Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2008

Mwaka wa malengo mahususi ndio huu

Mwaka unaishia leo. Watu wengi watakwambia jitathmini. Kuona wapi ulikosea. Wapi ulilikoroga. Wapi ulifanya vizuri na mambo kama hayo. Binafsi sioni sababu yoyote ya kufanya hivyo. Sioni sababu ya kufanya hicho kinachoitwa tathmini ya mwaka. Sababu ni kwamba hata kama ungegundua wapi ulikoharibu, huna unachoweza kufanya zaidi za kujiumiza moyo. Utaumia moyo, na historia itabaki pale pale. Maana historia ilikwisha kuandikwa. Kama ulishindwa mwaka huu, hesabu ni upepo umepita. Hata kama ungegundua wapi ulifanya vizuri, ukweli ni kwamba hayo wameshapita. Yaache yaende. Hakuna haja ya kulewa sifa zisizoweza kukusaidia leo. Siafa za jana zinabaki kuwa za jana. Huna sababu ya kuangalia nyuma. Historia haiwezi kukusaidia. Una sababu ya kuiacha ipite vile ilivyokuwa. Nionavyo mimi, huu ni wakati wa kutazama mbele. Kuwa na malengo. Usipojua unakokwenda, utaishia kokote. Wafanyakazi waangalie namna watakavoboresha utendaji wao wa kazi. Wanafunzi wajiangalie watakavyoweza kusoma kwa bidii. ...

Shule za "yeboyebo" na Mimba za utotoni

Ni ajabu na kweli. Baada ya kubaini kuwa karibu vijana wengi wanaotumia internet hapa Singida, lengo lao ni kujiridhisha na picha za ngono, kumbe lipo tatizo jingine. Mimba za utotoni. Sijafikia kuhalalisha uhusiano uliopo kati ya uangaliaji wa picha za ngono na hili la mimba. Lakini kwa mbali naanza kuhisi. Kwa sababu nimegundua pia kuwa mitaa mingi imesheheni sehemu za kuonyeshea filamu za "kikubwa" ambapo ndiko zilipo prepo za wanafunzi wengi wa shule za yeboyebo (kata). Ukweli ni kwamba siku hizi kila mwanafunzi "anafaulu" kuingia sekondari. Maana tumetoka nyakati zile za kufaulu na bado ukakosa nafasi, mpaka nyakati hizi ambapo unafeli na bado unaambiwa umefaulu. Pamoja na neema ya kufaulu, karibu kila familia ninayoitembelea hapa Singida inauguza maumivu ya binti kuzaa kabla ya wakati. Mabinti wa shule za msingi na sekondari wanapachikwa mimba (Mara nyingine na waalimu wao ambao wengi ni wale wa voda fasta). Wale walioshindwa kuendelea na masomo wanazalia ...

Nitautambuaje udhaifu nilionao?

Hivi karibuni tulijadili kwa ufupi kuhusu dhana ya ukosoaji na kusifiwa . Ninafurahi kuona namna watu wanavyotoa maoni mazuri tofauti tofauti ambayo ukiyasoma yanakupa uelewa mkubwa zaidi. Kwa hakika, maana hasa ya blogu ni majadiliano. Ule mtindo kongwe wa mwandishi kuandika kwa fikra kwamba anachokifikiria ndicho sahihi na kinachopaswa kumezwa na wasomaji, hapa si mahala pake. Blogu inatuweka karibu waandikaji na waandikiwa (ambao kimsingi inakuwa kama hawapo maana wote wanajadili kilicho mezani). Kwa hiyo, blogu ni majadiliano ndio maana binafsi sipendi kuandika kwa mtindo wa hitimisho. Hata kama mjadala utakaojitokeza unaweza usifikie hitimisho, bado huamini kuwa huko mbeleni, hitimisho husika laweza kufikiwa na wasomaji. Katika mada hiyo, kuna msomaji mmoja alinipigia tukajadili kwa muda mrefu. Ninawapongeza wasomaji wanaopenda kuendeleza mijadala tunayoianzisha katika blogu zetu hata kwa njia ya simu. Basi. Kilichojitokeza katika majadiliano hayo, ni namna tunavyoweza kuubain...

Gwamaka: Kile tusichofundishwa madarasani

Leo nilipata fursa ya kupata chakula cha mchana na rafiki yangu Gwamaka. Gwamaka ni kijana mwenye changamoto nyingi. Ukiongea naye hukosi jipya. Ni mwanaharakati, mwanafalsafa mwenye kichwa kinachofikiri. Ni msomaji mzuri wa vitabu. Na unaweza kubashiri inakuwaje ukikutana na msomaji wa vitabu kama Gwamaka. Ni lazima nikiri kuwa vitabu vingi nilivyosoma, yeye ndiye alinishawishi. Hivi sasa kaniambia anasoma kitabu kiitwacho: Why we need you rich . Ameniahidi kuwa kina mambo mazuri katika eneo la fedha. Japo sijawa msomaji mzuri wa vitabu vya "fedha" nimeshawishika kukitafuta. Kwa hiyo unaweza kuona kwa nini tukio la kukutana naye huwa na umuhimu wa aina yake kwangu. Basi. Gwamaka alipomaliza 'shule' aliamua kujikita katika shughuli binafsi. Hataki kuajiriwa. Aliwahi kuajiriwa miezi michache akaona sio. Hivi sasa yuko kwenye mchakato wa kutengeneza ofisi yake mwenyewe pale Mwenge, barabara ya Sam Nujoma. Mambo ya ujasiria mali. Kupata, kadiri ya unavyowekeza. Anayo...

Mkaribishe Koero

Naam. Idadi ya wanablogu inaongezeka. Na kila mwanablogu anakuja na mtazamao mpya. Hebu mtembelee Koero uone. Kama utakavyoona, ujio wa watu kama hawa ni wa muhimu sana. Karibu sana Koero tujadiliane.

Rariki yangu Rama muuza magazeti

Kazi ya kwanza niliyoifanya baada ya kufika Singida ni kulazimisha matangazo ya blogu zetu. nimekuwa nikibadili 'settings' kwenye kila kompyuta niliyoitumia kwa kubadili 'home page' iliyopo kuwa blogu moja wapo kati ya nyingi tulizonazo watanzania. Nimebadili badili baadhi ya kopyuta na mpaka sasa kuna kama blogu kumi hivi kama home page. Kwahiyo, kama inavyotarajiwa, kila mtumiaji wa kompyuta husika anapojaribu kuingia mtandaoni, atasalimiwa na blogu ya kiswahili. Hiyo nadhani inaongeza wigo wa blogu zetu. Nilifanya hivyo pia kwa baadhi ya miji niliyopita mwaka huu. Nadhani inasaidia kuzitangaza blogu. Ukweli ni kwamba bado matumizi ya mtandao yamekuwa zaidi katika kuandikiana barua pepe na mambo yetu yaleee niliyoyasimulia juzi. Hata ivyo naamini mabadiliko hata kama yanaonekana kwenda taratibu, bado yanakuja. Ni wajibu wetu kuyachochea. Leo nimekuja kwenye cafe nyingine. Hii kidogo iko wazi sio kama ile iliyokuwa imefunikwa gubi gubi. Kuna jamaa hapa tumekaa ka...

Singida: Here I come

Niko Singida. Baada ya kufika niliona ingefaa kupata huduma ya intaneti cafe. La haula! Nakutana na picha za ngono. Nahisi jamaa aliyekuwa akitumia kompyuta hii ndio kazi kubwa iliyomleta hapa. Uzuri, kama kweli ni uzuri, kompyuta za hapa zimewekewa uzio. Privacy. Unafanya kile unapenda bila hofu ya kuichunguliwa. Waswahili ukiwapa uhuru, ndo umeharibu kabisa. Jamaa aliyeondoka hapa ni mtu na heshima zake. Tai. Suti na vitu kama hivyo. Mtu na ofisi yake bila shaka. Sitaki kuamini kwamba ndicho alichokuwa anakifanya hapa. Ni lini net zitatumika kwa mambo ya maana, hilo ndilo twapaswa kujiuliza. Vijana wanajazana net siku hizi. Usifikiri (wengi wao) wanafanya vya maana. Ngono ndugu msomaji. Hivi hata nilitaka kuandika nini hata nimeshahau. Kwa nini ngono? Labda anajifunza lakini. Tuchukulie anajifunza. Sasa kujifunza kupi kwa picha za mnato wajameni? Mjadala hapa. Au tuwashauri wenye net waondoe uhuru? No. Hilo sio jibu. Siku hizi kuna simu. Watu "wanafaidi" mambo haya waki...

Yupi wa maana kwako: Akukosoaye ama akusifiaye?

Ipo haja kubwa ya sisi kama binadamu kuufahamu udhaifu wetu. Ni kazi ngumu ambayo watu wengi hatuipendi. Huenda ni kwa sababu ni kazi isiyoonekana kuwa na tija ya haraka haraka. Na pengine sitakosea nikisema ni zoezi linalojeruhi mtazamo wetu hasa ikiwa hatujielewi. Mtu asiyejielewa ni rahisi kuumia akiambiwa alikokosea. Hufarijika sana akisifiwa kizembe. Kwa nini iko hivi, hapo ndiko twapaswa kuanzia: Je, sifa zamsaidiaje asiyejielewa? Najua Mtambuzi ameandika mara nyingi kutusihi kuhusu kutokuutazama upande wa pili. Nakubaliana naye. Kwamba wengi wetu, hutumia muda mwingi sana kuutazama upande wa udhaifu/mapungufu waliyonayo watu wengine. Tunakuwa mafundi wa kuchambua madhaifu ya wengine. Kila kitu kinatazamwa kwa nia ya kugundua tatizo la wengine. Iwe katika haiba (personality), kazi, mafanikio nk. Ndio maana hata tunaposikia mwenzetu kaharibu mahala, twathubutu kufurahia (hata kama ni kimoyomoyo). Kutokuungalia upande wa pili, vile vile ni aina fulani ya faraja. Ni juhudi za...

Usawa wa viumbe mbele za Mungu uko wapi?

TURUDI kwenye ule mjadala wetu wa suala la Mungu ambalo bado ninalitafutia wakati mzuri zaidi. Kuna changamoto ndogo nadhani itastahili kutazamwa. Nayo inahusu usawa wa viumbe mbele za Mungu wao. Tunaamini kwamba Mungu alituumba sisi wanadamu pamoja na viumbe wengine mfano mimea pamoja na aina nyingine za wanyama. Na inavyoonekana, mbingu iko kwa ajili ya sisi wanadamu zaidi. Sasa hoja ni kwamba nafasi ya hawa viumbe wengine iko wapi katika ufalme wa mungu? Kwa sababu hatuelezwi wazi kuwa viumbe wengine watafaidikaje na umilele tunaoutarajia (sisi wanadamu) ambao tu viumbe kama wao. Jibu la haraka haraka ambalo mtu anaweza kulitoa kama majibu ni kwamba viumbe wengine hawana upeo/utashi wa kutambua. Lakini jibu hili nadhani haliwezi kuwa sahihi. Kwa sababu hebu tuchukulie mfano ng'ombe anapopelekwa machinjioni. Anapofikishwa pale, kiumbe huyu huonekana kupatwa na mfadhaiko mkubwa kiasi cha kuweza hata kubomoa uzio ushahidi kwamba anajua kinachoendelea. Kwamba kuna kundi la viumb...

Unafiki na kutokujiamini kwetu

Unafiki ni hali ya kukuficha kwa makusudi kile kilichomo mawazoni/moyoni kwa lengo la kumwonyesha mtazamaji kuwa anachokiona ndicho, wakati ukweli wa mambo ni kwamba anachokiona ni tofauti sana na uhalisia. Unafiki ni kama kuvaa gamba lisilo lako. Kubadili rangi ya mwonekano wako. Kuwa "artificial". Unafiki ni kinyume cha uhalisi. Kwamba naweza kuigiza mwonekano fulani ambao kimsingi si wangu katika hali halisi. Naweza kumtabasamulia mtu, wakati ukweli wa mambo ni kwamba ndani yangu nasikia kinyaa. Naweza tembelewa na mtu, rafiki yangu mathalani, na ukweli ni kwamba nina kazi nyingi za kufanya lakini kwa kutaka kumridhisha rafiki yangu huyo, basi namwonyesha kufurahia ujio wake ingawa moyoni (ukweli wenyewe) ni kwamba namwona kama mpotezaji mkubwa wa muda wangu.Simwambii jinsi alivyoharibu ratiba yangu. Ila usoni anaona ninavyofurahia kuja kwake kiasi kwamba anaendelea kubaki. Na hata anapoaga, naweza kumwomba aendee kubaki, kumbe moyoni nikimsema kwa kukosa kwake busara....

Kwa nini watu huongopa?

Kusema uongo ni kutokusema ukweli. Kupindisha uhalisia wa mambo, basi. Kwa namna moja ama nyingine, sisi kama binadamu tumewahi kuongopa. Tumewahi kuwaongopea marafiki. Wazazi. Waalimu wetu. Wakubwa zetu. Na watu wengine wanaotuzunguka. Na pengine tumewahi hata kujiongopea nafsi zatu wenyewe kwa namna moja ama nyingine. Na uongo huwa na sababu bila shaka. Haiwezekani kusema uongo bila sababu. Kwa sababu kwa hakika kila mtu hupenda kusema ukweli. Sasa ni kwa nini watu hudanganya hapo ndiko lilipo swali langu. Katika kulijibu swali hili, msomaji anaweza kurudi nyuma kadiri awezavyo, kukumbuka matukio yote ya uongo aliyowahi kukumbana nayo, halafu achunguze, ni kwa sababu gani alisema uongo? Alipenda kudanganya ama alilazimika? Kipi hasa kilisababisha aseme aindishe ukweli wa mambo? Je, uongo huo ulimpa faida ya nafsi ama hasara? Lakini pia kuna jambo la kukumbuka. Wapo watu ni waongo wazuri kiasi kwamba hawawezi tena kujua kuwa wao ni waongo (unakuwa mwongo mpaka unauona uongo kama...

Mawazo yako ndiyo nguvu uliyonayo

Upo uhusiano mkubwa sana baina ya namna unavyofikiri, na jinsi unavyoishi. Kushindwa kwako, hakutegemeani na nguvu yoyote ulivyonayo isipokuwa ufahamu wako. Kuanguka kwako hakutegemei maadui wengi ulionao, isipokuwa aina ya mtazamo ulionao. Kurudi nyuma kwako hakutegemei historia yoyote uliyowahi kuwa nayo, isipokuwa namna unavyoendekeza mawazo yako ya kushindwa. Naelewa kwamba panahitaji mjadala wa kina kuhusu kipi kinachomtawala mwenzie: mawazo yetu ndiyo yanayotuongoza ama ni sisi ndio tunayaongoza mawazo. Hapo inapidi tushukie penye uelewa na namna mawazo yetu yanavyojengeka vichwani mwetu. Kwa haraka haraka, nadhani, twawaza vile tulivyoviingiza ubongoni iwe kwa hiari yetu wenyewe ama pasipo hiari hiyo. Kwa maneno mengine sisi ndio watawala wa mawazo yetu. Hiyo ni kusema kwamba unavyojiona, ndivyo ulivyo. Ukijidharau, hakuna mtu atakuja kukufanyia kazi ya kukuonyesha thamani uliyonayo. Ukianza leo kujiona masikini, ni wazi kuwa akili yako itakubaliana nawe na kusema kweli, u...

Uhuru huu ni kwa ajili ya nani?

Ninaomba msamaha kama hutanielewa. Ila ninadhani jambo hili ni muhimu ukalitafakari kwa kina wakati ukisherehekea “uhuru” wa nchi yako iliyo masikini kuliko zote kusini mwa jangwa la Sahara. Hivi kweli nchi yetu ina haki ya kusherehekea hicho kilichopewa jina la “uhuru”? Uhuru maana yake ni nini? Ni kwa kiasi gani twaweza kujikagua kuona ikiwa tu huru kweli? Kama uhuru una maana ya mambo kuwa hivi yalivyo, vipi utumwa? Ni kwa kiasi gani uchumi wa nchi hii unathibitisha kuwa kweli tu “huru”? Ni kwa kiasi gani utamaduni wetu unathibitisha hicho kinachoitwa “uhuru”? Ni kwa kiasi gani? Ni kwa vipi tunaweza kujiridhisha kwamba elimu yetu inakubaliana na kelele zetu za “uhuru”? Hivi mababu zetu walipokuwa wakiusaka uhuru lengo hasa lilikuwa nini? Leo hii tunasoma Vyuo Vikuu kwa vitisho kutoka kwa wenzetu wanaofafana na sisi. Haturuhusiwi kufikiri. Elimu yenyewe imekaa mkao wa kitumwa. Tunafundishwa akademia ituondoayo katika wigo wa kuyaelewa matatizo yetu ya kila siku. Inatuondoa k...

Mpendao simu oneni

Picha

Kwa wageni: Ujumbe wa Mwenyekiti wetu

Waraka wa mwenyekiti wa Jumuiya ya wanablogu Tanzania (JUMUWATA) kwa wanablogu wote: "Wapendwa katika jina la Watanzania. Amani iwe juu yenu. Natumai wote muwazima. Hii ni kuwataarifu rasmi kuwa, baada ya kimya cha muda mrefu sana, mahangaiko ya hapa na pale na mambo mengine, hatimaye ndugu, kijana, mpiganaji, muungwana na mpigikaji mwenzenu nimerejea ulingoni. Najua kuna ambao walikuwa wangali wakinisaka katika www.msangimdogo.blogspot.com na najua kuwa kuna wale ambao watakuwa huenda ni wapya kabisa katika taarifa hizi.la nyote kwa ujumla, napenda kuwataarifu rasmi kwa, maskani yangu kwa sasa ni hapa . Kuna kitabu cha wageni pale, makala zangu zilizotangulia ambazo zilitoka katika sehemu mbalimbali nilizozurura nakadhalika. Ila hatimaye, nimeamua kutulia hapo. Nawakaribisheni sanjari na kuwaomba mwafikishie ujumbe huu Blogaz wenzenu ambao mnawafahamu, pamoja na kutiwekea taarifa hizi katika blogi zenu kwa wale watakaoweza. Mwisho kabisa, naomba wale ambao viungo vyao (link...

Dialectic thinking: Ukweli ni kinyume chake

Dialectic thinking ni nini kwa Kiswahili? Sijui. Ninahitaji msaada wa dharura wa BAKITA. Lakini wakati tunangoja fasiri fasaha, hebu, walau kwa sasa, tukubaliane kuwa dialetic thinking ni aina ya tafakuri inanyosisitiza katika migongano ya hoja. Migongano ya hoja, maana yake, ni kukubali kuhitalafiana kama namna njema ya ufikwaji wa hitimisho sahihi. Hebu na tuiangalie falsafa hii kwa mifano rahisi. Ukweli unatokana na tofauti. –tofauti hapa ikimaanisha opposite. Labda tuseme kinyume. Ukweli unatokana na kinyume cha ukweli huo. Kwamba vinyume (opposites) kwa asili hutegemeana. Hebu angalia: Unawezaje kulielewa giza kama huwezi kuuelewa mwanga? Huwezi kujua kwamba unapenda kama hujawahi kuchukia. Huwezi kuielewa furaha kama hujui huzuni ikoje. Utajiri hauna maana bila umasikini? Huwezi kuwa mwerevu kama hakuna wajinga wanaokuzunguka. Uhai hauwezekani ikiwa atakuwepo mwanamke bila mwanamme. Mifano ni mingi na hata wewe ndugu msomaji unaweza kukubalina nami kwamba vitu vyote tunavyo...

Matokeo ya utafiti wa Mwaipopo

Mwaipopo, mwanablogu wa Sauti ya baragumu ameonyesha mfano wa namna wanablogu tunavyoweza kuyachunguza mambo na kisha kupata michango yenye uzito unaovutia. Mfano huu ni wa kuigwa na kila mpenda mijadala. Nataraji kwamba wasomaji watakumbuka lile swali la lugha nililokuwa nimeliuliza kuonyesha ugumu uliopo katika kulitafsiri kwenda kwenye kiingereza ambacho hakitapoteza maana. Tulipata majibu mengi. Ndipo Mwaipopo kwa msukumo wa kupenda utafiti, akafanya uchunguzi na haya ndiyo majibu yake: " Jamani sikuishia hapo. Nilikuwa nafanya kautafiti kadogo ili nije tena...Swali hili liliponitoa jasho nikaona nimuulize rafiki yangu mzungu. Nae kaiona shida. Bahati njema anajuajua kidogo Kiswahili cha kuendea kariakoo. Kama mjuavyo mimi ni linguist. Niliwahi kusoma translation course. Hili ni tatizo miongoni mwa matatizo ya fasili - maneno ama miundo yenye kuegemea katika utamaduni wa lugha husika. hata hivyo panapo nia ya kutafsiri lazima njia itafutwe. hasa ni kwa nia ya kujif...

Elimu tu inatosha kupambana na UKIMWI?

Kuna jambo la msingi la kutazama taratibu kuhusu kampeni kabambe za kupambana na UKIMWI. Kampeni hizi zinalenga kuelimisha watu kuhusu namna ya kupambana na janga hili ambalo nina hakika linamtisha kila adhaniwaye kuwa na akili timamu. Na kwa kiasi fulani elimu hii imesambaa. Watu wanayo elimu hii. Kuhusu elimu tumefanikiwa. Makofi tafadhali. We tazama barabara. Kuta. Miti. Redio. Luninga. Kila eneo mabango ya kuelimisha kupitia ujumbe wa aina tofauti tofauti. Ajabu yenyewe ni kwamba kasi ya kuenea kwa UKIMWI inazidi kasi ya kusambaza ujumbe. Na inasikitisha kwamba hata hao wanaoitwa waelimishaji, nao wanashindwa kuitumia vyema elimu hiyo kijikinga na UKIMWI. Narudia. Waelimishaji wenyewe, hawajaweza kuitumia elimu hiyo nzuri wanayoigawa kwa wanajamii. UKIMWI unawaanza wenyewe. Kwamba watu wanaojua kusoma wanapita kwenye barabara zenye mabango yenye kuonya kuhusu tabia ya ngono na kuhimiza matumizi ya kondomu, wanapanga mikakati kwenye baa yenye mango hayo hayo, wanaingia kutenda...