuna suluba kama za maji, kuni, watoto, kulima na vingi, hata mke akikuzidi mbona haionekani?
    Tena kwetu sisi tubebao maboksi kuliko wake zetu nadhani ndio wakati wa kubadilika. Na kinamama nao ukikutana nao mtaani wala usijaribu kubahatisha umri wao maana wana Plastic surgeries zao zinawapunguzia muonekano mpaka muongo mzima.
    Hahahahahahahaha
    Naacha. Ila ukweli upo lakini hauna maana kwa sasa maana sote twadundulika na kwa kina mama kama akizeeka si unaingia gharama kumchongeshea ujana? Lol
    Blessings

    JibuFuta
  10. shayo anaongea kibiblia na kwa kifupi kafungwa na kitabu kimoja tu maishani!!!!

    kissima nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani lakini nilipokuwa kijana kuna binti alinikataa mara baada ya kujua kwamba ananizidi mwaka mmoja tu wa kuzaliwa!!!

    hapa kuna kitu mnakisahau nyie ehe? kesho. kwamba wanawake huzeeka kwa kasi na huishiwa na hamu ya kupenda tendo la ngono mapema wakati mwanaume huendelea kulifagilia na hivyo ili waendane, mke inabidi awe nyuma kiumri ili umri wa kuchoka ukija, wachoke wote na sio mama akikinai, baba akadodose nje, itakuwa suluba uzeeni! tupo hapoa.

    kuna wanaotafutiwa wake na kuzuiwa kuwowa chaguo lao

    JibuFuta
  11. Naona swali ni je wanaume hatujiamini au tu wadhaifu?

    Suala la umri katika kuoana pamoja na elimu ni suala muhimu sana ingawa factor muhimu ni wahusika wenyewe maana kuna akina dada akikuzidi mshahara mwanaume umepoteza utawala na utaumia hutajiamini tena, ingawa unaweza kwua si dhaifu. Umri hauna maana sana ingawa wanawake huanza mapema kuzeeka so hata kama haina maana ni vizuri mwanaume ukafikiria (sustainable)maiaka 50 ijayo itakuwaje?

    JibuFuta
  12. Naona swali ni je wanaume hatujiamini au tu wadhaifu?

    Suala la umri katika kuoana pamoja na elimu ni suala muhimu sana ingawa factor muhimu ni wahusika wenyewe maana kuna akina dada akikuzidi mshahara mwanaume umepoteza utawala na utaumia hutajiamini tena, ingawa unaweza kwua si dhaifu. Umri hauna maana sana ingawa wanawake huanza mapema kuzeeka so hata kama haina maana ni vizuri mwanaume ukafikiria (sustainable)maiaka 50 ijayo itakuwaje?

    JibuFuta
  13. Kuna ukweli safari ya ukuaji wa mwanaume na mwanamke ni tofauti tokea utotoni mpaka uzeeni.

    Msichana mwenye umri sawa na wewe kuna uwezekano aligundua kikojoleo kinamatumizi zaidi ya kukojoa kabla mvulana hujastukia.


    Hii mara nyingi huwafanya wasichana wawastukie na kuvutiwa na wavulana wakubwa kuliko wa wa umri waliolingananao pale utotoni..

    Katika safari ya ukuaji itafikia kipindi mwanamke atakaye mtoto apate mtoto la sivyo imetoka hiyo wakati lidume linaweza kudunda tu na usishangae hata kusikia Mandela kampa mimba hausigeli mwakani. Hii kitu ya kibaioloji hugeuza dainamiksi ya kitu. Halafu hapa wala sigusii maswala ya menopozi na mchango wa homoni za kiume na mbadiliko wake katika kipindi tofauti katika ukuaji.


    Nachojaribu kusema ni;
    Kuna kipindi wakati kidume unahaha, kijike wa umri wako kashatulia kwa sababu alisha haha tokea hujastukia. Kipindi unatulia yeye anataka halafu ndio pale hausiboi na muuza kigenge wanapo kuonjea. Hii mambo inasaiko.

    Umri wa Dume zima lenye mvi kutaka tena na hata kununua gari sports na kutoboa sikio ukifika, unakuta mwanamama kajichokea labda kaanza kuimba kwaya kanisani.


    Kupishana huku kupo na kulichangia kwanini ni busara mwanamke na mwanaume ni vizuri wapishane umri ingawa si lazima katika kupishana umri maana yake mwanamke ndio awe mdogo.

    Kama wewe ulishawahi kuwepo kwenye fani utastukia ni umri gani wakinamama walitaka wakushugamame.

    Na kama ni kigoli utastukia ni umri gani wa wanaume watu wazima waliokuwa washabiki wakutaka kukununulia chipsi mayayi na kutaka kukupakata kimjomba.

    Kama utachunguza utagundua kuna pateni za umri fulani ndio haya mambo hutokea na ni tofauti kwa wanaume na wanawake.


    Cha mwisho kabisa mimi naamini wanawake ndio wenye nguvu ndio maana mara nyingi hawatumii nguvu kukukubalisha .


    SI unakumbuka udhaifu wa apendaye kutumia nguvu za mabavu kusuluhisha?

    Topiki ngumu hii kuizungumzia kirahisi. Mimi binafsi napenda wanawake wakubwa na si mshabiki wa wanawake bikira:-(

    JibuFuta
  14. Kisayansi, inakubalika kwamba umri wa kuishi wa mwanamke (katika hali ya kawaida) ni mkubwa kuliko umri wa kuishi wa mwanamume. Angalia taarifa zozote za idadi ya watu utaona hilo. Au kirahisi tazama katika jamii: Wepi ni wengi, wanawake wajane ama wanaume 'wajane'?

    Kama hivyo ndivyo, hoja kwamba wanawake wanachoka upesi si ya kweli. Wanaume ndio wanaochoka haraka kuliko akina mama!

    JibuFuta
  15. KAKA BWAYA;
    NIKO HAPA KAKA
    www.ringojr.wordpress.com

    rasta hapa.

    JibuFuta
  16. Asante sana Rasta kwa kurudi tena. Ninakutembelea sasa hivi

    JibuFuta
  17. Ninachokifahamu hapa ni kwamba wanawake hulazimika kuolewa wakiwa na umri mdogo kwa sababu kuna umri fulani ukipita itakuwa ngumu sana kwake kupata mume,kwani atakuwa ameshachuja kiasi cha kukosa mvuto,(bahati mbaya sisi wanaume mbali na v4ezo vingine lkn mvuto wa wanawake pia huangaliwa)tofauti na sisi wanaume ,mwanaume wa miaka 35 anaweza kumwoa msichana wa miaka 20, ambapo mwanamke wa miaka 30 ni vigumu sana kuolewa na mwanaume wa miaka 20.

    Inapotokea bahati mwanadada wa umri mkubwa sana kuolewa na mwanaume mwenye umri mdogo,swala la mapenzi litategemea na wao wanapendana kwa kiasi gani.

    Hata wanaume kuna umri ukifika huwa tunachoka.Sasa kama mwanaume atachoka alafu mwanamke ndio mbichi kabisa,itakuwaje hapa wadau? Hamuoni kuwa huyu dada atakuwa anakosa haki zake za kimsingi?

    JibuFuta
  18. jamani mimi nilikuwa nasoma tu,
    sina cha kuongeza maana naona walionitangulia wamesema mengi mpaka wamepitiliza.
    Kaka Bwaya ahsante kwa kuibua mijadala yenye kufikirisha, kwani mijadala ya namna hii huwa inaleta changamoto.

    JibuFuta
  19. Du hapa sijui hata nisimamie wapi. Cha muhimu nilichokipata ni kwamba kuna kaukweli kuwa haya yote yanafanywa na wanaume kama silaha ya kujihami.

    JibuFuta
  20. Kila rika lina mahitaji yake ya kiumri. Wanapopishana sana wapenzi kinachojitokeza ni tofauti ya mahitaji hayo ya kiumri. Matokeo yake yanaweza kuwa migogoro isiyo na ulazima. Najaribu kumjibu kisima hapo juu.

    JibuFuta
  21. Da kunademu nimempenda balaa, kaumbika sana naye kafa kaoza kwangu, anapenda kunisikiliza huyo, yeye mda wote huwa chini yangu na nimshauri mzuri sana, ila kanizidi Mkono ki umri, vp wadau nikioa kwani kuna shidaa?

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?

Pay $900? I quit blogging